Hii ni high frequency hearing loss, au ni nini?

HumbleBoy98

JF-Expert Member
Aug 30, 2020
386
392
Habari zenu wakuu, natumai mko Salama na mnaendelea vyema na majukumu ya ujenzi wa taifa.

Niende Moja kwa Moja kwenye mada.

Mimi HumbleBoy98 nimekuwa na tatizo la usikivu kwa takribani miaka 9 sasa, sikuzaliwa hivi nilikuwa mzima kabisa Ila ilipofika mwaka 2011 nilianza kuhisi Hali ya tofauti katika usikivu wangu.

Ni kwamba mtu anapoongea namsikia sauti yake vizuri tu, ila tatizo ni kwamba Yale matamshi siyaelewi yanapotamkwa Yani nakuwa sisiikii baadhi ya herufi zinapotamkwa hivyo mtu anapoongea naona Kama anamung'unya tu maneno hivi na anachokiongea nakuwa sikielewi.

Tatizo hili halikuanza na dalili zozote sikuwahi hisi maumivu masikioni, Wala kutoa usaha, Wala Nini na nilishaenda hospitali Fulani pale maeneo ya magomeni mikumi inaitwa "EKENYWA", Pale wakaniingizia kifaa fulani kilichokuwa na kamera sikioni ila hawakuona uvimbe Wala tatizo lolote lile masikioni mwangu!

Hali hii imenifanya nishindwe kuelewa hili tatizo limetokana na nini sababu halikuanza na dalili zozote Yani Ni ghafla tu nimejikuta mtu anapoongea namsikia lakini simuelewi.

Sasa nimekuwa nikijaribu kuperuzi mtandaoni ili kuona Kama nitakutana na maelezo yatakayoendana na hili tatizo langu, na katika kuperuzi kwangu ndipo nilipokutana na kitu kinaitwa "High frequency hearing loss"

Kwa mujibu wa maelezo niliyosoma katika mtandao Ni kwamba hii "High frequency hearing loss" Ni Hali ambayo mtu anashindwa kusikia sauti au matamshi ambayo utamkwaji wake unatoa frequency za juu sana mfano herufi "s", "f", na "ch" anakuwa hawezi kuzisikia zinapotamkwa hivyo Basi kuhisi Kama mtu anamung'unya maneno na kutoelewa kinachoongelewa.

Niliposoma hayo nikahisi labda na Mimi Nina hii "High frequency hearing loss" maana yaliyoelezwa Hapo ndiyo hasa yanayonikabili, Ila nilikuja kupata sintofahamu baada ya kusoma vyanzo ama visababishi vya tatizo hili na kugundua hakuna hate kimoja ambacho kinahusiana nami.

Kwa mujibu wa maelezo hayo niliyosoma mtandaoni wanasema kwamba high frequency hearing loss inasababishwa na aidha kukaa sehemu yenye kelele nyingi kupita kiasi kwa muda mrefu au umri kuwa mkubwa (uzee).

Sasa kunachnichanganya ni kwamba haya yote mawili kwangu hayahusiki katika kumbu kumbu zangu sikumbuki kabisa Kama niliwahi kukaa sehemu yenye kelele nyingi kupita kiasi kwa muda mrefu kiasi Cha kuweza kusababisha madhara masikioni mwangu. Na hili la pili kuhusu umri kuwa mkubwa ndiyo kabisa halihusiani nami, umri wangu Ni miaka 22 tu!

Sasa wakuu ambao Ni wataalamu wa haya mambo naomba mnisaidie hili linaweza kuwa tatizo gani?? Inawezeoana ikawa ni hiyo high frequency hearing loss?? Mbona hivyo vyanzo tajwa havishabihiani kabisa na Mimi?

Nahitaji msaada kwakweli sababu Hali hii inanipa tabu Sana nashindwa kuwasiliana na niwapendao kwa raha, hapa nilipo Mimi Ni mwanachuo ila kwa 90% facilitator wangu ni Mimi mwenyewe sababu mwalimu anapoingia darasani kufundisha nakuwa sielewi chochote Ni mpaka mida ya prepo nianze kukaa na kujifundisha mwenyewe mpaka nielewe, ninaposikiliza muziki nasikia mdundo wa beat tu maneno yanayoimbwa siyaelewi, ninapotazama movie ni mpaka iwe na 'subtitle'ndo nitaielewa hata ikiwa ya kiswahili, tunapokuwa tumekaa watu wengi naonaga tu wenzangu wanapiga story wanacheka ila Mimi hata sielewi wanaongea Nini nasikia makelele tu! Hali hii inanifanya muda mwingi niwe napendelea kukaa peke yangu na kujitenga na watu.

