Hii ni kashifa kwa madakitari wa Tanzania: Ninaoza nikijiona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni kashifa kwa madakitari wa Tanzania: Ninaoza nikijiona

Discussion in 'JF Doctor' started by Mallaba, Feb 11, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Penina Tiamaru
  Florence Majani
  [​IMG]“NATAMANI hata kufa, hali niliyonayo inanipa mzigo mzito, wakati mwingine najiuliza kwa nini jambo hili limenikuta mimi? Roho inaniuma sana, nimekata tamaa kama siku moja nitaishi maisha yenye amani kama wengine (analia),” huyo ni Penina Tiamaru (29), mkazi wa Mbezi Salasala, mtoto wa sita wa aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Mikocheni, marehemu Obeid Tiamaru.

  Hawezi kuisahau Januari 2007, ndoto zake za kuwa mwalimu zilipoyeyuka baada ya kupata ajali ya mguu... “Nilikuwa natoka nyumbani kwetu Mikocheni nakwenda kwa jirani yetu, nikawa navuka mfereji na kwa bahati mbaya nikateleza, mguu wa kushoto ukageuka, nikaukanda kwanza kisha nikaenda Hospitali ya Mwananyamala kupata matibabu.”

  Anafafanua kuwa baada ya kufika hospitalini hapo, madakatari walimkagua bila kusema chochote na badala yake wauguzi wakaanza kumchoma sindano za ‘powersafe’ pamoja na dawa ya maumivu ‘diclofenac.’

  [​IMG]“Siku nne zikapita bila kupewa huduma nyingine ya ziada, nilikuwa na maumivu makali sana na mguu ukiwa umevimba kuliko kawaida tena umejaa malengelenge, ilinibidi niwaulize wauguzi kuhusu matibabu yangu wakaniambia kuwa mashine ya X-ray imeharibika, basi nikawa nasubiri ingawa nilikuwa katika mateso makali.”

  Anasema kwamba alikaa hospitalini hapo kwa zaidi ya wiki moja, ndipo siku moja jopo la madaktari lilipopita na kubaini kuwa hali ya mguu wa mwanamke huyo ilikuwa mbaya.

  “Baada ya madaktari kuniona vile, nikapewa rufaa niende Muhimbili, nikabebwa katika gari la wagonjwa nikapelekwa lakini cha ajabu, baada ya kunifikisha tu mapokezi muuguzi na dereva walionisindikiza waliondoka huku wakinitupia faili langu bila kutoa maelekezo yoyote. Madaktari wa Muhimbili walinipokea, nikaingizwa wodini na siku hiyo hiyo nilipelekwa katika chumba cha xray.”

  Anasimulia kwamba majibu ya Xray yalipotoka yalionyesha kuwa mfupa mkubwa unaoshikilia kikanyagio cha mguu umechomoka na siku hiyo hiyo saa tatu usiku iliamriwa aingizwe katika chumba cha upasuaji.
  “Baada ya operesheni nilifungwa vyuma vya kuunganisha mifupa pamoja na jiwe la kilo tano kwa ajili ya kuifanya damu itembee, nilikaa hospitalini hapo kwa zaidi ya miezi minne,” anasema mwanamke huyo mwenye umbile kubwa linalozidi kumpa shida wakati wa kutembea.

  Chanzo cha ulemavu
  Penina anasema hata baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani, alishangaa kuona mguu wake hauendi mbele kama kawaida, akajaribu kuwaambia madaktari lakini walimtia moyo kuwa utanyooka tu na kuwa autembelee vivyo hivyo.

  “Muda mrefu ulipita lakini mguu wangu ukawa haunyooki ndipo nilipokwenda kujaribu matibabu katika hospitali binafsi iliyopo Kibaha ambako niliambiwa kuwa madaktari walionifanyia upasuaji walikosea na kwamba mfupa mkubwa haujaungana na unyayo na ndiyo maana mguu haunyooki kama ulivyokuwa mwanzo.”

