Hii ni Made in Tanzania tu!

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,472
Points
1,250

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,472 1,250
Capital Hill,
Samahani mkuu labda sijakuelewa vizuri ktk hoja yako hapo juu...
Nachoshindwa kuelewa ni pale uliposema wazungu hutumia scare tactics ku potray Africa vibaya.. sawa nakubaliana na hilo lakini ikiwa watu hawa hawana kazi na wanahitaji kazi kuja Africa ku volunteer ama vyovyote tutakavyo ita inakuwaje wayafanye hayo hali mchango wa mawazo kama hayo unaweza katisha kabisa na kuwakosesha wao kazi?

I mean ikiwa mimi ni mtoa msaada nitaogopa kutoa msaada huo ama nitamuuliza huyo mtu ikiwa huko ndivyo wanavyoishi inakuwaje wewe uwe interested kwenda fanya kazi huko ambako wanakula watu?... Hii imenipa shida kidogo.

Nadhani ndugu yangu ni bora zaidi tuachane na jinsi wao wanavyotusema ila sisi kuudhirihishia Ulimwengu kuwa tunafuta historia hizo kwa vitendo..
Binafsi naamini kuwa dunia ya leo ni kubwa sana kimawazo na Internet ni kiungo kikubwa sana kwa kila mtaalam anayetaka kufanya jambo nchini. Mtandao nyumbani ni shida wala haina kificho, kwanza ghali sana - Umeme kama ulivyoona kanyaboya la Mzee Richmonduli, Je, hao wazungu kama walitembelea Tanzania wakati ule tutasema nini..Kila nyumba Tanzania ni lazima ijengwe na Pipa la kuhifadhi maji...Generator zinawaka 24 hours kuvuta maji na pengine swala la Umeme tena mji mkuu...Mkuu infrastructure yetu mbovu sana!..

Pia, tujiulize yawezekana kuwa hawa watu wanazungumzia sehemu ambazo wanataka kuwekesha kwa mfano wako kujenga shule... Ni kweli kabisa kuna baadhi ya sehemu hazina maji wala Umeme na hakika watu wanaishi kama vile hawapo ktk dunia hii!...na ukitazama mikakati ya serikali ni ahadi za kufikia mwaka 2015...
Tanzania ya leo sio kabisa sawa na ile niliyoiacha miaka 20 iliyopita.. Kuna Visma vya maji vilijengwa na Wasweden miaka ileee ya Nyerere leo hii hayafanyi kazi kabisa, Ni sehemu kubwa ya vitongoji vya miji yetu havina Umeme hadi leo hii tena ktk miji mikubwa..

Yes, ni kweli kuwa hawa wazungu wanaongeza sana chunvi lakini Je sisi tunafanya nini kubadilisha hali kama hiyo...nafikiri ni kidogo sana!
Kilichobaki sisi tunalalamika na Wazungu tu of what they say about us!..
Mimi naamini kuwa unapoambiwa na watu kuwa wewe mchafu unanuka domo mara nyingi kuna ukweli zaidi ya uongo pamoja na kwamba ni tusi kwa aloambiwa, mtu huyo atachukia na mara zote atakosekana mtu wa karibu kumwambia mjomba kweli domo lako linatoa... Kwa hali hiyo ataendelea kuamini kuwa hanuki, Mjomba Afrika inanuka na hasa tunapojaribu kutumia deodorant bila kuoga jasho...Sasa basi maadam tunaandika ktk lugha yetu ebu tupitie machache hapa!

Maghorofa yanajengwa Dar kila siku, tena sehemu kama Kariakoo ndio zinapendeza sana machoni lakini hakuna underground sewerage system ambayo ina divert waste toka sehemu hiyo... Sasa mzungu akija sema kunanuka tunapiga makelele..hali tuhahitaji misaada mikubwa kuuzuia magonjwa kama Cholera na Maleria. Sasa kama hatutaweza kubali kuwa tunafuga maradhi hayo kwa kuambiwa kuwa sisi ni wachafu, tutaweza vipi kuamini?....Ndio majengo yanajengwa lakini with disastrous consequences kwa wananchi. Haya tazama hizo nguo - Mitumba imejaa hali ilikubaliwa kuwa ni dharura leo hii imekuwa hali halisi sasa wakitusema kweli tunaweza ficha vibanda vya Machinga vilivyojaa nchini?

Mambo mengi nyumbani yanaendeshwa kienyeji na mara nyingi tunasingizia kuwa Ati Inatosha kulingana na hali yetu!.. Hivi ni kipimo kipi hawa watu hutumia kusema Mtanzania ama mwafrika anahitaji kiasi fulani cha maendleo kuliko mzungu?...I mean kuna chakula ama nutriation za mzungu na Mwafrika!.

Mkuu, Tanzania ina mambo mengi sana ambayo ONLY in Tanzania kwa ubaya wake....we have to change na wakati ndio huu - Mimi naamini kabisa kuwa mzungu huyo alosema ni ya kweli na labda atokee mtu ku prove otherwise!...Kwani anapata kitu gani haswa kwa kusema uongo?... atawafukuza wazungu ama ndio kuwaambia matapeli wengine kuwa wajinga wapo Tanzania...
Tukubali Ujinga, na huo utakuwa mwanzo mzuri wa kutafuta tiba ya maradhi yetu.
 

Capitol Hill

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2007
Messages
733
Points
195

Capitol Hill

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2007
733 195
Capital Hill,
Samahani mkuu labda sijakuelewa vizuri ktk hoja yako hapo juu...
Nachoshindwa kuelewa ni pale uliposema wazungu hutumia scare tactics ku potray Africa vibaya..
Mkuu nimeshuhudia hawa jamaa kwa nia nzuri tu ya kukusanya hela wakipotray the worst case possible ya situation kwa wenzao wasiolewa ukweli wa mambo yanayotokea huku nyumbani kwetu. Unaomba hela ya kujenga bweni la shule ya sekondari, shule yenyewe iko maeneo ya mjini, lakini unaonyesha picha na vielelezo vingine vya ndugu zetu wa makabila ya wafugaji huko maporini, wakiwa hawana nguo, picha za watoto wanaoonekana wana starve na wenye ma inzi machoni. Unatoa wrong information kwamba wanafunzi wengi hutembea mile 10 kila siku kwenda shule na mile 10 nyingine kurudi nyumbani, na huko njiani kuna wanyama wakali, simba, chui, nyati, tembo, nk. Kwahiyo wanahitaji bweni ili wanafunzi wasitembee umbali huo kutoka vijijini kwao. Sio kutia chumvi huku?
Kama wanafanya hivi kwa vitu vidogo tu kama miradi ya ujenzi wa bweni...ni statistics ngapi zinatiwa chachandu? Kuna kipindi nilisikia katika kila watanzania 10, 6 wana HIV. Ni kweli? Sitetei majanga ya umasikini na magonjwa yaliyopo nyumbani lakini naomba ujiulize kwa nini NGO's zina BOOM especially mijini zaidi kuliko kule vijijini zinakotakiwa ziwepo ziki reach out kwa targeted audience?
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2007
Messages
4,793
Points
1,250

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2007
4,793 1,250
Ukiangalia picha na kuwasikiliza utafikiri Tanzania bado tuko kwenye zama za mawe za kale na watu bado ni primitive pengine wana practice cannibalism. Ilinitia kichefu chefu kwa vile ndio japokuwa nchi yetu ni masikini lakini tuna umeme na maji ya bomba, na tuna internet na tunatumia compyuta za kawaida sio za mbao na kwamba tuna wanyama wa pori lakini sio mijini kama wao wanavyo potray.
Mkuu, tusikatae ukweli. Hawa wazungu unaowalaumu kuwa wanatia chumvi wengi wao wameishi katika sehemu za nchi zetu ambazo sisi wasomi wazawa hatujawahi fika. Wanaishi na watu ambao sisi wazawa wasomi ni aghalabu kukutana nao. Trust me, wengi wao wanaijua Tanzania kuliko sisi tuliozaliwa humu. Tanzania si Masaki au shoprite kama ambavyo wengi tungependa. Tanzania ni huko ambako watu hawana umeme na wala hawategemei kuupatat maishani mwao, watu bado wanajengea nyasi na matope, bado simba ni tishio na wanaimani zaidi na mganga wa kienyeji kuliko daktari maana ndiye aliye karibu nao. Tanzania ambayo hawanunui bidhaa za dukani kwa vile uwezo hawana. Tanzania ambako, ndio, wengi wanategemea misaada ya hao wazungu ambao leo tunaona wanatupakazia. Sikia kichefuchefu ndugu yangu lakini kielekeze kwetu sie ambao tunaifumbia macho hali hiyo na kukazania kushindana matanuzi yasiyo na maana wala msaada kwa watanzania wenzetu. Hatuoni aibu kutumia mamilioni kwa send off, kitchen party, reception na upuuzi mwingine lakini hatutaki kumchangia aliye dhaifu katika sisi!Nikuulize, ndugu yangu, lini ulichangia upatikana wa vyandarua? Au haujui watanzania wengi hawana uwezo wa kununua chandarua? Lini ulienda kijijini kwako kujitolea utaalamu wowote ulio nao bure kwa hao watanzania wenzako? Tusiwabeze hawa kwa kufanya kile ambacho ni wajibu wetu lakini hatutaki. Au ungetaka wote wawe kama hao wakina John Nolan ambao wanasuuza ego zetu wakati wanatuibia?
 

Morani75

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2007
Messages
619
Points
0

Morani75

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2007
619 0
Mkuu Fundi, that is deep..... Unajua umenikumbusha wakati fulani miaka ya 90 kulikuwa na kampeni za kwenda kuokota takataka kule bichi na maeneo mengine na kulikuwa na watu wa kutoka Marekani nadhani walikuwa wanaitwa "Jane Goodal" (spelling??).....

Sasa kama mpaka kuokota takataka ni mpaka tuambiwe na kuongozwa na wazungu......

Nilikuwa maeneo ya kule Iringa vijijini kuna wale Peace Corps nadhani, jamani, majamaa wanafundisha mashule na wanaishi na locals, sasa humu kwenye JF kuna mtu amefanya hivyo?!?!?!

Mimi sikatai lakini baada ya kusoma post ya Fundi nadhani nitafikiria cha kufanya kule kwetu Masaini hata kununua/kuchangisha vijitabu kina YEYO na MALAYONI wakasome.....

Fundi, asante it was a wake up call to me!!!!
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2007
Messages
4,793
Points
1,250

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2007
4,793 1,250
Mkuu Fundi, that is deep..... Unajua umenikumbusha wakati fulani miaka ya 90 kulikuwa na kampeni za kwenda kuokota takataka kule bichi na maeneo mengine na kulikuwa na watu wa kutoka Marekani nadhani walikuwa wanaitwa "Jane Goodal" (spelling??).....
Jane Goodall, Mkuu.
 

Capitol Hill

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2007
Messages
733
Points
195

Capitol Hill

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2007
733 195
Fundi Mchundo...
nimekulia kwenye umasikini lakini ninamshukuru Mungu kuwa nimebarikiwa kupata elimu nzuri na kuwa na nafasi ya kuweza ku influence mabadiliko ya watanzania wengine kule nyumbani kutokea hapa nilipo. Ngoja nikupe mfano. Mwaka 2006 kupitia kanisa ninalosali (United Lutheran)tuliweza kukusanya school supplies mahitaji ya shule moja ya sekondari (Moringe Sokoine) iliyoko Monduli. Kwa kupitia Operation Bootstrap Africa (OBA) ya hapa Minneaplis tuliweza kutuma hivyo vitu vya shule kwenye container shipment kwenda Tanzania. OBA walilipia shipment.
Hapa kazini kwetu wanataka ku phase out old computer tulizo nazo (Pentium III processor) na kuzi damp. Nimeshapeleka maombi IT deparment yetu kuomba 25 of them. Hizi kompyuta japokuwa ni generation ya zamani lakini zinaweza kukidhi mahitaji kwa basic computer applications kama kufundisha word processor, spreadsheet, na zina connect kwenye internet kwa ajili ya mawasiliano, na research. Nimelipia nini katika haya..zero..lakini kazi yangu kidogo ya ku raise awareness na kunyanyua simu au kuendesha mpaka ofisi za OBA na kupata kikombe cha chai na Deanna Miller bosi wa OBA ni kidogo mno ukizingatia na kazi results ya kuwajumuisha watu wengine kwenye hii cause. ndio maana nasema nimebarikiwa kuwa kwenye nafasi ya ku influence maisha ya wengine. Kila mtu angefanya kidogo kidogo--this world would have been a very better place.
I guess I will shut up now.
 

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2007
Messages
4,793
Points
1,250

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2007
4,793 1,250
Hongera CapitolHill. Ndiyo moyo unaotakiwa. Angalau kwenu kuna umeme, ndugu yangu. Hali ni mbaya na tunahitaji mchango wa KILA mtu. Kwa tahadhari tu, pamoja na juhudi zako utasikia watu wanasema umewadharau kwa kuwapelekea mitumba, au kuna namna unafaidika katika lote hili. Usiwasikilize, wewe endelea na moyo huo. Kama wenzako nao wanavyofanya. Hongera tena.
 

Capitol Hill

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2007
Messages
733
Points
195

Capitol Hill

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2007
733 195
Fundi nashukuru kwa maneno yako mema.
Hilo la kupeleka rejects nchini nilishaambiwa. Lakini kipi ni bora kwenda uchi ama kuvaa mtumba? Ukweli mtumba ni mzuri na unakidhi haja, kama huna alternative. Mimi naona kwamba tukisema tuisubiri serikali yetu itatue matatizo yetu makubwa..tuta perish. Ngoja nikuchekeshe mkuu. Mwaka 1998-99 Kuna mzee mmoja mkulima kutoka jimbo la Montana alitaka kusaidia kutatua tatizo la maji kule Monduli. Akaship Kontena lililojaa bomba za chuma na wanakijiji wa kijiji cha Musa ambapo bomba lilikuwa lipite wakakubali kutoa labor. Na yeye akachukua muda wake kutoka kwenye biashara zake za kilimo kuja Tanzania kwa miezi 4 na ni yeye aliyekuwa na capital ya kulipa wataalamu wa idara ya maji ya wilaya. Kwani mkuu ile kazi ilifanyika basi? Kibali cha kufanya kazi hakikutoka kwa sababu wanasiasa walikuwa wanataka kuwa involved na rushwa juu. Huyu mzee alikuwa anapigwa dana dana njoo leo, njoo kesho, bosi amesafiri, mara tukutane kwa lunch. What a shame! Mzee wa watu aka give up.
 

Forum statistics

Threads 1,381,373
Members 526,066
Posts 33,797,665
Top