Hii ni kauli ya kishabiki, kibaguzi na kitoto kutoka kwa kiongozi wa Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni kauli ya kishabiki, kibaguzi na kitoto kutoka kwa kiongozi wa Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Jul 3, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,330
  Likes Received: 3,120
  Trophy Points: 280
  Nimeshitushwa sana na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge, Sylivester Mabumba aliyekuwa akiendesha Bunge jana jioni. Baada ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Stella Manyanya kuwatuhumu Chadema kwa kuchochea mgomo na kudai kwamba walihusika na kumteka na kumjeruhi Dk Ulimboka, Mbunge wa Ubungo (Chadema), alikuja juu baada ya kauli hiyo akimtaka Mwenyekiti amtake Manyanya kuthibitisha au kufuta kauli yake.

  Katika suala ambalo liko wazi sana kwamba Manyanya hakupaswa kuwashutumu Chadema kwa namna hii, Mabumba alionyesha wazi kuendesha kikao kwa njia ambayo ni ya kishabiki, kibaguzi na kitoto pale alipomjibu Manyika yeye Mnyika ndiye athibitishe kwamba Chadema hakihusiki.

  Mie si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, lakini kwa kweli nimekerwa mno na jibu hili la Mabumba. Huu ni ushabiki, ubaguzi na utoto ambao haustahili kabisa katika kiongozi wa Bunge letu. Mabumba anapaswa kukumbushwa kwamba hili Bunge ni la Watanzania. Viongozi wa Bunge wamekuwa wakiwadai wabunge wa upinzani kutoa ushahidi hata katika mambo ambayo eidha si ya msingi au yako wazi kabisa. Huu ni ukandamizaji dhahiri wa wawakilishi wa Watanzania ambao hata sisi tusio wanachama wa vyama vya siasa tunaona unatia kichefuchefu.

  Niko tayari kumpa simu yangu Mabumba ili ikiwezekana tukutane ana kwa ana nimweleze dukuduku langu kwa jibu lake hili linaloonyesha upungufu mkubwa katika masuala ya uongozi wa Bunge. Kama kuna mtu mwenye email ya Mabumba aiweke hapa ili tulio na hasira na jambo hili tumwandikie kutoridhishwa kwetu na kile alichokifanya.

  03/07/2012
  Baada ya kupewa email yake, nimemwandikia email Mbunge Mabumba, iko chini hapa kwenye hii thread.

  Update: 04/07/2012:
  Mnyika ataka ufafanuzi juu ya wabunge kudhalilishwa

  Mbunge wa Ubungo, (Chadema) John Mnyika, ameomba mwongozo wa Spika, akitaka aelezwe hatua gani atahuchukuliwa Mwenyekiti wa Bunge, Sylivester Mabumba, kwa kitendo cha kuwadhalilisha wabunge wawili alipokuwa akiendesha kikao juzi jioni.
  Mnyika aliomba mwongozo huo kwa Mwenyekiti wa Bunge, Jenister Mhagama, mara baada ya kipindi cha maswali na majibu mjini Dodoma jana.

  Akitumia kanuni ya tano (1) kwamba juzi katika mkutano wa Bunge, Mwenyekiti wa Bunge, Mabumba (Mbunge wa Dole-CCM), alitoa maneno ya kuwadhalilisha wabunge wawili.

  Alimtaja Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, ambaye aliambiwa kuwa anadandia hoja na anajitafutia umaarufu.
  Alisema pia Mabumba, alitoa maneno kuwa yeye (Mnyika), ameshindwa kujibu taarifa, jambo ambalo halikuwa ni kweli kwasababu hakupewa nafasi ya kujibu.

  Alisema jambo jingine, Mabumba alimwambia kuwa `anawashwa washwa', na kwamba hayo maneno yameleta hasira sana kutoka kwa wananchi wake wa jimbo la Ubungo kwa kuwa wameona kuwa wamekashfiwa wao.
  Alisema na wananchi wa Kasulu Mjini, nao wanaona kuwa wamekashfiwa wao kwa kitendo cha Mbunge wao kutolewa maneno ya udhalilishaji.

