Hii ni kwa mabingwa wa maswali ya mtego tu

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
14,376
14,864
Naanza kwa kutoa salamu kwa mabingwa wote wa maswali ya mitego
Hapo majuzi kuna jamaa yangu mmoja aliitwa kwenye usaili ili akipita aweze kuajiriwa katika kazi ya kuuza duka, katika huo usaili kwanza aliulizwa maswali kadhaa yanayohusu mahesabu ya pesa (pesa, gharama ya bidhaa na chenji nk) maswali ya aina hiyo yalikuwa 4, sasa swali la mwisho ndiyo naona kwake lilikuwa kimbembe.

Swali lenyewe ni hili:
"Amefika mteja mmoja dukani amehitaji soda na keki na umempatia na baada ya huyo mteja kumaliza kunywa kaaaga na kuondoka BILA KULIPA PESA, wewe kama muuzaji utachukua hatua gani?"

Wadau naomba jibu/majibu, Mimi nadhani hilo ni swali la mtego.
 
Hawezi kunywa soda kabla ya malipo

Swali haliko sahihi

Nitamwomba pesa kabla si/hajafungua hiyo pesa. Hivyo akiondoka jua kashalipa tayari
 
Swali la tano ni hili kutoka kwangu, Amekuja mteja dukani kwako kataka soda ya sh 600. Akatoa noti ya sh 2000
Kabla haujamludishia chenji akaja mteja mwengine akatoa 1400 na kumpa mteja wa kwanza na akaondoka ukabaki na mteja wa pili naye akahitaji soda ya sh 800 mbili na kutoa noti ya sh 5000
Mara pap kapita ombaomba akakwambia umpe 700.
Je chenji yake kwako ni sh ngapi?
 
Swali la tano ni hili kutoka kwangu,
Amekuja mteja dukani kwako kataka soda ya sh 600
Akatoa noti ya sh 2000
Kabla haujamludishia chenji akaja mteja mwengine akatoa 1400 na kumpa mteja wa kwanza na akaondoka ukabaki na mteja wa pili naye akahitaji soda ya sh 800 mbili na kutoa noti ya sh 5000
Mara pap kapita ombaomba akakwambia umpe 700.
Je chenji yake kwako ni sh ngapi?
Kwenda zako 😅
 
Huyo umbwa anaye nunua soda na halipi ni mwizi na anahujumu duka lako.

Dawa yake ni kumkumbusha akigoma anakula nakos
 
(Mjue Mwajiri wako...nature of Activities) Kama nature ya duka hilo ni Cash Sales na siyo Credit Sales, mara nyingi 'Wateja' wa biashara hiyo ni wa malipo ya kabla ya huduma "Prepaid Customers" kwahiyo ili uutegue huo mtego, itakupasa uwe na knowledge mahsusi ya nature ya duka...kw mfano, jibu la swali hilo linaweza kua 'Haitofikia hatua hiyo na mteja, kwakua kabla hajapata huduma anatakiwa ailipie kwanza!'

Nature ya malipo ya Retail businesses nyingi ni Prepaid Payments (as per mazoea ya business models). Maduka mengi, kama inavyotofautiana na biashara ya Bars and the likes, hua unalipa kwanza kabla ya kupata huduma.

Kwa mfano, jibu nililotoa hapo juu lingekua tofauti kama hiyo scenario ingetokea Bar au Pub. Wanywaji wamejijengea utamaduni wa kua walipia huduma na bidhaa baada ya matumizi na cyo kabla yake "Postpaid Customers".

Kwa, Bar au Pub ungetakiwa kuainisha Appropriate Measures as per Standard Operating Procedures at your disposal!

Kind regards'
MwanaNjilo
 
Huyo umbwa anaye nunua soda na halipi ni mwizi na anahujumu duka lako.

Dawa yake ni kumkumbusha akigoma anakula nakos


Kumbuka hilo ni swali lenye mtego (a trick question), swali la mtego halina jibu la moja kwa moja.
 
Kosa liko mwanzoni pale ulipojenga imani kwa mtu huyo kua ni mteja hivyo ukampatia hitaji lake bila kumwambia akupe pesa kwanza ukiamini kua hatakuzingua.

Na hii ina-depend kulingana na mazingira mfano kama muuzaji ni mgeni hivyo atakua amefanya uzembe na kuna haja ya kumlaumu kwasababu hana uzoefu wa kutosha na watu wa eneo hilo kiasi cha kumuamini mtu akihisi ni mteja

Lakini pia yapo mazingira ambayo ni accidential haya mazingira mtu yeyote huu msala unaweza kumkuta hata kama we ni expert.

Ni ngumu sana mazingira haya ku-escape huu msala mfano uko ofisini kwa miaka kadhaa anakuja mteja wako ambaye amekua akinunua bidhaa nyingi na zenye thamani ya juu kwenye ofisi yako na hajawahi kukopa wala kuomba discount ya bidhaa.

Mteja huyo siku hiyo akaomba juice na keki ambayo thamani yake ni chini ya 5000 huwezi ukamuambia atangulize pesa kwanza kabla ya kupewa hiyo hudumu kwasababu utakua mtu wa ajabu na kushangaza

pengine hata boss wako akishuhudia hilo anaweza kukufokea mbele yake kua unafanya uzembe ambao unaweza kufukuza wateja kwasababu unawaaminisha kwamba pamoja na bidhaa za pesa nyingi wanazonunua lakini bado kwenye hii ofisi hawaaminiki

So ikitokea sasa mteja wa aina hiyo amekunywa halafu hajalipa na kasepa ni fresh tu wala haiwezi kuhesabika kua kama hasara au kumshurutisha mshikaji kwenye mamlaka za kiserikali kua ni mwizi au tapeli
 
Swali la tano ni hili kutoka kwangu,
Amekuja mteja dukani kwako kataka soda ya sh 600
Akatoa noti ya sh 2000
Kabla haujamludishia chenji akaja mteja mwengine akatoa 1400 na kumpa mteja wa kwanza na akaondoka ukabaki na mteja wa pili naye akahitaji soda ya sh 800 mbili na kutoa noti ya sh 5000
Mara pap kapita ombaomba akakwambia umpe 700.
Je chenji yake kwako ni sh ngapi?
Nitamzingua huyo mteja, maana nitahis ni teja sasa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom