Hii ni Made in Tanzania tu!

Mitomingi

Senior Member
Jan 15, 2008
130
0
Hii ni Made in Tanzania tu!

Januari 23, 2008


JOHN Nolan, yule raia wa Ireland aliyejaribu kuighilibu Serikali ya Tanzania imruhusu aanzishe mashamba ya kamba (prawns) ambayo yangeiharibu kabisa Delta ya Rufiji, alipata kuliambia gazeti moja la Uingereza kwamba kati ya nchi za "ajabu" alizopata kuishi ni Tanzania.

Nolan aliliambia gazeti hilo ya kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Mzungu anaweza kuingia akiwa na dola tano tu mfukoni na akaondoka miaka mitano baadaye akiwa milionea!

Alitoa mfano wa yeye mwenyewe kwamba aliingia Tanzania akiwa hana kitu, lakini ‘akatengeneza pesa' akiwa katika chumba chake cha hoteli kutokana na dili walizochonga na viongozi ambao walimwamini kwa kuwa tu ni Mzungu!

Lakini Nolan si mgeni pekee aliyepata kuikejeli Tanzania. Mwaka jana gazeti la Mtanzania lilipata kumnukuu mwekezaji mmoja kutoka China, anayefanya biashara ya kuuza kamba na kambakochi Mashariki ya Mbali, akiikejeli Tanzania kwamba rushwa yake ni "poa".

Kwa mujibu wa Mchina huyo, ni katika Tanzania tu ambapo unaweza kumwita hakimu nyumbani kwako na kumpa rushwa ya Sh. 100,000 tu, na kisha kumpa maelekezo ya namna ya kutoa hukumu ya kesi ya mamilioni ya pesa inayokuhusu!

Lakini kama utashangaa na kutoziamini kauli hizo za Nolan na za Mchina huyo, utasemaje kuhusu hii ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuanzisha kampuni yake ya biashara (ANBEM) yeye na mkewe, mwaka 1999, akiwa bado Ikulu?. Kwa kufanya hivyo, Mkapa akawa Rais wa kwanza katika historia ya Tanzania kufanya biashara akiwa Ikulu. Historia bwana, nani hapendi kuweka historia ya ujasiriamali?

Lakini hakuishia hapo. Mwaka mmoja kabla ya kuondoka madarakani; yaani Desemba 29, 2004, Mkapa huyo huyo akashirikiana na aliyekuwa Waziri wake wa Fedha na baadaye Nishati na Madini, Daniel Yona, kusajili kampuni nyingine binafsi iitwayo Tanpower Resources Company, na akaisimamia kununua asilimia 85 ya uliokuwa mradi wa umma wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.

Lakini pia hakuishia hapo. Akautumia wadhifa wake wa urais kuhakikisha kampuni yake hiyo mpya – wakurugenzi wakiwa ni pamoja na mkewe na mtoto wake, kuingia mkataba wa kuiuzia Tanesco megawati 200 za umeme katika gridi ya taifa.

Raia wema waliohoji iwapo hakuna mgongano wa maslahi kwa Rais kufanya biashara akiwa bado Ikulu; huku akinunua kampuni ya umma (Kiwira) na kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni nyingine ya umma (Tanesco), walinyamazishwa haraka kwa kuambiwa Mkapa ni "mjasiriamali", na kwamba anaonyesha "ujasiriamali" kwa vitendo akiwa Ikulu! Upo hapo?

Kama hiyo haitoshi kukuthibitishia vioja vya Tanzania, utaielezeaje hii ya Jeetu Patel kufanikiwa kughushi na kuchota Sh. bilioni 90 kutoka Benki Kuu kwa kutumia makampuni manane tofauti aliyoyasajili?

Ilikuja ya kwanza ikachota, ikaja ya pili ikachota, ikaja ya tatu ikachota, na vivyo hivyo mpaka kampuni ya nane! Na bado Watanzania tunatakiwa tuamini kwamba hakuna aliyejua kuwa hati zilizotumiwa na makampuni hayo ni za kughushi, hadi majuzi ripoti ya ukaguzi ya Ernest & Young ilipotua mezani kwa Rais Kikwete!

