Hii ni Orodha ya Teuzi ambazo Mheshimiwa Magufuli kateleza naye ameshajua anatafuta jinsi ya kuwatoa

Kwanza mkuu wa nchi nakupongeza kwa kazi nzuri unayofanya mpaka sasa tuache ushabiki na misimamo we unapiga kazi kwa hali na mali na Mungu anakuona kwa Hilo,

Lakin Mkuu kuna teuzi umezifanya ambazo kwakweli haziendani na kasi yako ya utendaji na hawa hapa ndo orodha kamili ya watu ambao hawakufai kabisa

1. Happy Salum Ally
Huyu umeanza naye kinondoni kama mkuu wa wilaya lakin wajuvi wa mambo tumeona kwamba kuna tatizo katika mtu huyo,

Hakuna kazi anayofanya tofauti na kupost picha Facebook kwa kila tukio mpaka anaboa,

Nikadhani umempromote kuwa mkuu wa mkoa na kumkanya kuachana na mitandao
Kila tukio ata akiwa anamfuta makamasi mtoto wake anapost, kwa ufupi anapenda sifa kuliko uwezo wake, na kazi zake haziwezi zinampwaya,
Kinondoni mapato yalipungua Mara dufu, afya vituo vilivyokuwapo havikuendelezwa, barabara ndogo ambazo zipo chini ya almashauri hiyo hakurekrbisha chochote, changamoto za serikali za mitaa ndani ya wilaya ya kinondoni zimeongezeka , kweli hakufika hata robo ya makonda akiwa Kinondoni,


2. Charles Mwijage
Huyu ni waziri wa viwanda, kwanza anaaibisha serikali yako kwa kutaja taja mambo ambayo hayana maana katika jamii, eti vyerehani vitatu seriously ni kiwanda?

Nchi sasa ina changamoto ya sukari, cement, mafuta ya kula, na urasimu katika uanzishwaji viwanda uko pale pale, kwa kifupi hafai kabisa, ataftiwe kazi nyingine,

3. Humprey Pole pole hawezi siasa za uenezi ni bora ungemuacha wilayani,
Huyu mtu yuko makin kwenye masuala ya utendaji siyo uenezi hayawezi haya ,hajafit kwenye viatu vya Nape,

4. Kangi Lugola,
Hapa ndo nasema kwamba mzee huyu japo bado ni mapema lakin naona dalili za kufeli ndani yake na italeta shida hapo mbeleni,

5. Mzee Philip Mpango naye kwa upande wangu simuelewi nisijue wengine,

Pamoja na hiyo kuna majembe umeyateua nakupa pongezi

A. Makamu wa Rais ni mtu sahihi kabisa mama Samia Suluhu Hassan

B. Waziri Mkuu Mheshimiwa majariwa umepatia

C. Paul Makonda umepatia sana, kusema ukweli

D. Mrisho Gambo huyo umelamba dume maana ni mtu wa kazi tu hana masifa, nadhani wa Iringa ajifunze kwa huyu

E. Dr wilbroad Slaa
Huyu Mzee namuamini sana katika kila kazi ambayo huwa anakabidhiwa,

F. Kigwangalla
Mungu amponye haraka huko alipo

G. Martin Shigela, huyu anafanya kazi kimya kimya kapikwa kaiva sana, na namuona ni miongoni Mwa wakuu wa mikoa safi,

H. Mongella mkuu wa mkoa wa Mwanza, huyu anafanya kazi kufa na kupona anapigana kweli kweli, hana majigambo, nadhani wa Iringa ajifunze hapa,

Kwakweli Mungu aibariki Tanzania,
unapima upepo?
 
Na moja ni chalamila mbili Makonda ma tatu Ali happy Hawa ni mashujaa wajameni!
 
Back
Top Bottom