MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 13,720
- 30,629
Watu wengi wanalaumu matajiri kutofundisha vizazi vyao namna ya kuendeleza utajiri wao hata pale wanavyoaga dunia bila kujiuliza sababu zinazosababisha hivyo.
Baada ya kutafakari nimeona UKOSEFU WA UADILIFU kwa mzazi na watoto wake inachangia pakubwa sana kwenye hilo. Matajiri wengi nchini wana upungufu mkubwa wa uadilifu kwenye kuupata utajiri.
Karibu kila tajiri wa kibongo ana siri fulani ya uhalifu alioufanya akawa tajiri. Ufisadi, ujambazi, ukwepaji kodi, madawa ya kulevya na uhalifu mwingine hufanywa sana na matajiri wengi ili kuendelea kuwa matajiri. Ili kuepuka mkono wa sheria wengi huamua kupiga kimya na kutomfundisha yeyote wakiwemo watoto wao namna alivyoupata na anavyoendeleza utajiri wao.
Kibaya ni kuwa watoto wengi hukua wakijiendea tu na kudhani maisha ni mteremko. Na wengine hudhani maisha ni ujanja ujanja.
Watanzania tujitahidi kuwa waadilifu ili kutengeneza kizazi cha waadilifu.