Hii ni kauli ya kishabiki, kibaguzi na kitoto kutoka kwa kiongozi wa Bunge

Wabunge wa CDM ndio wanaowalea CCM mle ndani. They have to change.Tumewatuma kuwashikisha adabu watu kama hao na si kunywa bia pamoja alafu baadae mnaoneana haya.tunataka iwe kama mwanzo mlipoingia bungeni hadi wawaombe muwape shikamoo!
 
M/kiti jana kaonyesha uwezo mdogo sana wa kuliendesha bunge na kutia shaka kwa wenyeviti wote ikiwemo maspika juu ya uwezo wao wa uendeshaji wa bunge la vyama vingi na wabunge wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo na kujua sheria kikubwa alichokikosea jana ALIACHA USHABIKI(UKADA) UENDESHE BUNGE BILA YA KUJITAMBUA pole sana kwa CCM na pole sana kwa wapigana maslai bugeni maana kazi kweli bado ni ngumu kwenu
 
Nimeshitushwa sana na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge, Sylivester Mabumba aliyekuwa akiendesha Bunge jana jioni. Baada ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Stella Manyanya kuwatuhumu Chadema kwa kuchochea mgomo na kudai kwamba walihusika na kumteka na kumjeruhi Dk Ulimboka, Mbunge wa Ubungo (Chadema), alikuja juu baada ya kauli hiyo akimtaka Mwenyekiti amtake Manyanya kuthibitisha au kufuta kauli yake.

Katika suala ambalo liko wazi sana kwamba Manyanya hakupaswa kuwashutumu Chadema kwa namna hii, Mabumba alionyesha wazi kuendesha kikao kwa njia ambayo ni ya kishabiki, kibaguzi na kitoto pale alipomjibu Manyika yeye Mnyika ndiye athibitishe kwamba Chadema hakihusiki.

Mie si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, lakini kwa kweli nimekerwa mno na jibu hili la Mabumba. Huu ni ushabiki, ubaguzi na utoto ambao haustahili kabisa katika kiongozi wa Bunge letu. Mabumba anapaswa kukumbushwa kwamba hili Bunge ni la Watanzania. Viongozi wa Bunge wamekuwa wakiwadai wabunge wa upinzani kutoa ushahidi hata katika mambo ambayo eidha si ya msingi au yako wazi kabisa. Huu ni ukandamizaji dhahiri wa wawakilishi wa Watanzania ambao hata sisi tusio wanachama wa vyama vya siasa tunaona unatia kichefuchefu.

Niko tayari kumpa simu yangu Mabumba ili ikiwezekana tukutane ana kwa ana nimweleze dukuduku langu kwa jibu lake hili linaloonyesha upungufu mkubwa katika masuala ya uongozi wa Bunge. Kama kuna mtu mwenye email ya Mabumba aiweke hapa ili tulio na hasira na jambo hili tumwandikie kutoridhishwa kwetu na kile alichokifanya.

Huyu Mambumbu alikuwa anawashwa ndo maana alikuwa insane vile. Mtu aliyeko sawa kichwani na mwilini hawezi kuongoza kikao cha bunge, chombo muhimu kabisa cha nchi kwa staili ile. Tena vijana na watoto wakiangalia live. Mwigulu na Stella nao wapo category hiyohiyo.
 
Si vizuri kumjadili mtu ambaye ana hitaji intensive care!

Hali ya kichwa chake ni mbaya sana.
 
Nimeshitushwa sana na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge, Sylivester Mabumba aliyekuwa akiendesha Bunge jana jioni. Baada ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Stella Manyanya kuwatuhumu Chadema kwa kuchochea mgomo na kudai kwamba walihusika na kumteka na kumjeruhi Dk Ulimboka, Mbunge wa Ubungo (Chadema), alikuja juu baada ya kauli hiyo akimtaka Mwenyekiti amtake Manyanya kuthibitisha au kufuta kauli yake.