  Alisema kanuni 64 (2) inatoa nafasi kutoa utaratibu kwa mambo yanayomhusu mbunge mwingine. Mnyika alisema pia maneno hayo yanakiuka ibara ya sita ya sheria ya maadili ya umma. Aliomba mwongozo wa Spika, wabunge hao wachukue hatua gani kwa jambo kama hilo.

  Kuhusu suala la Mnyika, Mhagama alisema suala hilo atalitolea maamuzi baadaye ama siku atakayoona inafaa.
  CHANZO: NIPASHE   
 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Nenda kwenye website ya Bunge utaipata email address ya Sylivester Mabumba
   
 3. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hakuna haja ya kuzungumza naye kwa kuwa ni chizi huyu huvi wa wapi huyu? amekashfu CCM, Amekashfu Bunge ?amekashfu Serikali?
   
 4. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  smabumba@parliament.go.tz Email ya MABUMBA anaeendesha Bunge kama kikao cha mashemeji zake.
   
 5. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Kaka mtoto wa mwenzako ndiye mhalifu ila wa kwako ni malaika, siku zao zinahesabika
   
 6. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Namrima email sasa hv
   
 7. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee kawaambia wabunge wa CDM "WANAWASHWA MAKALIO" hivi ana maana gani kutukana mbele ya UMMA wa waTZ ilibaki kidogo tu kuwaita Washenzi nini ?
   
 8. A

  Augustino Ntani Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana nawe moja kwa moja kumlaani Mabumba jinsi alivyoendesha kikao kitoto na kwa ubaguzi wa wazi. Mwenyekiti huyu nidhaifu na hafai. CCM mnazidi kujimaliza 2015 ni hukumu yenu.
   
 9. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  hata ukimwandikia email unapoteza muda kaka, huyu mtu ni mgumu kujisomea, ndio maana hata kanuni za kuthibisha kauli bungeni jana ni mh mnyika ndiye alimkumbusha na kumkosoa jana kuwa ni kifungu cha 64.....mabumba akabaki kushangaa wakati kanuni analala nazo kila siku ila kusoma ni ngumu
   
 10. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,311
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Alilo lifanya mapumba sijawahi kuliona mahalipopote pale kumtaka mtuhumiwa athibitishe kwanza utetezi wake kabla ya anae toa tuhuma kuthibitisha kwanza ni jambo la ajabu.hapa ametoa maamzi ya pumba kama jina lake.
   
 11. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Viongozi DHAIFU wanaongoza SILLY SEASON in a SILLY PARLIAMENT.
   
 12. m

  majebere JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  unajifanya sio mwanachama wa CDM wakati matapishi yako yote yanaonyesha uchadema wako.
   
 13. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sijawahi kufikiria tunaweza kuwa na viongozi wa ajabu kama huyu mzee. Nimeshamuandikia Email kulaani udhalilishaji alioufanya katika Bunge letu tukufu kwa unazai wa Wazi kabisa wa KITIKADI.. nCHI ZA WATU WATU WANGEENDA PALE NA mABANGO KUPINGA UJINGA/UPUMBAVU ULE
   
 14. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,606
  Trophy Points: 280
  Kuna haja kipengele cha elimu, na vidokezo vingine kuzingatiwa katika upatikanaji wa hawa wagombea wa ubunge kwenye kura za maoni. Ikiwezekana kuwe na usahili ili kupima uwezo wa kufikiria na mengineyo.
   
 15. T

  Tata JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  CCM imewahi kuwa na kiongozi mmoja tu na makasuku na waigizaji wengi waliomzunguka ambao walikuwa wakirudia kila alichokuwa akisema na kumuigiza kila alichokuwa akifanya bila hata kuelewa mantiki yake. Bahati mbaya kiongozi huyu alisharudi kwenye haki na sasa hakuna tena kiongozi ila wamebaki makasuku na waigizaji ambao hawana wa kuwaongoza. Matokeo yake kama walivyokuwa wakimuigiza kiongozi wao wameamua kuigiza utandawazi ulioletwa na IMF na World Bank bila hata kujua mantiki yake.
   
 16. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  jamaa jana aliudhi sana. huwa siku akikali kiti nakuwa sina hata hamu ya kuangalia bunge!
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Tanzania haina bunge ....ina kundi la wahuni ,wazinifu na watu wa kijiweni,,,hakuna la maana wanalofanya kule bungeni...
   
 18. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  watanzania wote tuandamane kudai kuwa bunge limepoteza mwelekeo na wanaopoteza mwelekeo wa bunge ni mwigulu, makinda, mabunba nk
   
 19. C

  Cecy Emmanuel Member

  #19
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakifupi bunge la jana chini ya mwenyekiti Mabumba yule jamaa anatakiwa apigwe kofi la kiingereza pengine akili ingerudi maana anaonekana hana akili ya kufikiri hata punje ya jambo dogo kama lile... tunajua fika kuwa serikali ni ya chama tawala ila kwenye uendeshaji wa bunge hutakiwi kubaze kwenye chama chochote, mimi namkubali sana Ndungai maana anakuwa fair sometimes.. Mabumba wapiga kura wake wanatakiwa wajue walimchagua mtu wa design gani maana ni hewa tupu...
   
 20. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,330
  Likes Received: 3,120
  Trophy Points: 280
  Nimemwandikia Mbunge Mabumba email ifuatayo:

  Ndugu Mabumba,

  Nimelazimika kuomba email address yako katika mtandao wa Jamii Forum, kutokana na kushitushwa kwangu kwa kauli zako kwa Wabunge wa vyama vya upinzani pale walipotoa hoja zako au kuomba muongozo katika kikao ha hii karibuni. Kwa kweli nimeshituka na kusikitishwa sana na kauli zako. Uliongea maneno ambayo Watanzania hatutegemei kutoka kwa kiongozi kama wewe.

  Kumbuka kwamba tukiwa Watanzania, walio wanachama wa CCM, wa wanachama wa vyama vya upinzani na wale ambao si wanachama wa chama chochote cha kisiasa, tuna matarajio makubwa sana na Bunge kama mhimili mmoja wapo muhimu wa uongozi wa nchi na serikali. Wabunge pamoja na viongozi wa Bunge, mnaweza kulifanya Bunge letu kuwa chachu mojawapo ya maendeleo ya nchi yetu, au mkaligeuza kuwa kama stage ya ushabiki wa kisiasa. Kwa kiasi kikubwa sana, tumekuwa tukishuhudia jinsi baadhi yenu mnaohusika na Bunge letu, kutia ndani viongozi wa Bunge, wabunge wa CCM na hata wabunge wa upinzania, siku hadi siku mmekuwa mnajiendesha kama watu wasiostahili hata kukanyaga sakafu ya Bunge letu, licha ya kuitwa Wabunge.

  Tungependa kuwakumbusha kwamba hili ni Bunge la Watanzania, na mpo pale Bungeni kwa niaba ya Watanzania , sio familia zenu, wala Raisi wa nchi, wala vyama vyenu. Basi tunawasihi mjiendeshe kama watu wazima wenye akili na busara ya kuwawakilisha Watanzania. Hili ni muhimu hata zaidi pale ambapo dunia nzima inaposhuhudia michezo ya aina ya kipwagu na pwaguzi ambayo imekuwa ikifanyika Bungeni, kwa jina la mijadala ya Bunge.

  Kikubwa kilichonifanya nikuandikie hii email ni mchango wako binafsi kama kiongozi wa Bunge katika kulifedhehesha Bunge la Watanzania. Sikufichi, binafsi nakuona katika tukio la hapa karibuni uliendesha kikao cha Bunge katika njia ya kishabiki, kibaguzi na kitoto, hasa kuhusu mjadala uliokuwa ukiendelea hivi karibuni, juu ya mgomo wa madaktari.

  La kwanza ambalo sikuamini kwamba kiongozi wa Bunge anaestahili heshima kama wewe anaweza kusema ni pale ulipomfokea Mbunge Lissu kwamba "akae chini, asitafute popularity". Hivi kweli, kweli, wewe kama kiongozi wa Bunge unaona ni sahihi kumwambia Mbunge muwakilishi wa wananchi wa Tanzania kwamba anatafuta popularity pale anapotaka kueleza dukuduku lake? Kwa nini isitoshe kwako kumwambia Mbunge Lissu akae chini bila kuongeza suala la kutafuta popularity? Mie binafsi niliona kwamba kwa kauli yako ya kutafuta popularity, mwenye kutafuta popularity hapa alikuwa wewe, labda kutoka kwa Raisi Kikwete au Wabunge wenzako wa CCM. Hainiingii akilini hata kidogo kwamba kiongozi wa Bunge anaweza kumwambia Mbunge asitafute popularity pale Mbunge anapotaka au anapokuwa ameongea kitu. Acha kila mwananchi wa Tanzania binafsi awe mwamuzi wa kama mbunge fulani yuko Bungeni kutafuta popularity au la. Hiyo si sehemu ya kazi yako katka kuendesha vikao vya Bunge.

  La pili ni jinsi ulivyoshughulikia mjadala wakati Mbunge Manyanya akitoa mchango wake. Katika suala ambalo liko wazi sana kwamba Mbunge Manyanya hakupaswa kuwashutumu Chadema kwamba walihusika na kumteka na kumjeruhi Dk Ulimboka, Mbunge wa Ubungo (Manyika, Chadema), alikuja juu baada ya kauli hiyo akikutaka umtake Manyanya kuthibitisha au kufuta kauli yake. Jibu lako kwa Manyika lilikuwa kwamba yeye ndiye athibitishe kwamba Chadema hakikuhusika. Kwa mara nyingine tena Ndugu Mabumba, hebu niambie kama nahitaji degree ya uongozi wa Bunge kutambua kwamba jibu lako kwa Mbunge Manyika lilikuwa na upungufu mkubwa wa busara kwa mtu ambaye ni kiongozi wa Bunge!

  Kutokana na haya nililazimika kupeleka maada katika Jamii Forum kwamba njia yako ya kusimamia mijadala ya Wabunge nimeona ni ya kishabiki, kibaguzi na kitoto. Ningependa kuchukua fursa hii kukusihi sana ubadilike, ukizingatia kwamba hili ni Bunge la Watanzania, na si la CCM wala Chadema wala chama chochote au kiongozi yeyote. Tunawasihi sana mfanye kazi katika Bunge letu kama watu ambao mna dhamana ya uongozi kutoka kwa Watanzania. Na hili lapaswa kuanzia kwa nyie viongozi wa Bunge. Hata kama Wabunge watakuwa na michango ya kishabiki - kitu ambacho tunatarajia kitatokea, nyie viongozi wa Bunge ndio mnaoweza ku-make or break Bunge letu.

  Viongozi wa Bunge na Wabunge kwa ujumla mnapaswa kukumbuka kwamba amani ya Tanzania inategemea pia yale ambayo Watanzania wanaona na kusikia yakiendelea Bungeni. Kwa jinsi uongozi wa Bunge na Bunge kwa jumla linavyoendeshwa kwa sasa, inachangia sana kui-polarize nchi yetu Tanzania na kuwajaza hasira Watanzania katika misingi ya U-CCM, na U-Chadema. Hii haitawasaidia CCM, wala Chadema au chama kingine chochote. Kama ambavyo tunakataa udini katika nchi yetu, ni hivyo hivyo tutakataa U-CCM na U-Chadema kuwa msingi wa mahusiano kati ya Watanzania. Tunaona mifano mizuri ya siasa za upinzani katika nchi kama Marekani, ambako hatuoni U-Democrat na U-Republican kuwa msingi wa mahusiano ya Wamarekani, bali tunaona Wamarekani ambao wana-support policy za Democrats au Republicans, mara nyingine hata bila kujali wao ni wanachama au supporters wa chama gani. Hilo ndilo tunataka kuona katika nchi yetu, kwamba ifikie hatua ambapo hata wanachama wa Chadema wanamchagua kiongozi wa CCM kutokana na sera, na vice versa. Siasa katika nchi si suala kama la Simba au Yanga, hili ni suala la maendeleo ya nchi. Basi msigeuze siasa kuwa suala la kishabiki. Pale Dodoma tuna Bunge kwa ajili ya kujadili maendeleo ya nchi yetu, sio uwanja kama National Stadium kuona nani anaweza kupiga kelele zaidi za kishabiki kati ya CCM na Chadema.

  Wa salamu


   
Loading...