Nilishauriwa kutumia zile 'hearing aid' ila na zenyewe nilitumia kwa muda mchache tu nikaamua kuachana nazo maana zinaongeza tu sauti ila Bado matamshi siyaelewi nikaona zitaniharibu zaidi saahizi sitaki hata kusikia habari za hearing aid!

Wakuu ambao mnaweza kuwa na uelewa na tatizo hili na wataalamu pia naombeni ushauri wenu tafadhali

Nawasilisha
 
Samahanini wakuu, Hapo kwenye heading nilimaanisha "Hii Ni high frequency...." Ni mambo ya 'autocorrect' nimejaribu ku edit hiyo heading nimeshindwa naomba mods wanisaidie kwa hilo tafadhali, Asanteni.
 
pole sana bro.

nadhani uende kwa ENT specialist pale muhimbili kuna hearing test wanafanya then unapewa hearing aid customized to your frequency problem.

kama fedha sio tatizo, nenda Upanga mtaa wa Mindu kuna specialist wa maskio ana vifaa vya kisasa zaidi
 
pole sana bro.
nadhani uende kwa ENT specialist pale muhimbili
kuna hearing test wanafanya
then unapewa hearing aid customized to your frequency problem

kama fedha sio tatizo, nenda Upanga mtaa wa Mindu kuna specialist wa maskio ana vifaa vya kisasa zaidi
Asante Sana mkuu kwa ushauri wako mambo yakikaa sawa nitaufanyia kazi, shukrani
 
Ila hapa mindu niliendaga mwaka juzi wakanipima then wakanipa hearing aids ambazo kwakweli hazikunisaidia. Kibaya zaidi zilikuwa Bei aghali Sana saivi zipo tu ndani nimeziweka ngoja no jaribu Hapo Muhimbiou labda
 
Kisema kweli mzee omba Mungu tu hilo tatizo halitibiki ni neva kwny ubongo zimekufa mie pia na shida hyo nishaenda huko Ekenywa, Upanga mtaa wa Mindu jwa wahindi wa bei mbaya bila mafanikio..

Hearing aid haziwez kukusaidia sababu sikio lipo vizuri ni mishipa kichwani imezingua ni kama vile mtu anapikua kipofu there is no way jikubali na hali yako na pia kuwa free usifiche ukifika sehemu ni mgeni sema kuwa husikii waangalie watakusaidieje ikitoke watu wame ku diss au kukucheka hujasikia take it easy mzee...

So jikubali Hospital kwa bongo haoa utapoteza pesa labda nje ya nchi
 
Tupo wengi mkuu. Mi nilishafanyiwa usafishaji zaidi ya mara tatu ila ikabuma. Nikafanya hearing test ndio nikagundua nina excess hearing loss ambayo imesababishwa na kuathirika kwa nerves. Nishatumia dawa kama gentamycene ya drop na vidonge flani hivi walisema ni nerves ila ikabuma bado.

Ni tatizo baya sana ila inabidi tukubali tu. Mimi siongei na simu yaani situmiagi dakika kabisa, mawasiliano yangu ni kwa sms tu.
Siangalii movie bila subtitles, never, Nahisi kukosa body balance hivyo huwa inaniwia vigumu sana michezoni na nishaacha kucheza step kwenye kwaya maana unakuwa kichekesho,

In short, ilivyoeleza ndivyo nilivyo. Cha msingi ni kama alivyosema mdau hapo juu ni kujikubali na kuwa muwazi basi.
 
Tupo wengi mkuu. Mi nilishafanyiwa usafishaji zaidi ya mara tatu ila ikabuma. Nikafanya hearing test ndio nikagundua nina excess hearing loss ambayo imesababishwa na kuathirika kwa nerves. Nishatumia dawa kama gentamycene ya drop na vidonge flani hivi walisema ni nerves ila ikabuma bado.

Ni tatizo baya sana ila inabidi tukubali tu. Mimi siongei na simu yaani situmiagi dakika kabisa, mawasiliano yangu ni kwa sms tu.
Siangalii movie bila subtitles, never, Nahisi kukosa body balance hivyo huwa inaniwia vigumu sana michezoni na nishaacha kucheza step kwenye kwaya maana unakuwa kichekesho,

In short, ilivyoeleza ndivyo nilivyo. Cha msingi ni kama alivyosema mdau hapo juu ni kujikubali na kuwa muwazi basi.
Inauma sana kaka sana sana kipengele cha simu kinakosesha mengi mana kuna watu meseji huwa hawajibu
 
Back
Top Bottom