Katika suala ambalo liko wazi sana kwamba Manyanya hakupaswa kuwashutumu Chadema kwa namna hii, Mabumba alionyesha wazi kuendesha kikao kwa njia ambayo ni ya kishabiki, kibaguzi na kitoto pale alipomjibu Manyika yeye Mnyika ndiye athibitishe kwamba Chadema hakihusiki.

Mie si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, lakini kwa kweli nimekerwa mno na jibu hili la Mabumba. Huu ni ushabiki, ubaguzi na utoto ambao haustahili kabisa katika kiongozi wa Bunge letu. Mabumba anapaswa kukumbushwa kwamba hili Bunge ni la Watanzania. Viongozi wa Bunge wamekuwa wakiwadai wabunge wa upinzani kutoa ushahidi hata katika mambo ambayo eidha si ya msingi au yako wazi kabisa. Huu ni ukandamizaji dhahiri wa wawakilishi wa Watanzania ambao hata sisi tusio wanachama wa vyama vya siasa tunaona unatia kichefuchefu.

Niko tayari kumpa simu yangu Mabumba ili ikiwezekana tukutane ana kwa ana nimweleze dukuduku langu kwa jibu lake hili linaloonyesha upungufu mkubwa katika masuala ya uongozi wa Bunge. Kama kuna mtu mwenye email ya Mabumba aiweke hapa ili tulio na hasira na jambo hili tumwandikie kutoridhishwa kwetu na kile alichokifanya.

Nitakuwa nafkiri "kimasaburi" iwapo nitarajia kazi iliyotukuka toka kwa uongozi huu wa bunge hili.
Tukumbuke ndugu zangu jinsi demokrasia ilivyobakwa wakati wa uchaguzi wa spika, baada ya kuona kuna uwezekano wa mtu nadhifu, aliekwisha onesha anaifahamu kazi na majukumu ya bunge barabara (yakuihoji serikali) mwenye mawazo na fikra sahihi kuhusu kesho ya nchi hii kuwa atashinda, vigezo vilibadilishwa ghafla kuwa lazma spika awe mwanamke bila kujali uwezo wake ukiulinganisha na waspika aliyepita. Watanzania (wasomi na wasio wasomi) kama kawaida yetu ya kutofikiri na kuhoji mambo kwa mapana na marefu tukakubali kigezo dhaifu cha jinsia bila kujali uwezo. Haya ndo matunda yake, kwakuwa spika kakirimiwa cheo hatutarajii kwenda kinyume na waliomkirimu, na hata waliochini yake hawanauwezo wa kuliongoza bunge hili lenye baadhi ya watu smart wanaotafakari mambo kwakina kabla ya kuzungumza, wanaoonesha upeo mkubwa hata kuliko wale wanao ongoza vikao. Kinga kubwa ya mtu asiye na hoja ni kujaribu kuwakebehi wenzake, kwa nia ya kuwakatisha tamaa.
Tumeona hlo kwa wanaoliongoza bunge letu wanapo wadhihaki, kebehi na kuwapiga vijembe wawakilishi makini.

Kama mwalimu ambaye hajajiandaa kufundisha anavyojilinda na maswali kwa kuwa mkali, kuingia na kiboko darasani na kuwadhihaki wanafunzi wanaouliza maswali kla mara.
Bunge letu limekuwa la ajabu sana, limepoteza credibility, kwasababu ya ushabiki wakisiasa wa waziwazi wa viongozi wa bunge hilo.

Mama yangu Anna nikuonapo kanisani tukisali pamoja huwa na Muomba sana Mungu akusaidie uone kuwa cheo hcho umempora mtu kisiasa, kwa maslahi ya watu au kundi flani, roho ikuume, ubadilike, utende haki kama mtangulizi wako, bunge liwe sehemu ya kumpa mtanzania wakawaida matumaini ya Tanzania mpya na demokrasia ya kweli,uelekeze kina Mabumba kuacha ushabiki wa kisiasa, unaonesha incompetence na utaoliangamiza tafa letu.
 
sifa kubwa ya kua mwenyekiti ni lazma uweze kutetea upuuzi na udhaifu wa magamba
 
Wanaendesha bunge kiccm wanashindwa kuelewa wapo kwa ajili ya wananchi
 
Back
Top Bottom