Hii ni Hatari: Wabunge wa CCM watishiwa maisha

Ndo maana nasema ccm ni chama cha kimafia, hakipo kwa ajili ya kutetea wananchi bali ni genge la wahuni la kuhujumu uchumi wa watanzania. Ndo maana viongozi wake wanawatisha wabunge wanaowatetea wananchi. Mungu awalaani viongozi wote wa ccm!
 
Anayechukia kukosolewa ni mwoga wa ukweli, waache wabunge waikosoe na waielekeze serikali ikibidi watumie mamlaka yao ya kikatiba kuiwajibisha, wabunge pia wajifunze kwa tukio hili kwani hata wao waliitisha serikali ilipowanyima ongezeko la posho, pande zote zicheze mchezo wa haki.
 
Majimbo mengi yatakuwa wazi na Chadema wataongeza idadi Bungeni.

Vita ya panzi furaha kwa kunguru.
 
CCM a fool political party mkome kabisa msije mkamgusa filikunjombe, patachimbika, mlimuua ndugu yetu mpendwa kolimba basi pale tulipokuwa wajinga, sasa imetosha,wachawi kabisa nyie.
 
BAADHI ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi, walioshiriki kusaini hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa nia ya kushinikiza kujiuzulu kwa mawaziri wanaotuhumiwa kufuja mabilioni ya fedha, wametishiwa maisha.

Habari za kuaminika zilizothibitishwa na mmoja wa wabunge hao, zimesema kuwa wabunge wawili kati ya wanne wa chama hicho wamelazimika kuukimbia mji wa Dodoma na kujificha kwa muda kusikojulikana.

Wabunge hao (majina yao tunayo) waliondoka mjini Dodoma mara baada ya kupewa taarifa na watu wao wa karibu kuwa walikuwa wakisakwa kwa vile baadhi ya wakubwa ndani ya CCM walikuwa wamechukizwa na kitendo hicho.

Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa wabunge waliokimbia na kujificha, amedai kuwa alilazimika kufanya hivyo baada ya kushauriwa sana na rafiki zake, ingawa awali aligoma kuondoka akisema angekuwa tayari kukabiliana na lolote hata kufa kwa vile anaamini hajafanya kosa lolote la kuhatarisha amani ya nchi.

"Ni kweli niko nje ya Dodoma, nimefanya hivi baada ya kuwepo kwa hisia hizo, maana naziita hivyo kwa sababu binafsi siogopi kutishwa," alisema mbunge huyo.
Kwa upande wake, Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) ambaye ni mmoja wa wabunge wa chama hicho waliotia saini hoja hiyo, alikiri kupigiwa simu za shutuma na lawama kwa madai ya kukisaliti chama na kuunga mkono hoja ya wapinzani ya kutaka kuwawajibisha mawaziri wanaoitumikia serikali ya chama hicho.

Filikunjombe alisema ingawa hajapata vitisho rasmi, lakini alijua hatua hiyo ingemgharimu. Alisema kuwa hajutii hatua hiyo kwa sababu ndiyo mahali pekee pa kusemea na kwamba kama asipoyasema yeye machungu ya Watanzania, hajui nani atayasema.

Mbunge huyo machachali na asiye na woga aliongeza kuwa ni wajibu wake kukisadia chama chake kwa moyo mnyoofu na kuwasilisha kilio cha Watanzania na cha wananchi wa Ludewa.

Alizidi kumshambulia Waziri wa Kilimo na Chakula, Jumanne Maghembe, kwa kuzembea na kupeleka mbolea ya kupandia jimboni kwake Ludewa mwezi Machi badala ya mwezi Oktoba, tena ikiwa feki.

"Katika hali ya hovyo kiasi hiki, walitaka nicheke na kutetea upuuzi eti kwa sababu nalinda chama? Nimechaguliwa na watu kuwalinda na kuwaletea maendeleo sio umaskini. Kibaya wamewakopa hata mawakala. Badala ya kunisaidia na kuwawajibisha waliofanya uzembe huu eti nalaumiwa mimi," alisema.

Lugola apigiwa simu ya vitisho

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, alipigiwa simu juzi saa saba za usiku na kiongozi mmoja wa juu wa CCM akimtaka ajiandae kwa mapambano kwa kile kilichoelezwa kuwa amekisaliti chama.

Akithibitisha tukio hilo, Lugola alisema kuwa kiongozi huyo mzito (jina tunalo) ambaye ni bingwa wa kufoka na kutukana vyombo vya habari vinavyomkosoa, alimwita mbunge huyo mnafiki, mzandiki na kwamba kwa hatua yake ya kusaini hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu atambue kuwa ametangaza vita.

"Ni kweli nilipigiwa simu na..(anamtaja) na kuanza kunifokea na kunitukana. Nilishindwa kuamini kama kiongozi mzito kama yeye anaweza kuniambia maneno hayo. Nami nilimwambia kwa kuwa sina kosa na nimetumia haki yangu, afanye lolote analoweza."

Mbunge huyo alisema pamoja na kuambiwa kuwa leo kigogo huyo wa CCM atafika Dodoma kumshughulikia na wale wote tuliotia saini, haogopi lolote na yuko tayari kukabiliana na magumu kwa ajili ya maslahi ya Watanzania.

"Hata wakiniua, sitaogopa naamini katika ukweli na ni kilio cha wengi. Lakini wengi wananiunga mkono, na wamenipigia simu na wanakubali kuwa wako nyuma yangu.

Alisema maisha ya Watanzania ni mabaya, shuleni hakuna walimu wala madawati, hospitali ziko taabani kwa kukosa dawa huku madaktari wakililia maslahi, na kila wakati serikali imekuwa ikidai haina fedha kumbe, zipo na zinaliwa na wajanja.

"Hakuna cha kunitisha katika hali kama hii. Wanaonitisha ndiyo wasioitakia mema CCM na Watanzania na hao lazima tuwashughulikie mchana kweupe. Na katika hili, lazima wote bila kujali wao ni nani lazima wajiuzulu bila kusubiri eti wajipime na kutafakari," alisema Lugola.

SOURCE:TANZANIA DAIMA

Mwambie huyo kigogo aliyekupigia simu kuwa TANZANIA KWANZA CCM baadae. Muulize je suala la Katiba lilikuwepo kwenye ilani CCM? Jk amelichukua kwa sababu ni la kitaifa. Au wanaangalia Vidagaa ndivyo vya kutishwa. Wanaweza kuua watu na sio HAKI (wimbi la mageuzi linalodai haki na uwajibikaji). History ime-prove hivyo. Wapi Dr. Martin Luther King Jr?
 
Waandishi wengine.. Sasa wewe Mtu keshamtaja aliyempigia kunachokufanya wewe umfiche ni nini Kama sio unafiki... Kwenda zako kulee.. !! Wewe Ungemtaja pasipo kificho kwani source ni wewe ?!?! Mwandishi ni mwoga tu.. Hawa ndo wale wale!!
 
Hii inadhihirisha kwamba; kama kweli unataka kuongoza watu kwa haki na uhuru basi huna budi kufanya hivyo kupitia vyama vya upinzani.
 
Huyu anayewatisha siyo Mukama kweli?

.
Aah bana eeh. Mukama yule mukamuaji wa pesa ya machinjio ya kisasa DSM? Ama kweli nchi hii hujenwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno.
.
 
Mimi naomba tuchague majambazi kuliko hawa wanafiki wanaojificha nyuma ya uungwana. Mchi hii imegeuka ya umafia na ufreemason
 
Back
Top Bottom