Lakini kama hilo halikushangazi au kukushtua, hebu tafakari na hili jingine: Watanzania masikini wanapandishiwa umeme kwa asilimia 21 kwa sababu Tanesco iko hoi kifedha. Kwa nini iko hoi? Kwa sababu vigogo serikalini wameiingiza katika mikataba mibovu ya Richmond, IPTL na Songas.

Kwa sababu ya mikataba hiyo mibovu, Tanesco inailipa IPTL Sh. bilioni 3.3 kila mwezi, Songas Sh. bilioni 5.8 na Richmond Sh. bilioni 4.7. Kwa viwango hivvyo vya malipo, unahitaji kuwa na kampuni yenye utajiri wa Microsoft ya Bill Gates, kutotetereka kifedha. Na hivyo Tanesco ilitetereka. Ili isife, ikaamua kuongeza umeme kwa asilimia 21!
Hiyo maana yake ni nini? Hiyo maana yake ni kwamba Watanzania masikini na walalahoi wa nchi hii ndiyo "wanaobebeshwa" zigo hilo la Tanesco la kufidia gharama zilizosababishwa na vigogo serikalini za mikataba ya IPTL, Richmond na Songas. Cha kushangaza zaidi, vigogo hao waliotubebesha zigo hilo kwa kuingia mikataba hiyo mibovu, bado wanadunda mpaka leo serikalini!

Na bado wameona hiyo haitoshi. Sasa Serikali inajiandaa kuwasilisha bungeni muswada wa sheria kuziruhusu kampuni binafsi kufanya biashara ya kuuza umeme nchini. Yaani; Serikali inakuwa mstari wa mbele kulitafutia shirika lake (Tanesco) wapinzani wa kuliua kibiashara, tena inafanya hivyo ikiwa yenyewe tayari imeshalikamua hadi kuwa hoi bin taaban!

Na Tanesco ikifa na biashara hiyo ikashikwa na makampuni binafsi ya nje, (ambayo bila shaka baadhi ya vigogo nchini watakuwa na hisa), nani atayazuia yasipange bei ya pamoja ya kuuzia umeme (cartel) ili yanufaike zaidi kwa kuwakamua zaidi Watanzania? Na bado tunaambiwa kuna vita inayoendelea nchini ya kuwakomboa masikini.
Biashara ya chakula ipo mikononi mwa watu binafsi, nishati nayo sasa inawekwa mikononi mwa watu binafsi, maji nayo yataelekea huko huko …mwishowe sekta zote nyeti zinazohusu usalama wa taifa zitakuwa mikononi mwa watu binafsi hususan wageni. Tusisahau Nyerere alitabiri: "Mtabinafsisha hata Magereza."

Lakini yawezekanaje mambo yote haya yatokee nchini na umma wa Watanzania ukae kimya tu? Jibu ni kwamba ni kwa sababu Tanzania ni nchi ‘poa', nchi ya amani. Watanzania ni watu wasiotaka makuu, na ndiyo maana kina Nolan wanaamini kwamba duniani hakuna nchi kama Tanzania. Hayo aliyoyaona Nolan akiwa Tanzania ni Made in Tanzania tu. Huwezi kuyakuta kwingineko duniani!
 
ni kweli tupu,sijui tufanye nini? labda tuwape kinga ili baadaye wasituibie kama kijiji alivyosema (LOL)
 
Sijui ni mimi tu au na wenzangu pia saa nyingine nikisoma JF huwa naona tu chozi linatiririka lenyewe. Kwa mlioko nje ya nchi sasa hivi ukipita posta utawaona si chini ya 10 wakiwa wanaomba omba wengine wadogo mno na wanatia huruma. Where is their future! Wnere is our future?
 
kuna wengi wanao kuja TZ na kuondoka matajiri wakiwa kwao hawana kitu .Kuna wazamiaji wa kizungu wengi kwa kuwatumia dada zetu eti wanawaoa wako TZ ni majiri na wanafanya mambo haya behind ours sisters backs na kodi hawalipi na wanajipatia maeneo mepesa ya bure .
 
Sijui ni mimi tu au na wenzangu pia saa nyingine nikisoma JF huwa naona tu chozi linatiririka lenyewe. Kwa mlioko nje ya nchi sasa hivi ukipita posta utawaona si chini ya 10 wakiwa wanaomba omba wengine wadogo mno na wanatia huruma. Where is their future! Wnere is our future?

Inatuuma wengi mama..tena sana sana..ni masikitiko na uchungu mkubwa jinsi tunavyopelekeshwa.

Lakini nina matumani makubwa kwamba siku zao zinahesabika sasa.
 
Ama kweli waswahili wanasema "ukishangaa ya Musa utayakuta ya Firauni", hii mijitu alituwachia nyerere hii.
 
Ama kweli waswahili wanasema "ukishangaa ya Musa utayakuta ya Firauni", hii mijitu alituwachia nyerere hii.

Hebu acha kuropoka wewe, 'hii mijitu ametuachia Nyerere' unamaana gani hapa?.. Ni miaka mingapi tangu Mwl. Nyerere (RIP) aondoke? Kama kuna nia dhahiri ya kuweka mabadiliko na mapinduzi ya kiuchumi hapa nchini hata miaka mitano ni mingi. Acha kusingizia mtu kwa sababu tu hayupo kujitetea na kwa kutaka hali iliyopo iendelee hicho kikiwa kama kisingizio.

Zomba, nisingependa kulitumia neno 'kuropoka' ila kwa ulicho kisema nimelazimika kulitumia. Natumaini nimeeleweka.

SteveD.
 
Mkuu Mitomingi,
Kweli kabisa, na inatia uchungu sana, yaani sijui tuanzie wapi, maana hii haikubaliki kabisa...
 
Sijui ni mimi tu au na wenzangu pia saa nyingine nikisoma JF huwa naona tu chozi linatiririka lenyewe. Kwa mlioko nje ya nchi sasa hivi ukipita posta utawaona si chini ya 10 wakiwa wanaomba omba wengine wadogo mno na wanatia huruma. Where is their future! Wnere is our future?

Mama Lao:
Usiwe na shaka mama, maendeleo hayo yanakuja na akina Kichaka mwezi ujao Feb. kama tunavyoambiwa humu.
Tutaletewa kambi za kudumu za majeshi hapo nyumbani; dada zetu watapata ajira za kimwili, madege makubwa yanayoruka toka Marekani moja kwa moja hadi hapo Bongo bila ya kusimama popote, Watalii wa Kimarekani kwa wingi tu - kwani mashirika ya utalii yatakuwepo mengi ya wafanya biashara tokea huko majuu; na mengi mengine mazuri tu yamo njiani yanakuja.

Hao vijana uliowaona hapo posta usiwe na shaka, serikali itawajengea kambi wasitutie aibu mitaani mwetu tena. Na kama hao wanaojiona wanao uchungu wa nchi yao wanaleta fyoko, walinzi wetu wa usalama wakishirikiana na marafiki zetu wenye makambi ya kijeshi watazimwa midomo. Mkileta makelele ya 'haki za binadamu' mtapewa somo gumu msiloweza kulielewa kwa kuzungusha lugha. Mwanajeshi wa kigeni akiua, hata kwa kusudia, mahakama yenu hayana uwezo wa kumhukumu, atapelekwa nyumbani kwao akahukumiwe huko.

Kwa ujumla, Mama Lao, tujiandae kwa maendeleo haya yanayokuja kwa ari, kasi na nini? Mpya.
 
Hebu acha kuropoka wewe, 'hii mijitu ametuachia Nyerere' unamaana gani hapa?.. Ni miaka mingapi tangu Mwl. Nyerere (RIP) aondoke? Kama kuna nia dhahiri ya kuweka mabadiliko na mapinduzi ya kiuchumi hapa nchini hata miaka mitano ni mingi. Acha kusingizia mtu kwa sababu tu hayupo kujitetea na kwa kutaka hali iliyopo iendelee hicho kikiwa kama kisingizio.

Zomba, nisingependa kulitumia neno 'kuropoka' ila kwa ulicho kisema nimelazimika kulitumia. Natumaini nimeeleweka.

SteveD.

SteveD:
Hivi kweli unao mda na nguvu za kujadili na huyo ndugu? Mambo mengine huwa ni bora kuyaacha yabaki yalivyo kama hayaleti tija.
 
Sidhambi kwa Julius K.Nyerere kutuzaa sisi watu wehu, si ajbu kwake maana hata Adam kiumbe wa kwanza wa mungu alimzaa mtu katiri Kaini. Sisi sote ni mali yake hivyo sifa njema tulizo nazo ni za kwake na zile mbovu ni za kwake.
Mungu ibariki Tanzania,tunasonga mbele wananchi,haturudi nyuma.
 
Where is their future! Where is our future?

It's the matter of time. Wengine kilichotupeleka Dodoma kimetimia. Ni kuwahamasisha wabunge wazidi kuwa na moyo kwa taifa lao. The future of Tanzania is being spoiled by a few people. We'll win the battle. Only time will tell!

Invisible
 
Kwa kweli Tz nimekata tamaa nayo sio utani. Hili swala la kutukuza watu weupe ni baya sana. Tunashabikia sana tunapoona vijana wetu wakienda majuu wanarudi na wake za kizungu, basi sisi twaona kafanya kitu cha maana kulikoni, bila ya kuelewa maana ya huyu kijana mwenye akili zake timamu kwa nini aoe mzungu? Kumbe yeye amelelewa kwa kuamini kuwa mtu mwanamke mweusi si mzuri, kwa hiyo ndani ya moyo wake unakuta anaamini kabisa yeye si kitu, kwa hiyo msilaumu hao majaji wenu na viongozi wenu wanapojigonga kwa wazungu na kuwatajirisha, ni kwa sababu they are very ignorant enough kufikiria kuwa wao si bora, na lolote analosema mtu mweupe ni zuri daima.
Just a thought.
Na huyu mmarekani anayekuja jenga kambi ya jeshi huku Tz, ehe mtalia nyie, Waulizeni wajapani na wakorea wanavyolia kila siku na hao wanajeshi wa kimarekani, hawuni kweli kwel. Basi tena mwisho wa Tz naona umefika sasa.
Mbona hawakwenda popote Africa, wakaamua kuja Tz? Si unaona sasa hayo mambo ya ushamba wa Watz, hata raisi wetu mwenyewe anakubali kujengwa kwa kambi ya nchi nyingine katika ardhi ya Tz. Hii ni namna moja tu ya Marekani kutaka kuitawala dunia.
Kwa kweli sioni sababu ya Kikwete kusifiwa sasa hivi.
Basi tu ana bahati watz ni wajinga kupindukia, wanafikiria sasa hivi tu, lakini hawawazi baadaye watoto wao wataishi wapi.
Mfano mzuri ni hawa makaburu wamejaa humu Tz, na wanaleta mpaka wafanyakazi wao requirements eti ni kuongea ki-Afrikaan, hii ni Tz nani anataka kuongea Ki-Afrikaan? kama mteja ni Mtz kwa nini mhudumu awe anaongea lugha tofauti? Yaani hii ni disrespect kubwa sana kwa Tz, lakini naona ni makaburu sasa wanatukomesha kwa kuwaunga mkono South Africans wakati wa ubaguzi wa rangi, sasa ndio wanakuja kuitawala Tz taratibu tu. Sasa watanzania watalazimika kujifunza ki- China, Japanese, Afrikaan na kila lugha wazungu watakakayotaka bwana we!
check this out

MZUNGU NI MZUNGU TU UKIONDOA 'Z' INABAKI MUNGU.

Hii ndio mantra ya raisi wenu!
Nyie mwamshabikia Bush anakuja Tz. Unafikiri anakuja kufanya nini, nchi yenyewe mwaimbiwa inanuka kila siku. Mh analo analokuja lifuata nyie kaeni mkao wa kun'gon'wa. Na wazungu na tabasamu zao za dharau.
I was so upset to my stomach kumuona mwanamke mmoja bungeni marekani wakati Bush anatoa STATE OF THE UNION speech hivi majuzi. Huyo dada anatokea KCMC hospital Moshi, ni nesi hapo hospitalini, na alikuwa na mtoto wake kavaa Mink coat, eti Bush anajidai kuwa ataangamiza Malaria Tz. Kumbe anataka tu kuwakazia mbali. Hiyo malaria kaisikia leo, mbona ndio biashara kubwa ya wazungu, madawa mpaka na neti za malaria.Aache uongo wake huyu bwana yeye anataka support ya wananchi wawakubali hao wamarekani wajenge hiyo kambi ya jeshi hapo, halafu ndio watawatambua Wamarekani ni watu wa aina gani.
Huyu nesi alinishangaza sana, huko kwenda bungeni marekani ni kupumbaza watu tu, haswa watz. Kwani wazungu bado wanaamini kuwa watu weusi ni NIGGA's , akili kama za watoto wadogo ukiwapa pipi, basi you can get away with anything.
yaani nimechoka hata kufikiria huyu baba anataka nini zaidi huku Tz.
 
HII NI MADE IN TANZANIA TU!

JOHN Nolan, yule raia wa Ireland aliyejaribu kuighilibu Serikali ya
Tanzania imruhusu aanzishe mashamba ya kamba _(prawns)_ ambayo
yangeiharibu kabisa Delta ya Rufiji, alipata kuliambia gazeti moja la
Uingereza kwamba kati ya nchi za "ajabu" alizopata kuishi ni
Tanzania . Nolan aliliambia gazeti hilo ya kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee
duniani ambayo Mzungu anaweza kuingia akiwa na dola tano tu mfukoni na
akaondoka miaka mitano baadaye akiwa milionea!
Alitoa mfano wa yeye mwenyewe kwamba aliingia Tanzania akiwa hana
kitu, lakini 'akatengeneza pesa' akiwa katika chumba chake cha hoteli
kutokana na dili walizochonga na viongozi ambao walimwamini kwa kuwa
tu ni Mzungu! Lakini Nolan si mgeni pekee aliyepata kuikejeli Tanzania . Mwaka jana gazeti la Mtanzania lilipata kumnukuu mwekezaji mmoja kutoka China ,
anayefanya biashara ya kuuza kamba na kambakochi Mashariki ya Mbali,
akiikejeli Tanzania kwamba rushwa yake ni "poa".
Kwa mujibu wa Mchina huyo, ni katika Tanzania tu ambapo unaweza
kumwita, hakimu nyumbani kwako na kumpa rushwa ya Sh. 100,000 tu, na kisha
kumpa maelekezo ya namna ya kutoa hukumu ya kesi ya mamilioni ya pesa
> > inayokuhusu!
Lakini kama utashangaa na kutoziamini kauli hizo za Nolan na za Mchina
huyo, utasemaje kuhusu hii ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kuanzisha
kampuni yake ya biashara (ANBEM) yeye na mkewe, mwaka 1999, akiwa bado Ikulu?. Kwa kufanya hivyo, Mkapa akawa Rais wa kwanza katika historia
ya Tanzania kufanya biashara akiwa Ikulu. Historia bwana, nani hapendi
kuweka historia ya ujasiriamali?
Lakini hakuishia hapo. Mwaka mmoja kabla ya kuondoka madarakani; yaani
Desemba 29, 2004, Mkapa huyo huyo akashirikiana na aliyekuwa Waziri
wake wa Fedha na baadaye Nishati na Madini, Daniel Yona, kusajili kampuni
nyingine binafsi iitwayo Tanpower Resources Company, na akaisimamia
kununua, asilimia 85 ya uliokuwa mradi wa umma wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya.
Lakini pia hakuishia hapo. Akautumia wadhifa wake wa urais kuhakikisha
kampuni yake hiyo mpya - wakurugenzi wakiwa ni pamoja na mkewe na
mtoto wake, kuingia mkataba wa kuiuzia Tanesco megawati 200 za umeme
katika gridi ya taifa. Raia wema waliohoji iwapo hakuna mgongano wa maslahi kwa Rais kufanya biashara akiwa bado Ikulu; huku akinunua kampuni ya umma (Kiwira) na kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni nyingine ya umma (Tanesco), walinyamazishwa haraka kwa kuambiwa Mkapa ni "mjasiriamali" ,
na kwamba anaonyesha "ujasiriamali" kwa vitendo akiwa Ikulu!
Upo hapo? Kama hiyo haitoshi kukuthibitishia vioja vya Tanzania , utaielezeaje
hii ya Jeetu Patel kufanikiwa kughushi na kuchota Sh. bilioni 90 kutoka
Benki Kuu kwa kutumia makampuni manane tofauti aliyoyasajili?
Ilikuja ya kwanza ikachota, ikaja ya pili ikachota, ikaja ya tatu
ikachota, na vivyo hivyo mpaka kampuni ya nane! Na bado Watanzania
tunatakiwa tuamini kwamba hakuna aliyejua kuwa hati zilizotumiwa na
makampuni hayo ni za kughushi, hadi majuzi ripoti ya ukaguzi ya Ernest
& Young ilipotua mezani kwa Rais Kikwete!
Lakini kama hilo halikushangazi au kukushtua, hebu tafakari na hili
jingine: Watanzania masikini wanapandishiwa umeme kwa asilimia 21 kwa
sababu Tanesco iko hoi kifedha. Kwa nini iko hoi? Kwa sababu vigogo
serikalini wameiingiza katika mikataba mibovu ya Richmond , IPTL na
Songas. Kwa sababu ya mikataba hiyo mibovu, Tanesco inailipa IPTL Sh. bilioni 3.3 kila mwezi, Songas Sh. bilioni 5.8 na Richmond Sh.. bilioni 4.7. Kwa
viwango hivvyo vya malipo, unahitaji kuwa na kampuni yenye utajiri wa
Microsoft ya Bill Gates, kutotetereka kifedha. Na hivyo Tanesco
ilitetereka. Ili isife, ikaamua kuongeza umeme kwa asilimia 21!
Hiyo maana yake ni nini? Hiyo maana yake ni kwamba Watanzania masikini
na walalahoi wa nchi hii ndiyo "wanaobebeshwa" zigo hilo la
Tanesco la kufidia gharama zilizosababishwa na vigogo serikalini za
mikataba ya IPTL, Richmond na Songas. Cha kushangaza zaidi, vigogo hao
waliotubebesha zigo hilo kwa kuingia mikataba hiyo mibovu, bado
wanadunda mpaka leo serikalini!
Na bado wameona hiyo haitoshi. Sasa Serikali inajiandaa kuwasilisha
bungeni muswada wa sheria kuziruhusu kampuni binafsi kufanya biashara
ya kuuza umeme nchini. Yaani; Serikali inakuwa mstari wa mbele
kulitafutia shirika lake (Tanesco) wapinzani wa kuliua kibiashara, tena inafanya
hivyo ikiwa yenyewe tayari imeshalikamua hadi kuwa hoi bin taaban!
Na Tanesco ikifa na biashara hiyo ikashikwa na makampuni binafsi ya
nje,(ambayo bila shaka baadhi ya vigogo nchini watakuwa na hisa), nani
atayazuia yasipange bei ya pamoja ya kuuzia umeme _(cartel)_ ili
yanufaike zaidi kwa kuwakamua zaidi Watanzania? Na bado tunaambiwa kuna
vita inayoendelea nchini ya kuwakomboa masikini.
Biashara ya chakula ipo mikononi mwa watu binafsi, nishati nayo sasa
inawekwa mikononi mwa watu binafsi, maji nayo yataelekea huko huko
.mwishowe sekta zote nyeti zinazohusu usalama wa taifa zitakuwa
mikononi mwa watu binafsi hususan wageni. Tusisahau Nyerere alitabiri:
"Mtabinafsisha hata Magereza."
Lakini yawezekanaje mambo yote haya yatokee nchini na umma wa
Watanzania ukae kimya tu? Jibu ni kwamba ni kwa sababu Tanzania ni nchi
'poa', nchi ya amani. Watanzania ni watu wasiotaka makuu, na
ndiyo maana kina Nolan wanaamini kwamba duniani hakuna nchi kama
Tanzania Hayo aliyoyaona Nolan akiwa Tanzania ni _Made in __Tanzania__ _tu.
Huwezi kuyakuta kwingineko duniani!

