Hii ni zaidi ya dharula....Mwanadamu ana taabika na kudharirika. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni zaidi ya dharula....Mwanadamu ana taabika na kudharirika.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Consigliere, Aug 12, 2011.

 1. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,026
  Likes Received: 7,422
  Trophy Points: 280
  251482_267299539962265_100000466644920_1149591_3604030_n.jpg

  Ni matokeo ya tamaa ya madaraka, ung'ang'anizi na ufinyu wa fikara, uelewa na tafsiri mbovu ndivyo vinavyotupelekea wanadam kufikishana hapa. Tuweke pembeni hilo, kwa sasa kwani si muda wa kusubiri majibu ya vipimo yarudi ili kuanza kutibu tatizo bali hata Clinical observation itatosha sana kwa mazingira haya, pia tusikae au tusitende Ki-polisi bali ki-daktari, yaani kutibu bila kuhukumu.

  Watu hawawezi tena kulima, wala kufanya uzalishaji wa aina yoyote ile, hukuna muamko wowote toka viongozi wa africa, Somalia haitawaliki tena ni eneo lisilolotawalika, hakuna mamlaka rasmi pale ni eneo ambalo labda linaongoza kwa kuwa na watoto wasiowajua baba zao, na labda hata mama hana uhakika wa baba halisi wa mtoto (Matokeo ya vitendo vya kibakaji).

  Imegeuka Jehanamu ya walio hai.....familia zenye idadi kubwa ya wanawake na watoto, hii inaashiria watoto wanaachwa hai kwa kuonekana hawana madhara, na wanawake ni kwasababu ya kutimiza tamaa za kimwili za mabwana wa kivita.....wanaume wengi either wamekimbia kwa sababu katika vita hii ndiyo walengwa ili kuounguza nguvu za upande pinzani au wameuawa kwa sabababu hiyo hiyo na walio hai ni wa upande wenye nguvu wanaoendeleaza maafa hayo.

  Tunaiangalia Somalia na mambo yanayoendelea huko kana kwamba ni jambo la kinjozi na halituhusu kabisa. Heri kwenu wakulima watanzania ambao jitihada zenu za kujaza maghala ya taifa zimeisukuma na kuipa nguvu serikali yetu kuweza kutoa msaada wa tani 300......tuangalie kama tupo kwenye nafasi nzuri tusaidie zaidi, japo tuna ya kwetu mengi lakini kwa kweli ukilinganisha na ya wenzetu, hayafananishiki wala kupimika katika mzani mmoja.

  Wako wapi viongozi wa kiafrika, uko wapo umoja wa nchi huru za kiafrica?......hili ni janga la kibinaadam na linahitaji dharula hasa, sidhani kama ni busara au ni kumbukumbu nzuri kwa kizazi hiki chetu kushuhudia jamii nyingine ya mwanadamu ikifutika, kwa taabu, uchungu na aibu kama inavyotokea Somalia.
   
Loading...