Hii ni moja ya taratibu za TRA?

TaiJike

JF-Expert Member
Dec 14, 2011
1,483
666
Habari zenu Wakuu.

Naomba kueleweshwa kama mfanyakazi wa TRA anaruhusiwa kuingia ndani ya duka la mfanyabiashara na kufanya ukaguzi wa mapato mpaka ndani ya droo ya pesa? Hii imemtokea kwa mfanyabiashara mmoja ndani ya jiji la mwanza.
 
Ndio mkuu, walishakuja kwenye duka langu wakafanya hivyo ila mimi ndio nahesabu wao wanahakikisha...
 
Ndio mkuu, walishakuja kwenye duka langu wakafanya hivyo ila mimi ndio nahesabu wao wanahakikisha...

Mkuu, hii wamekuja na mmoja kuvamia meza na kufungua droo huku mwingine akikamata daftari la mauzo na kuanza kulinganisha kati pesa na maandiko.
 
Wanayohaki yakukagua ila sio kushika hela, wanachofanya wao ni kuangalia tu
 
Ni kweli kabisa kukagua na kuhakiki ni kazi yao ila hii ya kufungua droo na kuhesabu pesa kwangu imekuwa mpya.

Thank you sana Mkuu kwa mchango wako.
 
Sheria ya kodi ya mapato (ibara ya 138) inasema hivi:

Commissioner's Access to Information
138. -(1) For the purposes of administering this Act, the Commissioner and every officer who is authorised in writing by the Commissioner –
(a) shall have -
(i) at all times during the day between 9am and 6pm and without any prior notice; and
(ii) at all other times as permitted by a search warrant granted by a district or resident magistrate's court,

full and free access to any premises, place, document or other asset;
 
Habari zenu Wakuu.

Naomba kueleweshwa kama mfanyakazi wa TRA anaruhusiwa kuingia ndani ya duka la mfanyabiashara na kufanya ukaguzi wa mapato mpaka ndani ya droo ya pesa? Hii imemtokea kwa mfanyabiashara mmoja ndani ya jiji la mwanza.

Kwan uliibiwa mkuu? kama waliacha kila kitu salama haina tatizo
 
Wanafanya hivyo kwa wafanyabiashara wachanga tu.
Mbona maduka ya wahindi hawaingii hivyo.
Wakifika pale wajichekeshe basi,wachukue chao wasepe.
We jiulize,kwanini mtu akikuambia anafanya kazi TRA unamuona anapesa?Je ni kweli miashaha yao au Deals.
Sasa kama wanakagua hizi machine za nini sasa,ndio maana hatuzitaki.
Wapo baadhi yao ni wakomoaji wa wafanyabiashara na wanataka waonekane miungu watu
 
Back
Top Bottom