Hii ni kwa wana-CHADEMA tu

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,377
8,351
Ndugu zangu wana CHADEMA( nasisitiza ni chadema tu) matokeo ya Igunga yamenifanya nije na wazo. Huu si wakati wa sie kutulia na kuacha hili jambo linapita bila kulifanyia kazi.

Kifupi ushauri wangu harakati za chama ziendelee chini ya viongozi hapo wilayani kwa kuimarisha chama kama walivyoshauri watu wengi mikutano mijini na vijijini watu wapewe elimu ya uraia.

Kukubalika kwa CHADEMA kumenistua sana na hili jambo lisiachwe hivi hivi, mwalimu aendelee na mikutano ya kushukuru wananchi na kuendelea kuwapa taarifa wale 22000 na zaidi ambao hawaitaki CCM.

Wana CHADEMA tuwe tayari kusapport juhudi kama hizi. Maeneo mengine wameweza kwa kutumia michango toka kwa wanachama na changizo mbalimbali. Hili linawezekana wana CHADEMA tujitoe hata kwa mali ili ukombozi upatikane.

Naomba kuwasilisha
 
Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Barikiwa kwa mawazo yako mazuri.
 
ndugu zangu wana cdm( nasisitiza ni chadema tu) matokeo ya igunga yamenifanya nije na wazo.Huu si wakati wa sie kutulia na kuacha hili jambo linapita bila kulifanyia kazi.Kifupi ushauri wangu harakati za chama ziendelee chini ya viongozi hapo wilayani kwa kuimarish chama kama walivyoshauri watu wengi mikutano mijini na vijijini watu wapewe elimu ya uraia .kukubalika kwa cdm kumenistua sana na hili jambo lisiachwe hivi hivi.mwalimu aendelee na mikutano ya kushukuru wananchi na kuendelea kuwapa taarifa wale 22000 na zaidi ambao hawaitaki ccm.wana cdm tuwe tayari kusapport juhudi kama hizi. Maeneo mengine wameweza kwa kutumia michango toka kwa wanachama na changizo mbalimbali. Hili linawezekana wana cdm tujitoe hata kwa mali ili ukombozi upatikane naomba kuwasilisha

Hii imekaa njema sababu nilichokiona pia raia kutokuwa na elimu ya uraia hasa kwa kuzitambua haki zao za msingi.Vijijini elimu bado haijafika kabisa.
 
....Yah!!! Nadhani hilo ni la msingi,twende na wilaya nyingine...Lakini mpango mkakati uwe ni kuvamia vijijini maana huko ndiko kunaonekana kuna kazi sana...!!!
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Hii imekaa njema sababu nilichokiona pia raia kutokuwa na elimu ya uraia hasa kwa kuzitambua haki zao za msingi.Vijijini elimu bado haijafika kabisa.
ni kweli nimesoma habari moja ya kustua kwamba gari moja la matangazo la ccm lilikuwa likipita kwenye baadhi ya vijiji siku ya uchaguzi wakitangaza kwamba mgombea wa cdm amejitoa laiti wale wananchi wangekuwa na elimu ya uraia leo tugekuwa tunasema haya na ushahidi kamili.sijajua mstakabali wa mwalimu kuhusu ajira yake hivyo wana chadema lazima tufikirie haya sio kutulia kuja kuibukia 2015.
 
Hivi hatuwezi kumwajiri Mwalimu Kashindye kufanya hii kazi kwa mkoa mzima wa Tabora? Nadhani si ngumu kumlipa japo allowance sawa na ule mshahara na malupulupu aliyokuwa anapata wakati akiwa afisa elimu.

Tujiulizeni jamani mchango wetu ni upi katika ukombozi wa nchi hii? Wenzetu wanatumia matajiri kufadhiri chama lakini cdm haina matajiri hivyo ni sisi walalahoi tutawafadhiri cdm mpaka kieleweke.

Tunaomba viongozi wa cdm watupatie ile namba ya kutuma neno 'CHADEMA' kwenda kwenye short code ya wasp ili tuchangie kwa airtime. Ni pesa ndogo sana lakini kama kila mtu atafanya hivyo mara kwa mara anapo recharge simu yake itasaidia sana kupata kiasi fulani kikatumika kwa ajili ya Elimu ya uraia vijijini.
 
hoja zoote ni nzuri, lkn kubwa lingine ni kuwa tuwe na utaratibu wa kudumu hasa vijana, kuhamisishana kama vile tunavyojitokeza kkt kampeni , basi kwa nguvu ile ile tujiandikishe ili tuweze kuitumia haki yetu vzr, wasiwasi wangu nahisi tunapokosea ni sehemu hiyo tu, kadhalika tuwe na kampeni nyumba kwa nyumba ndugu kwa ndugu, rafiki kwa rafiki, haya magamba yanatumia saana wajumbe wa nyumba kumikumi kufanikisha ushindi na wizi pia huratibiwa na hao hao ******* zao. majitu mengine yameisha staafu lkn bado yamo. wanajua ushindi wa cdm ni safari ya wao kupelekwa mahakamani******* zao
 
kwa speed hii,cdm watapata mafanikio makubwa 2,cha msingi ni kuhakikisha elimu ya uraia iwafkie wananchi wengi zaidi hasa walioko vjjn,,
 
Naunga mkono hoja! na hii isiwe kwa igunga tuu, ifanyike kwa maeneo mbali mbali haswaa vijijini ambako kuna uelewa mdogo wa elimu ya uraia
 
Tunaweza mno kuichangia Chadema na hasa Mwalimu akafanya mambo makubwa kwa miaka 4 iliyo bakia .Hebu tujipange for sure tunaweza tufanye matendo na si maneno kwenye forum .Je hatuwezi kuchaguana hapa hapa kwenye forum na tukaanza kuratibu mambo haya ?Mfano ahadi zetu zikamwagwa hapa hapa jamvini na malipo kupelekwa mahali penye code maalumu like Igunga ili Chadema makao makuu wajue kwamba safari hii ni kuijenga Igunga ?
 
Pia vijana wengi ambao ni wanachama wa chadema hawana vitambulisho vya upiga kura hivyo haki yao ya msingi inakuwa imepotea...jambo la maana ni kuwahimiza vijana wajiandikishe kwa wingi kipindi kijacho....bila ivo hataweza kumwangusha ccm
 
viongozi wa cdm ni wa sikivu sana naimani haitakuwa mwisho bali utakuwa mwanzo wa mapambano,kwangu huo ni ushindi mkubwa kwa cdm ,tuhamasishane tujiandikishe tupige kura tufanye mageuzi
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom