kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Jaji ni mtu mkubwa na mwenye hadhi ya juu Sana katika mfumo wa Mahakama. Majaji pamoja na kuwa na hadhi ya juu pia ni watu ambao wanamajukumu mahususi na wanapaswa kufuatilia mambo nyeti kwenye kesi zinazofikishwa mbele yao. Hili kuweka heshima ya Mahakama na kuzuia Mahakama kuchezewa Jaji anapobaini Kuna watu wanafika mbele yake kwa lengo yakuidanganya Mahakama anapaswa kuchukua hatua hili watu wengine wanapofika mahakamani wawe na nidhamu na waeleze facts za ukweli kulingana na mazingira ya kile wanachokijua.
Inatia huruma na naamini majaji serious wakifuatilia kinachofanywa n Jamhuri kwenye upelekaji wa mashahidi mahakamani na ukimya wa jaji wanaumia Sana. Mahakama wakati mwingine zinapaswa kuilinda Serikali ila Serikali pamoja na kulindwa inapaswa kuonyesha kwamba ipo serious na jinai kweli ilitendeka.
Nimesikiliza maelezo ya mashahidi wa tatu na wanne waliyoandika Polisi yansikitisha. Siyo melezo ya shahidi kwenda kusomwa kwa jaji Bali yanapaswa kuishia Mahakama za Mwanzo. Lakini kwanini mashahidi wamekuw na kiburi n kwanini DPP na Polisi wameshindwa kufanya kazi yao ya kitaaluma? Ni kwasababu Wana uhakika 100% Jaji awezi kufanya chochote. Ukali n hadhi ya ujaji havionekani mahakamani. Uwezi kutofautisha kazi ya hakimu na Jaji, hakuna sehemu Jaji anasimamia standard za ujaji, hakuna professionalism Mahakama imebaki kucheka hata inapodanganywa wazi.
Nadhani Ni muda Sasa kesi hizi zirejeshwe Mahakama ya chini maana hakuna ladha ya kesi hizi kusikilizwa Mahakama kuu au Mahakama y mafisadi.
Shahidi Hana facts, hakuna muunganiko wa ushahidi, hakuna analosema la ukweli, dakika chache anasema hiki baada ya muda anajisemea mengine n hakuna kukemeana. Hizi siyo Mahakama, tunajidhalilisha Sana. Jaji asipoonyesha ukali wa kiti kwa mashahidi Mahakama zitaendwlea kuchezewa na kuwa sehemu ya majaribio.
Polisi awapo serious, DPP yupo tu mradi analipwa salary na Jaji naye katulia tu kulinda haki ya shahidi. Tunachezea Sana mhimili huu. Ukiona wakili wa utetezi anafika mahali anamwambia Jaji tushauriane tukurahisishie kuandika hukumu basi wakili wa utetezi ameona wazi anadhalilisha taaluma yake Bora wakayazungumze gizani huko labda Mahakama utafumbua macho