Hii ni mara ya pili Basilika la Sofia Hagia kubadilishwa kuwa msikiti

Polycarp Mdemu

Senior Member
Jun 2, 2019
165
209
HII NI MARA YA PILI BASILIKA LA SOFIA HAGIA KUBADILISHWA KUWA MSIKITI.

Mara ya Kwanza HAGIA SOPHIA lilibadilishwa kuwa msikiti mwaka 1453 na halafu kuwa makumbusho kuanzia mwaka 1934 mpaka mwaka huu tulipojuzwa litakuwa Msikiti tena.

HAGIA SOPHIA ni jina la Kigiriki la kanisa kubwa mjini Istanbul - Konstantinopoli huko Uturuki, Jina linatoka katika Kigiriki " Ἅγια Σοφία" likimaanisha (hekima takatifu) na kwa Kituruki linaitwa "Ayasofya".

Katika Historia ujenzi wa kanisa hili ulianzishwa mwaka 532 B.K na Kaisari Justiniani I aliyekuwa mtawala wa Roma ya Mashariki au tuite tu Ufalme wa Byzanti

Lengo la Jamaa huyu (Kaizari) Alitaka kuwa na kanisa (Jengo) kubwa kuliko yote duniani akafaulu kwa sababu Hagia Sofia ilikuwa ukumbi mkubwa duniani hadi mwaka 1520.

Hagia Sophia lilikamilika tu baada ya miaka mitano na Kaizari Justiniani alipoingia mara ya kwanza ndani Alisema:
"Suleimani nimekushinda", hapa alimlenga mfalme Suleimani wa Israeli ya Kale aliyejenga hekalu la Yerusalemu

Mwaka 1453 Waturuki Waislamu waliteka mji wa Konstantinopoli na kufanya mji mkuu wa Dola la Osmani

Hapo Hagia Sofia likabadilishwa kuwa msikiti na Waturuki wakatamka jina la kigiriki kama "Ayasofya".

Jengo la kanisa likaongezwa minara minne ya mtindo wa Kiislamu

Mwaka 1934 Baada ya anguko la Waosmani katika vita kuu ya kwanza ya dunia kiongozi wa taifa Kemal Atatürk akaamuru jengo liwe makumbusho, Na likawekwa kwenye Orodha ya UNESCO kama moja ya Jengo ambalo ni "Urithi Wa Dunia"

Lakini Hapo Jana Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Aliamuru kwamba Basilica La Hagia Sophia litatumika kama msikiti tena, kufuatia uamuzi kutoka kwa Baraza la Nchi, Na litafunguliwa rasmi kuanza kutumika hapo Tarehe 24 Julai mwaka huu

Mkubwa Au Baba wa Kanisa la Waorthodox, Ambao Ni Wamiliki Halali wa Jengo hili, Aligusia Uamuzi huu wa Serikal .....Patriach Bartholomew Alisema "Hagia Sophia Si tu la wamiliki wa Sasa, Ni kanisa la watu wa Ulimwengu wote, Watu wa Uturuki wana jukumu kubwa na heshima ya kufanya umoja wa jumba hili la ajabu," alisema, na kuongeza kuwa kama jumba la kumbukumbu ni kama "mahali pa ishara pa kukutana, mazungumzo, mshikamano na uelewano kati ya Ukristo na Uislamu"

Pia Patriach wa Waorthodox Wa Jiji La Moscow alisema "Kuibadilisha Hagia Sophia Kuwa Msikiti ni Dharau na Tishio kwa Wakristu"

Pia Papa Francis katika Misa ya Jumapili alisema "Ninafikiria kuhusu Hagia Sophia na nina huzuni sana".........UN pamoja na UNESCO wameonyesha kutounga mkono Mkono maamuzi haya, Lakini Raisi wa Uturuki Amedai asipofuata Maamuzi yao wenyewe inaana wazi hawapo huru juu ya Mali za nchi yao.

Kila Laheri Kwa HAGIA SOPHIA (THE MASTER PIECE) katika kazi yake mpya.... Hakika Hata wanaolitumia, Wanajua nani ni Mmiliki.

Polycarp Mdemu

27be03499f3a74f4e99d8f199348aa55.jpeg
bfa76b56bc627871cba5a5c06c7042ec.jpeg
9bdb7fac6f6f77750fc66e7cee21357e.jpeg
a5f0730de720bd64af372fabe2e63571.jpeg
34d2f6d8b614e45a8f5fd8127e599928.jpeg
5df6ec4563c0143e1e54a5ebd805499b.jpeg
 
Kubadili kanisa kuwa msikiti sio sahihi.Makanisa huwa na maluweluwe yake yatawasumbua waturuki na waislamu wanaosali humo
 
Yanakemewa sababu eneo walilopo ni takatifu hawaitajiki hivyo waondoke, na uzuri maombi yakianza tuu km pepo yupo ndani yako analipuka sababu sehemu yaliyopo sio sahihi ni pahala patakatifu. Majini wanashiriki ibada ya swala mskitini na ipo dhahiri inajulikana, ni ukwel ni uongo nijibu swali
Wapi kati ya msikitini na kanisani wanakemea mapepo?kama kanisani hakuna maluelue huwa mnakemea nn?
 
Yanakemewa sababu eneo walilopo ni takatifu hawaitajiki hivyo waondoke, na uzuri maombi yakianza tuu km pepo yupo ndani yako analipuka sababu sehemu yaliyopo sio sahihi ni pahala patakatifu. Majini wanashiriki ibada ya swala mskitini na ipo dhahiri inajulikana, ni ukwel ni uongo nijibu swali
Hivi unajua tofauti ya majini na mapepo?
 
Duuuh...hv kuna tatizo nyumba yangu nikaigeuza msikiti au kanisa...mbona wachungaji wengi wanageuza makanisa yao kuwa misikiti na wala hakuna kelele zozote.....au bar kugeuzwa nyumba ya ibada napo hatujawai kuona.

Vp wale waisraeli waliochukua ardhi kwa dhulma na mabavu na bado wanang'ang'ania ule mskiti masjid Al-Arqsa hali ya kuwa upo ktk ardh ya Palestine....je,umoja wa mataifa na mapadre hawajui hyo ni dhulma....mbona hawapanui midomo.

Kimfaacho mtu chake,Kama inauma pindueni dola mlifanye kanisa
 
Kupindua Dola ni Dakika mbili,
 
Back
Top Bottom