nimepostiwa nami wazee

je kuna ukweli hapa?
 
Pls do not make me Cry!!!

Hii mambo unaongea wewe umeisoma kwa magazeti. Ila napenda kuwaambia wa Bongo mimi nimbahatika kufanya kazi na watu wa aina hiyo. Wameanza kazi wakiwa hawana nyuma wala mbele. Hawana utaalamu wowote. Ila sasa ni multi bilioneas. Na wanaishi Tz kwa mwavuli wa Taaluma Nyeti. Kwao walikuwa watandika vitanda vya hoteli. This is how Wabongo tunavyo endeshwa.

Lakini tujipe Moyo iko siku tutapata Kiongozi mwenye maono. Na mambo yatabadilika.
 
Wanabodi,
Hizi habari zipo ktk magazeti yetu?...
Kama hazipo basi kila gazeti, blog na tovuti zenu zibebe habari hii ili wananchi na huyo rais wapate kufahamu kwamba UOZO haupo ktk mawaziri peke yake. Kubadilisha mawaziri ama kwa lugha yangu matumizi ya Expel hayawezi kuwafukuza Kunguni waliojaa nyumbani watakacho kifanya ni kubalisha kambi mbali na hewa hiyo ambayo hadi sasa hivi wengi tunawasikia wakidai ni chafu, na sio sumu kwao.
Hivyo basi Ufagio wa chuma - ikiwa ni pamoja na ku-Freeze mali za wahujumu uchumi wote...
Kumbukeni tu kunguni wanyonyaji damu zetu hufa kwa baridi kali na sii expel (kufukuzwa kazi) ama Rungu (kifungo) - Mali zao wafilisiwe!... Waya mkali hauna wadhifa!
 
Kwani wazungu bado wanaamini kuwa watu weusi ni NIGGA's , akili kama za watoto wadogo ukiwapa pipi, basi you can get away with anything.
yaani nimechoka hata kufikiria huyu baba anataka nini zaidi huku Tz.

Wazungu walio wengi hutoa mis information ama wana exaggerate mambo kuhusu hali halisi ya nchi wanazotaka kutoa misaada. Nimewahi kuhusika kwenye fundraising event moja hapo Madison, Wisconsin kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana la shule moja ya Sekondari katika mkoa wa Arusha. Stori (narration) ya waliokuwa wanatoa presentation ambao waliwahi kufika Tanzania na wengine wameishi nchini kwa muda kama waalimu (volunteers) vilinifanya nipate hasira sana. Mambo mengi yameongezewa chumvi, na walikuwa wana potray the WORST CASE ever. Ukiangalia picha na kuwasikiliza utafikiri Tanzania bado tuko kwenye zama za mawe za kale na watu bado ni primitive pengine wana practice cannibalism. Ilinitia kichefu chefu kwa vile ndio japokuwa nchi yetu ni masikini lakini tuna umeme na maji ya bomba, na tuna internet na tunatumia compyuta za kawaida sio za mbao na kwamba tuna wanyama wa pori lakini sio mijini kama wao wanavyo potray. Kutokana na hii fundraising nimejifunza yafuatayo.
1. Ukitumia scare tactic kwamba watu wa sehemu fulani wako desperate, utaweza kuwafanya watu watoe hela bila tatizo, kusaidia hiyo cause either elimu, afya, miundo mbinu, n.k.
2. Kuna wazungu nyumbani kwao hawana deal, hawana kazi za maana, na wengine waliishia high school na hawana mbele. Wanaona njia rahisi ya kupata ujiko na kuinua maisha yao ni kwenda 3rd world countries ku save the world. Wakija huko wakawa wachafu wachafu wavaa kandambili, wakirudi kwao wanapata attention, na fedha...wengi wa hawa watu ni so incompetent.
3. Wazungu wengi (haswa Americans) hawajui geography na information za kutosha kuhusu nchi za ulimwengu wa tatu, na they don't care about it. Muda wao mwingi uko tied na maisha yao ya kibepari na namna gani wataongeza vipato chao. Kwao mzungu yeyote anayeondoka Marekani kwenda kufanya kazi nchi ya dunia ya tatu ni HERO.
4. Wazungu wengi wanaamini kuwa bado sisi especially waafrika weusi ni inferior kwenye akili zetu. Na kwamba wao ndio watakaoweza kutuongoza kwenda kwenye civilization.

Sasa basi ukiangalia hizi points zangu utakuta zina ukweli. Ni wazungu wangapi wako nchini kwetu either wanaendesha mashamba, hospitali, ama makampuni binafsi ambao ni bure tu, uozo mtupu na ni volunteer wangapi wa PEACE CORP ambao hawajui wanachofundisha mashuleni? Mimi nilikuwa na mwalimu mzungu sekondari lakini kazi yake ilikuwa ni kujipaka chaki...I learned 0 from him. Je wewe?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom