Hii ni kwa ajili ndugu Paul Christian Makonda aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa - DSM

The Palm Beach

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
528
1,037
✓Ni ajabu lakini ni kweli kuwa ndugu huyu ambaye amewahi kuwa RC maarufu sana enzi zile wa mkoa wenye watu wengi zaidi Tanzania yaani DSM analalamika kuwa anawindwa na kundi la watu ili wamuue..

✓Ndugu Makonda ukiwa RC - DSM, unatuhumiwa kuongoza kundi la UGAIDI WA KIDOLA (State Sponsored terrorism) la kuteka, kujeruhi, kuua na kupoteza wakosoaji wa sera za aliyekuwa Rais awamu ya 5 na chama chake - CCM hayati John P. Magufuli..

✓ Ukisoma posts zako huko Instagram utatambua kuwa ndg Makonda wewe bado ni mtu mwenye kiburi lakini wakati huohuo nafsi yako kwa ndani ukiwa na hofu na mashaka makubwa ya kukosa usalama yaani KIFO. Huoni kubwa na ulinzi tena uliokuwa unautegemea na unaowategemea wamekupa kisogo. Unaona giza nene mbele yako. Hulioni tumaini..!

✓Sisemi au kuandika haya ili kukuhukumu ndugu Makonda kwa kukuona ni mtu mwenye dhambi sana, mkosaji sana na huku mimi nikijihesabia haki ..... la hasha... Sina maana hiyo..!

✓Nataka kuonesha kuwa sisi ni binadamu. Wote tuna tabia moja ya kurithi tokana na ubinadamu wetu, yaani ya tabia ya kuzaliwa ya asili ya dhambi tuliyorithi kwa babu na bibi yetu Adamu na Hawa/Eva...

✓Hakuna mwenye haki hata mmoja unless tumekubali kupokea neema ya kufanywa wenye haki mbele ya Mungu kwa njia ya sadaka (tambiko/dhabihu) ya mwanae wa pekee yaani Yesu Kristo aliyemtoa afe, amwage damu msalabani miaka 2022 iliyopita ili iwe ondoleo la dhambi ya ulimwengu wote. Kumbuka dhambi ndiyo chanzo cha hofu na mashaka yetu. Dhambi ni lango la shetani la kuingilia ndani mwetu na kuleta uharibifu ikiwemo mauti yaani Kifo..

✓Kwa sababu hii, Makonda, wewe ni binadamu na unabeba tabia zote za kibinadamu za udhaifu wa kibinadamu kama ilivyo mimi na wewe. Unafanya makosa kama ambavyo kila mtu hufanya makosa. Na neema iliyo Ktk Yesu Kristo iko kwa ajili ya kila mtu apendaye na anyenyekeaye na aipokeaye..

✓Tofauti pekee tuliyonayo binadamu mmoja mmoja ni uwezo wa kuiona na kuikubali njia au neema ya wokovu iliyokwisha funuliwa kwa watu wote, yaani YESU KRISTO..

✓ Neema hii inamkalia mtu iwapo tu ataamua kuipokea kwa UNYENYEKEVU na UTII na MOYO WA SHUKRANI na kumwezesha kutii amri na maelekezo (guidelines) za Mungu zinazompa namna bora ya kuishi hapa duniani kupitia kwa Yesu Kristo Bwana na mwokozi wa watu wote, ukiwemo wewe na mimi..

✓ Nikukumbushe kubwa kuna time katika maisha, watu huwa tunakwama na kukosa msaada kabisa haijalishi tuna marafiki na utajiri wa vitu na fedha kiasi gani. Kwa wakati huo, haya yote huwa yanakuwa hayana msaada ili kuthibitisha kuwa furaha na amani na wokovu wa mtu haupo katika mali na utajiri..

✓Na Mungu huamua atuweke katika hali hiyo ngumu kimwili na kiroho (nafsi), ili yamkini tupate muda wa kumgeukia yeye na kumuona kuwa yeye ndiye pekee mwenye msaada wa kutuokoa kutoka katika mtanziko tuliomo wakati huo..

✓Ndugu yengu Makonda na wengine wenye tabia kama yako, mko Ktk hali hii. Mnahitaji msaada. Na kama mauti imefungwa kwa sasa, maana yake mna bonus ya muda wa kutengeneza mambo yenu. Maana yake mnayo neema ya Mungu, lakini tatizo lenu ni upofu wa fikra za ndani. hamuioni neema hiyo..

✓Watu wa namna hii wamejaa KIBURI cha uzima. Bado Wanawaangalia na kuwatazama wanadamu kama misaada wao. Kwamba wao ndiyo watawaokoa. Wamekosea. They are wrong. Hakuna mwanadamu hata mmoja awezaye kuondoa nguvu na hukumu ya dhambi isipokuwa mwana pekee wa Adamu - Yesu Kristo..!

✓Katika scenario hizi, naongea na Paul Christian Makonda. Namhurumia sana. Dunia na watu wote wanamhukumu. Naye anajaribu kupambana nayo kwa akili na nguvu zake mwenyewe. HAKIKA hawezi kushinda. Asipoigeuikia neema ya Mungu iliyofunuliwa kwake ktk Yesu Kristo, hakika yanayomtia hofu na mashaka, YATAMPATA SAWIA..!

✓Paul Makonda rafiki yangu, bado unakabiliwa tatizo la KIBURI. Yaani huoni kuwa wewe ni binadamu wa kawaida kabisa kama tulivyo sisi wengine na kwamba binadamu wote tunakosea na mara zote tunahitaji msaada..

✓Ndugu yangu Makonda kiuhalisia kwa sasa ulipaswa uwe umekufa. Lakini wewe Mungu anakupenda sana. Mungu bado anakupa NEEMA YA UHAI ili urekebishwe mambo yako..

✓Bahati mbaya ni kuwa umejaa KIBURI. Huonekani kutaka kujishusha na kunyenyekea kwa kukiri na kutubu makosa yako kwa Mungu muumba wako na kwa wote aliowakosea..

✓Paul Makonda uliishi maisha ya kumtegemea binadamu aliyezaliwa na mwanamke, anayekufa, kuzikwa na kisha kuoza ardhini badala ya Mungu aliye muumba na kumpa uhai. Ulianza kukosea hapo. Leo mwanadamu uliyemtegemea hayupo, kafa. Utafanyeje sasa?

✓Inasikitisha kuwa, kwa sababu ya kiburi chako, huoni kabisa kuwa upo msaada mbele yako. Bado unajaribu kujitetea kwa kujihesabia haki. Unajaribu kukwepa kuwajibika kwa makosa yako mwenyewe. Unajaribu kutwisha mzigo wa makosa yako watu wengine. Hiyo haiwezi kukusaidia. Tabia inakusindikiza kwenye mauti yako ya kimwili na kiroho. Fungua macho ya ndani ya ufahamu wako. Jiepushwe na hukumu ya Mungu iliyo mbele yako..

✓Msaada wako kwa sasa uko kwa Mungu Yehova pekee kupitia kwa Yesu Kristo, mwokozi wa ulimwengu huu na watu wote..

✓Kimbilia huko ndugu yangu Makonda. Nenda kakiri na kutubu makosa yako. Mungu atakusamehe kabisa na kukuondolea adhabu au hukumu ya dhambi zako iliyoko mbele yako..

✓ Ukifanya hivyo, nenda hatua moja mbele. Chukua ujasiri wa kuonana na wote uliowaumiza wakati ukiwa na madaraka ya kiserikali. Waambie NISAMEHENI niliwakosea. Ni ngumu lakini ndiyo njia ya kupona kwako. Huna njia nyingine..

✓Ukimaliza hatua hiyo, rudisha kila mali au vitu vya watu uliyochukua kwa nguvu Pasipo ridhaa yao wakati ule ulipokuwa na mamlaka na madaraka ya serikali..

✓ Kumbuka machozi ya uliowaumiza na kuwanyanyasa na kuwanyang'anya [kuwaibia kwa nguvu] vitu walivyovipata kwa kufanya kazi zao halali kwa sababu tu walikupinga au mlitofautiana nao yamemfikia Mungu na hayo ndiyo yanayozalisha ghadhabu ya Mungu na hasira za Mungu kuku - torment wewe..

✓Ukikubali ushauri wangu, hakika neema ya amani ya Bwana Yesu Kristo itakuwa juu yako. Utasamehewa makosa yako kabisa kama mimi nilivyosamehewa maana nilikuwa mbaya na mchafu kuliko wewe. Hakika kwa kuchukua uamuzi huu, utabaki na moja tu, kuuguza makovu ya matokeo ya dhambi za kihistoria. Ukikataa na kuendelea kubeba kiburi chako hakika Mungu anasema UTAKUFA kabisa..

Asante, NEEMA YA BWANA YESU KRISTO iwe pamoja nawe..
 

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
12,617
11,303
Inasikitisha kuwa, kwa sababu ya kiburi chake haoni kabisa kuwa upo msaada mbele yake. Msaada wake kwa sasa ni Mungu Yehova kupitia kwa Yesu Kristo.
Makonda ukimuona kanisani analia ujue kuna kitu anawinda; yeye ni mtu wa ushirikina wa majini [ urafiki wake na sheikh wa mkoa DSM] na hata akampoteza Jiwe kumpeleka kwa huyo sheikh wa mkoa waDSM akawa anawasomea kuwa wasizulike kumbe alikuwa anawapandikiza majini!!! Yakamcharukia Jiwe ndio yakampoteza halafu mnasingizia watu kuwa wamemuua!!! Muulizeni Makonda kwa yule sheikh wa Mkoa walikuwa wanakwenda kufanya nini na Jiwe? This is how Makonda blackmailed Jiwe!!!!
 

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
3,894
9,782
Makonda baada ya kufikishiwa ujumbe wa mleta mada.

giphy.gif
 

Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
17,675
18,802
✓Ukikubali ushauri wangu, hakika neema ya amani ya Bwana Yesu Kristo itakuwa juu yako. Utasamehewa kabisa na utabaki na moja tu, kuuguza makovu ya matokeo ya dhambi zako. Ukikataa na kuendelea kubeba kiburi chako hakika UTAKUFA.
Makonda ajitathmini ili aishi kwa amani.
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
11,382
14,599
Muacheni huyo jamaa ndg zangu, akiongea ana kibri, akikaa kimya anapower nyuma yake, binadamu hatuishiwi.

Mimi naona acha aongee ana haki na ni hulka ya binadamu yoyote, mzee wa ubeligiji hawezi kukaa kimya hata siku moja iwe kabla au baada, mbona hasemwi nowdays?.

Asee tuchukue jembe tukalime asee is too much!.
 

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,192
17,139
Ni ajabu na kweli kuwa huyu ndugu aliyewahi kuwa RC maarufu sana enzi zile wa mkoa wenye watu wengi zaidi Tanzania yaani DSM analalamika kuwa anawindwa na kundi la watu ili wamuu
Wewe unamzungumzia mtu aliyewahi kujiona yeye ni mungu mdogo aliyekuwa akimsaidia mungu mkubwa? Utatoa ushauri gani kwa mtu kama huyo!

Tabia ya mtu haiwezi kubadilika, inaweza kufichwa tu kwa muda, halafu inarudi palepale. Kwani vituko alivyokuwa akifanya akiwa mkuu wa mkoa ni tofauti na tabia aliyokuwa nayo kabla ya kuwa mkuu wa mkoa?

Angewezaje kumzaba vibayo mzee wa heshima kama Warioba, kama siyo mtu mwenye tabia mbaya kiasili!
 

flank

Senior Member
Jan 14, 2017
167
209
Atarudisha damu za aliyomwaga?

Ushauri wako ni mzuri kwake. Sote tunajua kuwa mwenye kutoa hukumu ya haki ni Mungu pekee. Paul yampasa atubu ili abaki mwepesi mbele ya Mungu.

Ila kwa hapa duniani yampasa akutane na adhabu kali ili iwe fundisho kwa viongozi wengine na namna hiyo. Tunajua wazi kuwa alishiriki kuuwa vijana wasio na hatia, waliotegemewa, na waliokuwa na maono mbele yao
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
12,087
12,665
Makonda ukimuona kanisani analia ujue kuna kitu anawinda; yeye ni mtu wa ushirikina wa majini [ urafiki wake na sheikh wa mkoa DSM] na hata akampoteza Jiwe kumpeleka kwa huyo sheikh wa mkoa waDSM akawa anawasomea kuwa wasizulike kumbe alikuwa anawapandikiza majini!!! Yakamcharukia Jiwe ndio yakampoteza halafu mnasingizia watu kuwa wamemuua!!! Muulizeni Makonda kwa yule sheikh wa Mkoa walikuwa wanakwenda kufanya nini na Jiwe? This is how Makonda blackmailed Jiwe!!!!
Mawazo ya kitoto sana....

Yaani unatengeneza swali lenye majibu unayotaka wewe.....

Kwanini tukuamini wewe kuwa JPM aliuawa na majini ?!!!😲🤣🤣

Wewe ni nabii wa Mwenyezi Mungu aliyekushusha na kukupa majukumu maalum ili akueleze SIRI za vifo vya watu anavyovijua yeye tu halafu uje utueleze sisi?!!!!

Isn't it INSANITY?!!!
Isn't it GRANDEUR DELUSION uliyonayo?!!!!

Pathetic

#Siempre JMT🙏
 

mzeewaSHY

JF-Expert Member
Aug 31, 2021
3,139
2,646
✓Ni ajabu na kweli kuwa huyu ndugu aliyewahi kuwa RC maarufu sana enzi zile wa mkoa wenye watu wengi zaidi Tanzania yaani DSM analalamika kuwa anawindwa na kundi la watu ili wamuue..

✓ Ukisoma posts zake huko Instagram utagundua kubwa Paul Makonda bado ni mtu mwenye kiburi na asiyeelewa maana ya unyenyekevu..

✓Sisemi au kuandika haya ili kumhukumu Paul Makonda kwa maana ya kumuona mwenye dhambi sana, mkosaji sana huku mimi nikijihesabia haki ..... la hasha... I don't mean that.!

✓Nataka kuonesha kuwa sisi ni binadamu. Wote tuna tabia moja common kwa kila mtu, kuwa, sisi wote tu wenye dhambi. Hakuna mwenye haki hata mmoja. Sisi sote kiasili ni uzao wa babu yetu mmoja - Adamu. Na kupitia Adamu dhambi iliingia kwa kila mmoja..

✓Kwa hiyo, Makonda ni binadamu na anabeba tabia zote za kibinadamu za udhaifu wa kibinadamu kama ilivyo mimi na wewe...

✓Lakini tofauti pekee tuliyonayo binadamu mmoja mmoja ni namna ya kuona njia ya kuyaepuka maisha ya dhambi za makusudi..

✓ Njia hiyo ni UNYENYEKEVU na UTII wa amri na maelekezo (guidelines) za Mungu za namna bora ya kuishi hapa duniani kupitia kwa Yesu Kristo Bwana na mwokozi wa watu wote..

✓ Kuna time ktk maisha, watu huwa tunakwama na kukosa masaada kabisa. Hata kama tuna utajiri na pesa kiasi gani, kwa wakati huo zinakuwa hazina msaada..

✓ Mfano rahisi ni kifo cha Magufuli. Huyu alikuwa Rais wa nchi. Kwa ugonjwa aliokuwa anaugua angeweza kupata matibabu popote na kwa gharama yoyote kwa sababu utajiri au pesa haikuwa tatizo ili kuahirisha kifo chake kwa wakati ule. Lakini alikufa. Why? Jibu ni KIBURI. Njia pekee kuepusha madhara kwa wengine ilikuwa lazima afe, aondoke..

✓Paul Makonda bado anakabiliwa na KIBURI. Haoni kuuwa yeye ni binadamu na binadamu huwa tunakosea. Bahati njema kuwa yeye bado ana NEEMA YA UHAI. Bahati mbaya ni kuwa haonekani kutaka kujishusha na kunyenyekea kwa kukiri na kutubu makosa yake kwa Mungu wake na kwa wote aliowakosea..

✓Paul Makonda aliishi maisha ya kumtegemea binadamu aliyezaliwa na mwanamke, anayekufa, kuzikwa na kisha kuoza ardhini badala ya Mungu aliye muumba na kumpa uhai. Leo mwanadamu aliyemtegemea hayupo, kafa. Atafanyeje sasa?

✓Inasikitisha kuwa, kwa sababu ya kiburi chake haoni kabisa kuwa upo msaada mbele yake. Anajaribu kujitetea kwa kujihesabia haki. Anajaribu kukwepa ku - take responsibility ya makosa yake. Anajaribu kutwisha mzigo watu wengine kwa makosa yake..

✓Haoni kuwa kwa sasa msaada wake ni Mungu Yehova kupitia kwa Yesu Kristo pekee..

✓Kimbilia huko ndugu yangu Makonda. Nenda kakiri na kutubu makosa yako. Mungu atakusamehe kabisa na kukuondolea adhabu au hukumu ya dhambi zako iliyoko mbele yako..

✓ Ukifanya hivyo, nenda hatua moja mbele. Chukua ujasiri wa kuonana na wote uliowaumiza wakati ukiwa na madaraka ya kiserikali. Waambie nisameheni. Kisha, rudisha kila mali ya mtu iliyoichukua kwa nguvu Pasipo ridhaa yao..

✓ Kumbuka machozi ya uliowaumiza na kuwanyanyasa kwa sababu tu walikupinga au mlitofautiana nao yamemfikkia Mungu na hayo ndiyo yanayodhalisha ghadhabu ya Mungu na kukutafuna..

✓Ukikubali ushauri wangu, hakika neema ya amani ya Bwana Yesu Kristo itakuwa juu yako. Utasamehewa kabisa na utabaki na moja tu, kuuguza makovu ya matokeo ya dhambi zako. Ukikataa na kuendelea kubeba kiburi chako hakika UTAKUFA..
Duh! Ujumbe mzito sana huu kwa Makonda na kwa watu wengine wote ambao wamekuwa na tabia za kuwaonea binaadamu wenzao na kuwadhalilisha Eti tu kwa sababu wao wana uwezo wa kufanya hivyo !! OLE WAO ! SIKU HAZIGANDI ! YOU GONNA PAY THE BIG PRICE ONE DAY !!!
 
27 Reactions
Reply
Top Bottom