Hii ni Orodha ya Kazi zilizodharaulika mwanzoni lakini zikiwa na pesa nyingi

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
2,328
2,283
Miaka michache nyuma kabla ya ajira kuwa kitendawili (kuwa adimu)kuna kazi hazikupendwa kabisa japo zilikuwa na pesa nzuri sana.

1.MAMA NTILIE/BABA NTILIE.
Kwanza ilionekana kazi wanayofanya watu duni wasiokuwa na elimu. Wasiokuwa na kazi walikuwa tayari kukaa nyumbani kuliko kufanya kazi hii huku wakikubali hata kazi ya kufagia ofisini kwa ujira mdogo.
Ukweli ni kwamba ukiwa eneo zuri la biashara ukiuza chakula unaweza kuingiza faida ya 20,000 kwa siku. Ukiweka 15k kwa mwezi bei gani?

2. UKONDAKTA WA DALADALA.
Kwanza hii kazi ilionekana ya kihuni sababu ya muonekano wa makonda wenyewe na lugha zao. Vijana wasio na ajira walioogopa sababu walihofia kufharauliwa na wanawake (kukosa mademu) inakuweka bize sana hupati muda wa kufanya mambo mengine.
Ukweli ni kwamba kama ukiwa konda unaweza kulaza 20,000 bila posho yako na mshahara.
Fanya hivi kila safari moja ukatoa 1000,kwa siku una safari ngapi za kwenda na kurudi? Je utakataa hiyo kazi na kuendelea kusota nyumbani?

3. UMACHINGA:
Hii kazi iliwapa sana pesa walioiwahi kuifanya mapema, ushuhuda ni mwingi fanya utafiti mwenyewe kwa wamachinga wa zamani.vijana walioogopa sababu ya kudai hawawezi kupigia vitu debe.
Ila kuna watu walijenga na kufungua biashara kubwa sababu ya umachinga. Kwa sasa sio ishu tena sababu wamekuwa wengi mno.

4. KUKOPESA VITU MITAANI (KAZI ZA WAHA):
Hii mpaka leo inadharaulika lakini waha wanapata pesa sana. Piga hesabu ndogo tu. Mkopo wa bidhaa bei yake huwa mara mbili ya bei ya kawaida. Na baada ya mkopo lazma apitie tsh.1000 kila siku.

Tufanye kitenge kinauzwa 10,000 amekopesa kwa 20,000 kwa wateja 150. Faida ni sh. Ngap? Akipitia sh 1000 kwa watu 100 (watu 50 hawakutoa au hawakuepo nyumbani) ana bei gani? Anapata 100,000 akitoa 50,000 ya msingi anabaki na faida ya 50k!! Ni ni ndogo? Uko tayari kukaa bila kazi tena?.

Je ni kazi gani unaamini inadharaulika mtaani kwako? Itaje ili uwape fursa vijana wa kitanzania.

KUMBUKA
UKITAKA KUFANIKIWA ZAIDI JISHUSHE,NA KUJICHANGANYA
 
Hiyo mpaka leo haina pesa lakini inapigwa mpaka na wanaotoka chuo siku hizi
Mkuu unaendaga bar.Bar medi hubana chenji, hununuliwa bia kisha kuziuza, hutoa K kwa wahitaji, bei ya chini kabisa buku 5 kwa saa.
Bar medi sight nzuri wanaingiza 20+. Unamnunua bar medi, huko ndani anakwambia sijala, bia moja ya kutoa nishai na wizi mwingine wa kilaghai.
 
Back
Top Bottom