  Anasema baada ya kufanyiwa upasuaji, madaktari wa Muhimbili walimwambia alale chali akiwa amenyoosha miguu na kuilaza ili mifupa iliyoachana iungane jambo ambalo akiwa Kibaha alielezwa kuwa hayo hayakuwa masharti kwa tatizo kama lake na ndiyo sababu ya mguu huo kwenda upande.

  Kisa cha kidonda kudumu miaka minne
  Baada ya kuumia, kabla hajaenda hospitali, alipewa huduma ya kwanza ambayo ilikuwa ni kukandwa na maji ya moto na hiyo ndiyo sababu ya mguu wake kuota malengelenge.

  “Mpaka naruhusiwa kurudi nyumbani malengelenge yalikuwa yameisha isipokuwa kifundo cha mguu (ankle) kilibaki kidonda ambacho mwanzoni kilikuwa kidogo lakini kikawa kinaongezeka ndipo nilipoamua kurudi Muhimbili.”
  Alipofika hospital madaktari walimkagua na kumwambia kuwa kidonda chake ni kikubwa hivyo watamfanyia upandikizaji wa ngozi ya mwili wake katika kidonda (skin grafting) ili kikauke haraka.

  “Nilikatwa nyama za paja, tazama (anafunua paja lake na kunionyesha makovu makubwa meusi) humu zilimeguliwa na baada ya hapo wakaziambatanisha katika kidonda, lakini cha ajabu kesho yake asubuhi nikapewa ruhusa nirudi nyumbani kabla hata sijajua hatma ya kidonda hicho.”

  Anaamini kuwa si haki hata kidogo kwa mgonjwa aliyefanyiwa upandikizi wa ngozi katika kidonda kuruhusiwa kurudi nyumbani katika kipindi kifupi na hiyo anadhani kuwa huenda ndiyo sababu ya kuoza akijiona.

  “Wakaniruhusu wakisema nirudi baada ya wiki moja, lakini kidonda kilikuwa kikitoa harufu na ukungu wa kijani ukionekana kwa juu. Hata hivyo, baada ya kipindi hicho nikaenda na nikaambiwa madaktari hawapo, sikuwa na jinsi nikarejea nyumbani.”

  Alikwenda tena hospitali kujaribu bahati yake lakini aliambiwa madaktari wametingwa kwani kuna wagonjwa wengi wanaofanyiwa upasuaji hivyo arudi baada ya wiki. Kuona hivyo, akafanya juhudi hadi akaonana na daktari mmoja na kumuonyesha mguu wake. Akamfanyia usafi.

  “Baada ya hapo nikawa napangiwa tarehe za kurudi nafanyiwa usafi lakini kidonda hakiponi na huu ni mwaka wa nne sasa niko katika hali hii. Kidonda kinazidi kuchimbika, maumivu na harufu kali vinanikosesha raha. Inzi ndiyo rafiki zangu.”

  Kwa mujibu wa maelezo ya Penina, hata kuoza kwa mguu huo kumesababishwa na madaktari kwani akiwa Kibaha aliambiwa kuwa alipewa masharti potofu baada ya kufanyiwa upandikizi huo wa ngozi na ndiyo maana kidonda hicho hakiponi kwani damu ilikuwa haitembei vizuri.

  Hata hivyo, daktari mmoja anayefahamu historia ya ugonjwa wa Penina anasema kidonda chake na pamoja na ulemavu alioupata yawezekana umetokana na yeye mwenyewe kukosea masharti kwani kutokana na tatizo lake inaelekea alikuwa anauweka mguu chini hivyo damu ikawa haitembei.

