Hewa mkaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2012
- 742
- 377
Kwa wafanyakazi tulio wengi, hiki kibwagizo tumekutana nacho sana. Ama kutoka kwenye vinywa vya viongozi wetu kazini au kwa wafanyakazi wenzetu wasio na maono. Kwa ufupi ujumbe wa mara kwa mara ni "kuheshimu ajira".
Wengi tumekuwa waoga kuthubutu kuacha ajira. Visingizio tunavyotumia mara kwa mara:-
1)Bado watoto wanasoma
2)Mi umri wa kustaafu bado
3)Bado sijajenga
4)Bado sijamaliza mkopo
5)Aliyenitafutia kazi atanielewaje
6)n.k
Sababu hizi zote zimeyufanya kuwa waoga na kushindwa kuanza maisha ya kujitegemea.
Lakini kwa wale waliofumba macho na kufanya maamuzi ya kujiajiri, kauki hizi hazipo tena vinywani mwao. Kauli mbiu zao ni:-
1)Mtaji mdogo
2)Riba za benki ni kubwa
3)Mikopo inasumbua
4)n.k
Kwa ufupi ukijiajiri unaachana na woga kujibembeleza kwa bosi, unajiamini na kujipangia ratiba zako we mwenyewe.
Hakuna aliyewahi kuwa tajiri kwa kutegemea mshahara na posho. Hata kama unasubiri kiinua mgongo kikubwa ni bure tu kwa sababu umri huo uwezo wa kupanga mambo kwa umakini ni mdogo.
Shime tuchangamke mapema. Achana na kazi ukiwa bado na nguvu zako. Jifunze kupanga shughuli zako za binafsi ambazo ni muhimu kuliko kazi za kuajiriwa.
Kumbuka kuwa hata kama umeajiriwa kinachomata ni "unamiliki nini cha kwako" siyo "umewahi kufanya kazi gani". Unapoumwa au kufa jamaa zako watarithi kile ulicho nacho lakini mwajiri wako atawaza namna ya kujaza nafasi yako. WASALAAM
Sent using Jamii Forums mobile app