Hii ni miongoni mwa sababu ya utume kushuka kwa wingi kwa watu weupe

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,192
15,892
Usione kama tumeonewa sisi watu weusi kutoshushwa mitume kwetu katika nyakati nyingi kama ambavyo wameshuka kwa wenzetu weupe.Mungu mwenyewe ndo mjuzi lakini tukitumia akili zetu kutafakari tunaona mambo yafuatayo ambayo yamepelekea mitume wingi kuwa weupe.

Si unajua kazi ya Mtume ni kufikisha ujumbe wa kuonya kutokana na mabaya.? Sasa unafikiri hao watu weupe kama hawakuwa wabaya na wakatili walikuwa na sababu gani ya kupekekewa mitume?

Ili awaonye kwa lipi na hali wao wameshakuwa wasafi?

Ushawahi kumuonya mwanao kwa jambo ambalo analitii na kulifanya kila siku ? Bila shaka huwezi kumsumbua afanyee jambo ambalo analifanya na kulitii.

Basi hata mitume wanatumwa kwa watu ambao wanafanya maovu Mengiii sana ndo mana wanatumwa mitume ili wakakataze maovu hayo.

Wewe fikiria tu watu wa LUTWI wale ambao walikuwa hawawataki wanawake wao walikuwa wanawataka wanaume wenzao tena wanafanya hadharani hasaa na wanapiga duara ili kila mmoja apate na apatwe.sasa kwa mtindo kama huu kwa nini wasiteremshiwe mtume awaonye?

Africa ina historia gani ya kuwa wanyama na wafuska na wakatili kama watu weupe kama sio kuonewa na kutawaliwa tu na kufanywa watumwa?

We angalia Hostoria ya watu wa MAKKA walikuwa wanawazika watoto wao wakike wakiwa wazima wazima kwa kuogopa fedheha ya kuchekwa sasa kwa namna hii kwa nini asitumwe mtume kwenda kuwaonya?

Africa ni watu tunapokea wasikivu na ni wepesi kuamini ndiyo mana mitume walianzia huko kwa vichwa vigumu huko ili wakinyooka hao sisi wengine ni rahisi sana.

Kwa namna hii ndo mana tunaona kwamba Africa ni bara la watu ambao walikuwa mbali na ukatili ndiyo maana hawakuwa na historia ya mitume na manabii.
 
Hapo unahisi tu, lakini Allah ndie anajuwa zaidi.
Ndo mana nikasema Mungu mwenyewe ndo mjuzi.lakini tukiangalia uhalisia wa mambo waafrica tuna historia za kutisha ukilinganisha na wenzetu?
 
Africa ni watu tunapokea wasikivu na ni wepesi kuamini ndiyo mana mitume walianzia huko kwa vichwa vigumu huko ili wakinyooka hao sisi wengine ni rahisi sana.

Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi. Ikakunyakueni radi nanyi mnaangalia. Quran 2:55 yaani hasa wanaisrael dah wabishi sana
 
Umefkiria kweli mkuu,safi kuwa na mawazo fikilishi
Nikizisoma historia za watu weupe katika vitabu vya dini napata kujua kwamba kumbe wengi walitumwa kwa watu waovu ambao walikuwa na unyama na ukatili.

Si umemsoma firauni na Musaa pale misri,firauni alifanya unyama ambao haukuweza kufanya na mwafrica yeyote yule.

Hata tukiangalia kwa jicho lingine tunaona kwamba hata Mungu lengo lake kuu ni hilo kwamba watu wakipelekewa mitume ili waache mabaya..

Mfano tu.

[ T'AHA - 24 ]
Nenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepindukia mipaka.

Mwenyezimungu lengo la kumtuma Musaa kwa firauni ni kwa sababu jamaa alivuka mipaka yaani alikuwa na unyama wa hali ya juu sana.
 
Africa ni watu tunapokea wasikivu na ni wepesi kuamini ndiyo mana mitume walianzia huko kwa vichwa vigumu huko ili wakinyooka hao sisi wengine ni rahisi sana.

Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatutakuamini mpaka tumwone Mwenyezi Mungu waziwazi. Ikakunyakueni radi nanyi mnaangalia. Quran 2:55 yaani hasa wanaisrael dah wabishi sana
Yap yap Mkuu.

Mungu katuumba waafrica na neema kubwa kubwa ambazo hazifungamani na kiburi.
 
Yap yap Mkuu.

Mungu katuumba waafrica na neema kubwa kubwa ambazo hazifungamani na kiburi.

Na Allah anajua zaidi lakin ukisoma kweli historia na visa vilivyomo ndani ya Quran tunapata funzo kubwa sana umma kama za akina A'ad na Thamudi ni miuongoni mwa watu viburi sana, pamoja na neema na ishara zote lakini walikadhibisha amri za Allah
 
Naam kumbe umenipata concept yangu.
 
Kina mwamposa, mwingira, nabii mwasha, n.k ni weusi

'When you’ve been an Arsenal fan as a kid, you will be one your whole life in some way.” David Alaba
 
Back
Top Bottom