  Lakini Penina anasema ameambiwa atoe Sh300,000 ili arekebishwe mguu na kutibiwa kidonda upya lakini mpaka sasa ndugu zake wamemsusa hawampi msaada wowote hivyo amekata tamaa na anachosubiri ni kudra Mungu.
  0657 118585
   
 2. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  ni kwanini na nikwa udaktari upi wa kumfanyia mtu skin grafting na kuruhusiwa kesho yake?
  hivi wadaktri hao waliohusika walikuwa wanafanya kazi zao? au walikuwa wanasukuma punda bora liende?
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mallaba Mpe pole zangu jingi Mgonjwa(Penina) mpe Ushauri wangu huu inshallah Mwenyeezi mungu atamjaalia kupona, Kutibu Kidonda kisichopona Atatumia Gundi ya asali kwa hayo Maradhi yake Atajifunga Bendeji kwa gundi ya

  Asali pamoja na Kukisafisha Kidonda kilasiku na kubadilisha Bendeji pamoja na kunywa Asali Safi Mbichi ya Nyuki kijiko kimoja Asubuhi na jioni kila siku kabla ya kula chakula.

  Matibabu ya Kidonda kilichooza

  Atachukuwa Asali ya nyuki Safi mbchi isiyopikwa Kikombe kimoja na Mafuta ya ini la Samaki Kikombe kimoja,yote hayo atayachanganya vizuri na atajipaka baada ya kusafisha kidonda kwa Asali iliyochanganywa na Maji moto,halafu atajifunga kitamba,tiba hii ataendelea nayo kila siku pamoja na kunywa asali kwa wingi.

  Matibabu ya kidonda

  Atachukuwa Asali nusu kikombe na kikombe cha maziwa ya Ng'ombe na atachanganya na unga wa wa Ganda la ndizi lililokaushwa kiasi cha kijiko Atumie kila

  siku kabla ya kula kitu Asaubuhi na jioni kwa muda wa Mwezi mmoja. atapata afya njema wala hataweza kupasuliwa tena.
   
 4. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  seriosly???:coffee::sick:
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  ''Seriously'' What are you mean? Mimi naitwa nani jina langu ? MziziMkavu hauchimbwi Dawa nakupa Dawa unauliza Swali? Seriously? Naongeza Dawa ingine hii kama Kidonda chake hakiponi kila Siku asubuhi anapo amka ajaribu kukinga Mkojo wake mwenyewe kisha ajipakae kwenye hicho kidonda kisichopona kwa muda wa miezi kama mitatu atapona kitakauka hicho kidonda inshallah.
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Nimekuelewa mzizimkavu,
  lakini umeona hali halisi ya hicho kidonda?
  Inaonekana kuna tatizo la mishipa ya damu
  pia kuna uwezekano wa kuwa na Gangrene kitu ambacho ni hatari sana
  hivyo huyo kwa matibabu ya haraka either angehitaji Upasuaji ikiwezekana afanyiwe hata Amputation ili kuzuia further complications.
  sijui unaonaje hilo?
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Sawa hiyo dawa inaweza kumsaidia si unasikia amekwenda hospitali lakini mpaka sasa huko hospitali wameshindwa kumtibia ndio maana nimetowa hizo dawa sasa kama wewe unakiona hicho Kidonda kama ni ( Gangrene) anaweza kutumia hii dawa yangu hapa lakini atakuwa

  anawashwa sana aweze tu kuvumilia Afanye hivi Atakiponda Kitunguu Saumu kikubwa kimoja mpaka kiwe kama Marhamu halafu atajifunga nacho

  bendeji,japokuwa kitawasha sana lakini Kitazuia Ugonjwa wa ( Gangrene) ambao unaweza ukapeleka kukatwa Kiungo chake. Mwenyeezi Mungu amkinge na hayo matatizo ya kukatwa mguu inshallah amina.
   
 8. BWANYEENYE

  BWANYEENYE Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Jun 2, 2010
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu amjaalie uzima haraka inshaallah aamin!!!!!vr sad hao ndio madaktari wetu...Mungu tustiri
   
 9. Papa Diana

  Papa Diana JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 304
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
 10. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  i feel sorry for her!!
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Thanks mkuu MZIZIMKAVU.....tupo pamoja broda nimelizika kwa majibu yako.....
   
 12. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mzizimkavu umewahi kunipa ushauri juu ya kutoa harufu kinywani bado natumia lakini maendeleo yananiridhisha
   
Loading...