hii ni kwa watoto wa kishua!

The Magnificent

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
2,694
1,247
Someni, kuweni serious kwenye shule, mmepata fursa ya kuwa kwenye familia inayowasapot ipasavyo kwenye elimu halafu mnaleta upuuzi kwenye mambo muhimu. Tambueni wapo wengi wanaotamani kuwa kama nyie lakini hawawezi, inaniuma kuona mnafanya mambo ya ajabu ajabu wkt mna fursa nzuri ya kufanikiwa maishani.

Msipuuze ujumbe huu, hakika mtayakumbuka maneno yangu siku wazaz/walezi wenu watakapofariki dunia!

Kila la kheri!
 
Mmmh...ungeweka facebook ujumbe ungefika kwa wengi zaidi i think... Hapa wengi watafutaji and wanaharakati. But nways ujumbe utawafikia wahusika i guess!
<br />
<br />
naamini hata hapa wapo,hata wazaz wao wapo...wawahimize watoto wao kuwa serious na shule,sio kuwaacha free kupitiliza,hawawajengi kwa kufanya hvyo,wanawaharibia future yao2.
 
Kwanini wahangaike bwana wakati nyumbani mambo ya 'ndizi nyama' kila siku? Shule wanaenda na gari, poketi mane akichanga kwa mwezi ni mshahara wa mwalimu wa praimari, sasa mambo ya kujichosha kusoma - soma mara homuweki wapi na wapi bwana.

Subiri siku huyo mshua afe au kinuke kazini ndio huwa wanashtuka!
 
Hivi mzee wako hakiwa ana pesa au hakiwa anafanya kazi serikalini ndio unakuwa mtoto wa kishua au hakiwa Fisadi?
 
Niongeze kidogo, na wakishua mlio nje ya nchi, someni na mrudi TZ, kukaa kuaa huko nje manaacha nchi inachukuliwa na University of Dar graduates walio toka ,wakuja toka mikoani , na wakishua watoto wa mjini mbabaki kupiga picha mko LA, Chi-Town ,NY na sehemu nyingine za kighetto kuringishia mko Ulaya majuu wakati wenzenu bush star wana chukua nchi huku kilaini !
 
Ujumbe ni mzuri sana, lakini vijana wenyewe wamezibwa masikio kwa pamba nzito hawasikii, mwishoni mzazi unashindwa hata pa kuwepeleka.
 
jiulize kwa nini hapa dar kwa sasa kuna daladala zinazoenda masaki wakati zamani hazikuwepo.jibu ni kuwa wazee waliofanikiwa kujenga huko walikuwa nazo kwa sasa kwa chati nzuri au mbaya hawako tena na walisíndwa kuwakuza watoto fresh ndo hao leo h tunanapanda nao daladala.amani kwenu masharobaro
 
Back
Top Bottom