Hii Ni Heshima kwa wakwe Au Nini???

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,700
Kuna jamaa mmoja jana amefanya kituko..........alikuwa kakaa kijiweni na rafiki zake, ghafla kwa mbali akamuona mama wa mkewe akija na njia ile kilipo kijiwe chao. Jamaa akakimbia na kujificha hadi yule mama apite, lakini na yule mkwe wake kumbe nae alimuona jamaa naye akabadili njia. Jamaa aliporejea pale wenzake wakaanza kumtania kwa kuwa muoga mbele ya mkwe wake lakini yeye akajitetea kuwa ile ni heshima..
Hivi hii ni nini maana sehemu nyingine watu wanakimbia kabisa ili kukwepa tu wasikutane na wakwe zao wawapo barabarani......
 
Hiyo ni nidhamu ya woga bana
May be jamaa ana madhambi yake ndo maana kakimbia au wanakutana na mkwe wake maeneo ambayo siyo kabisa
Ila kumuogopa kiaina hivyo ni nidhamu ya woga kabisa
 
Inategemea alivaa vipi na alikuwa ktk hali gani pengine alikuwa anakwepa aibu
 
Ndio shida ukioa kwa wenye uwezo na wewe uwezo wako mdogo...kujiamini kwapotea kabisa.
 
Huo ni umasikini wa akili tu. Kwa nini umwogope Mama Mkwe? anapaswa kuheshimiwa sio kuogopwa.
Jamaa kuna mambo hayaendi sawa kwenye familia yake ...
 
Kuna jamaa mmoja jana amefanya kituko..........alikuwa kakaa kijiweni na rafiki zake, ghafla kwa mbali akamuona mama wa mkewe akija na njia ile kilipo kijiwe chao. Jamaa akakimbia na kujificha hadi yule mama apite, lakini na yule mkwe wake kumbe nae alimuona jamaa naye akabadili njia. Jamaa aliporejea pale wenzake wakaanza kumtania kwa kuwa muoga mbele ya mkwe wake lakini yeye akajitetea kuwa ile ni heshima..Hivi hii ni nini maana sehemu nyingine watu wanakimbia kabisa ili kukwepa tu wasikutane na wakwe zao wawapo barabarani......
amekimbia deni! alikua anadaiwa na mama mkwe wake mahari ya binti hakua amemaliza kuilipa na aliahidi siku iyo angemaliza !
 
Labda alikuwa kwenye situation ambayo kwa namna flani aliamini ingemtia aibu, so ili kuiepuka akaamua kukinyepesha kwa muda!!
 
<br />
<br
Nakuunga mkono mamamkwe, hakuwa na njururu, mapesa mfukoni, hata ningekuwa mimi ningemkwepa kiaina.

upo kijiweni na washkaji,halafu mm mkwe anatokea unakimbia eti hauna kitu mfukoni_mama mkwe kama ana shida ndio akufuate kijiweni,...hamna kitu kama hicho_huyo jamaa ni muoga na hana lolote la kusingizia
 
Nimeshasikia baadhi ya makabila wana huo utamaduni sijuhi mila ya kukimbia wakwe. Na ni makabila mengi tu yana huo utamaduni. Ila kwa hapa mjini; wakwe wengi wanakaa kochi moja kwani hatujali mila wala tamaduni.

Hiyo nasikia iliwekwa ili kuepusha uzinifu kati ya mtu na mkwe wake. Na makabila yale ambayo mila hii walikuwa hawana kabisa kuna kesi nyingi za wababa kuzaa na wakwe zao.
 
Huo ni umasikini wa akili tu. Kwa nini umwogope Mama Mkwe? anapaswa kuheshimiwa sio kuogopwa.
Jamaa kuna mambo hayaendi sawa kwenye familia yake ...

ni kweli kabisa mkuu,...mama wa mke wako ni kama mama yako_sidhani kama ni busara kumuogopa hadi kukimbia vijiweni,...kwani hata mambo ya familia yakiwa sio sawa ndio mama mkwe aje kijiweni kuyasolve,.......jamaaa ni muoga bana
 
kama nyumba kubwa alivyotujuza ni mila tu kwani hamjui kuna kabila baba mkwe akiwa sebuleni mkeo haingii hata kumsalimia watasalimiana nje!
 
Nimewahi sikia sijui ni kweli kuwa kuna makabila....mume hakataliwi kitu
kama mke mgonjwa unapewa mdogo mtu,ikishindikana mama mkwe anajitolea
nalitafuta hilo kabila lol
 
Nimewahi sikia sijui ni kweli kuwa kuna makabila....mume hakataliwi kitu
kama mke mgonjwa unapewa mdogo mtu,ikishindikana mama mkwe anajitolea
nalitafuta hilo kabila lol
makubwa hebu tuambie kabila gani hilo makaka zetu wakaoe!
 
Nimewahi sikia sijui ni kweli kuwa kuna makabila....mume hakataliwi kitu<br />
kama mke mgonjwa unapewa mdogo mtu,ikishindikana mama mkwe anajitolea<br />
nalitafuta hilo kabila lol
Kabila gani hilo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom