Hii ni moja ya success kubwa katika kipindi cha miaka 15 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni moja ya success kubwa katika kipindi cha miaka 15

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M'Jr, Jul 13, 2012.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Moja ya mafanikio makubwa ambayo nakiri mimi mwenyewe kuyashuhudia katika kipindi hiki cha miaka 15 iliyopita ni jitihada kubwa sana katika kuimarisha sekta ya miundombinu hasa barabara. Kwa wale wenzangu na mimi tuliokuwa na akili japo kidogo ya kuona mwanzoni mwa miaka ya 90 mtakumbuka namna barabara zilivyokuwa katika hali mbaya. Kwa mfano wale wakazi wa mwanza mtanikumbusha lami ilikuwa maeneo gani maana hata mjini kwenyewe haikuwepo zaidi ya mtaa ule wa rwagasore maarufu kwa duka la Dubai Bazar enzi hizo. Lakini pia mtakumbuka safari za kutoka Mwanza kwenda Dar maeneo kama Sekenke na makeke yake. Wale wa Dar mtakumbuka wakati huo Konoike ndio walianza kazi ya kurekebisha barabara za jijini. Nakumbuka enzi hizo nasoma shule ya msingi ushindi pale Mikocheni kwenda mjini barabara ilikuwa hatari mpaka unapofika Morocco ndio unakutana na ka lami ka uzishi. Hii ni mifano michache tu inayoonyesha namna tulivyokuwa nyakati hizo.

  Ila kwa sasa naona mpaka mikoa ambayo haikuwahi kuwa na lami sasa ina lami ingawa sasa hii inazindua changamoto mpya kabisa ambazo kama hazitashughulikiwa itakuwa huko kuimarisha barabara ni kumpigia mbuzi gitaa. Kwa mfano, viwanda vingi vimekuwa magodown ya kuhifadhia bidhaa za kichina hivyo barabara hizi kutosaidia sana kuinua uchumi in terms of kusafirisha manufactured products kutoka kwenye viwanda vyetu. Kama tunataka kuendelea kuwa nchi ya walanguzi na wachuuzi basi na tuendelee lakini kuna kila namna ya wale wenye mamlaka ya kufanya transformation hasa ya kuinua manufacturing wafanye hivyo haraka.

  Ni hayo tu kwa leo nimeona at least nitoe mawazo yangu "positive" kwa serikali katika kipindi cha miaka 15 hii iliyopita
   
 2. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Wamejitahidi kwa kweli, ni sawa na Gunia la sukari baharini.......
   
 3. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa na hapo ndipo penye challenge kubwa badala ya kukaa kupigia kelele hilo wangeweka nguvu zaidi kwenye maeneo mengine ili ku supplement success hiyo
   
 4. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Unajua kinachowasumbua ni kule kuona mwanga wa mshumaa na kusahau kulitafuta Jua liko wapi. Bro umeona mradi wa barabara wa jirani zetu Kenya?
   
 5. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Nimeuona bro, unajua tatizo letu kubwa huwa tunafanya comparison kwenye yale mambo ambayo tunajua tuko mbele lakini hatutaki kuchukua yale ambayo tuko nyuma ili tufikie pale walipo wenzetu na kuzidi. We are not ready to learn na tunapoambiwa huwa tunakimbilia kusema unajua nchi yetu ni kubwa sana na bla bla bla...........

  Lakini pamoja na success niliyoisema bado pia ina challenge ya ubora, kama haitaangaliwa pia tutakuwa tunatupa pesa zetu for something that will end in 12 months
   
 6. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,927
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  pamoja na jitahada hizo nzuri bila kuimarisha reli ni kazi bure coz zinategemeana.
   
 7. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  failure storie;epa,reprinting of new currencies(batiki),offshore bank account scandals,stimulus package scandal,inflated cost of twin towers-bot,hunting blocks et al
   
 8. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tanzania bhana tunasifia mshumaaa kwenye giza totoro eti kisa unatoa mwanga
   
 9. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Shida ya watu wenye mawazo finyu ufikiri kiduchu, Nchi yetu Tanzania inaweza kufanya maajabu ya dunia kwa sababu ya utajiri wake, Katika Africa inaweza kuwa nchi ya pili au ya tatu. Sasa shida yetu watu wanalinganisha nchi yetu na nchi maskini, Kenya ni nchi maskini sana kwa utajiri, wamepiga hatua sana kwa sababu ya watu wenye akili nzuri , lkn sisi licha ya kuwa na mali nyingi tupo kwenye mfumo wa magamba tumelala . Tungejua potential yetu mbona tunaweza kuiweka nchi hii mahali pa ajabu sana
   
Loading...