Hii ni Serikali ya wanafunzi wa CCM muelekeo uko gizani

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,851
2,000
Tulijawa na matumaini ya kusonga mbele na kurekebisha makosa yaliyofanyika. Tatizo likaanza kwa kiongozi wetu kuamini anastahili kuunda serikali upya. Kila kitu kipya. Akatikisa mawaziri ili wajisikie wapo kwa sababu yake. Ikawa hivyo. Akakusanya washauri toka NGO, akatafuta mabalozi toka NGO. Akachukuwa wachumi toka NGO. Baraza la mawaziri likaundwa.

Hii ni serikali ya wanafunzi wa CCM kama zilivyo serikali za wanafunzi vyuoni. Watendaji wakuu ni wanafaunzi wa siasa za CCM. Samia ni mwanafunzi, haijui CCM, haijui nchi (Tanganyika), haujui muungano zaidi ya vijembe vya mitaa ya Makunduchi. Mpango ni mwanafunzi, haijui CCM, siasa hazijui. Majaliwa yuko katikati akiwa na nguvu kidogo. Hana tena bashasha ya mwanzoni akiwa na Magufuli. Waziri wa fedha, ni kituko, hajawahi fanikiwa wizara yoyote, Hajui uchumi zaidi ya vitini vya darasani, hana aibu ya kukosea, hana uangalifu, amejawa furaha ya kuteuliwa na anajua kuteuliwa kwake ni maagizo ya nani.

Hii ni serikali ya wanafunzi wanaojifunza kuongoza. Wanaojifunza kuchukuwa madaraka ya nchi. Muelekeo haunonekani ni nguvu na visasi. Mwishoni tutashuhudia wizi mkubwa kama ilivyokuwa awamu ya 4, maana walioko madarakani wanajivunia urafiki.
 

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
2,270
2,000
SI MLISEMA MAGUFURI ALIKUWA MBAYA HADI WAKUMUONDOA..SASA UNALIA NINI AU UMEKUWA SAWA NA WATU WA LIBYA
 

Mightier

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
5,755
2,000
Labda leo niwaambieni kwa Kadri mnavyoisakama CCM 24/7 msidhani kuwa ndiyo mnaibomoa bali jueni ndiyo mnaipaisha tu.

Dawa pekee ya Kuinyoosha CCM ni kwa nyie Wapinzani kubadilisha Mikakati yenu ya Siasa za Kuvizia na za Kishamba mlizonazo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom