Hii ni tamaa ya wazi kwa mwendo huu hautufikishi popote

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,415
21,110
Vyama vikubwa vya ngumi haswa WBC na WBO wameonyesha tamaa ya wazi wazi bila kuzingatia sheria zao walizojiwekea.

Kulikuwa kuna malalamiko ya muda mrefu kuhusu uwepo wa minor champions katika chama hicho hicho kimoja na uzito mmoja , uwepo wa champions kama regular, interim , super champions , wengi mwanzoni hawakukubaliana na suala hili kwa sababu ukichunguza kwa undani zaidi ni kama wamepanua mianya zaidi ya kukusanya ada za kumiliki mikanda.

Vile vile hawa minor champions huwa wanachaguliwa kama mandatory challenger dhidi ya super champion, vile vile super champion akishindwa kutetea mkanda wake kwa sababu zisizokuwa za msingi basi atavuliwa mkanda na hawa minor champion (mf interim champion (haswa kwa WBC) hupandishwa hadhi na kuwa the super champion.

Twende kwenye hoja husika sasa, wiki chache zilizopita kulitangazwa mapambano mawili kati ya unified heavyweight champion Anthony Joshua na Lineal &WBC heavyweight champion Tyson Fury ili apatikane Undisputed heavyweight champion as well as the New Lineal heavyweight champion.

Lakini hili pambano halitakiwi lifanyike mpaka mandatory fights zikamilike.

Kwa Anthony Joshua ana Mandatory fights mbili, moja dhidi ya Kubrat Pulev na ya pili dhidi ya Oleksandry Usyk.

Kwa Anthony Joshua hii mandatory fight dhidi ya Oleksandry Usky haina nguvu sana maana sheria ya mandatory fight , ukishapigana moja , itabidi ukae mwaka mzima ili upigane mandatory fight nyingine ,tofauti na fight za kawaida ambazo mara nyingi huwa ni miezi mitatu tu.

Hata hivyo uwezekano wa Anthony Joshua kushinda pambano lake dhidi ya Kubrat Pulev ni mdogo sana hivyo kupelekea ugumu zaidi yeye kufanikiwa kupambana pambano la Tyson Fury ili ku unify belts zote nne na kuwa Undisputed champion.

Tukija upande wa Tyson Fury, yeye ana mapambano mawili pia , ila moja tu ndio mandatory hilo jingine si mandatory fight, ana trilogy fight dhidi ya the former WBC heavyweight champion Deontay Wilder na mandatory fight dhidi ya WBC interim champion Dillian Whyte.

Lakini kwa maajabu kabisa licha ya hawa wote wawili kuwa na mandatory fights , rais wa WBO POCO Varcarcel na rais wa WBC Mauricio Suleiman wote wanataka kukiuka sheria zao na kutaka kuruhusu AJ na Tyson wapigane kabla ya kumaliza mandatory fights zao ,kisa tu tamaa ya kuingiza pesa kupitia pambano la AJ na Tyson Fury.

Upande wa Mandatory Challengers wote wamegoma mapambano yao kusogezwa mbele mpaka AJ na Tyson wamalize mapambano yao yote mawili.

Dillian Whyte amekuwa wa kwanza kupinga hilo pambano mpaka pale pambano lake dhidi ya Tyson likamilike, na kwa upande wa Oleksandry Usky naye amechachamaa apate pambano lake kwanza kabla ya hayo mapambano yao.
 
.
Screenshot_20200613-202838.jpg
 
Kipi kimekufanya useme uwezekano wa AJ kushinda dhidi ya Pulev ni mdogo?
 
Back
Top Bottom