CCM:Watumia udini kupitisha bajeti
Mgawanyiko umeibuka miongoni mwa wabunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ukihusishwa na masuala ya udini katika kupitisha bajeti za wizara zilizowasilishwa bungeni.
Mbunge wa Mchinga, Saidi Mtanda, anatajwa kuwa nyuma ya mkakati unaojikita katika misingi ya kidini, hususani alipochangia hoja katika hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa. Moja ya hoja iliyojengwa na Mtanda katika kuichangia bajeti hiyo, ni kuhoji sababu za kutofautiana kwa alama za ufaulu wa kimadaraja, kati ya wanafunzi wanaosoma elimu ya dini ya kiislamu na ile ya kikristu.
Kama vile haitoshi, Mtanda anaelezwa kukitumia kituo kimoja cha luninga kupitia moja ya vipindi vyake vya asubuhi, kujenga hoja zinazoashiria kuwapo ‘ubaguzi' wa kidini katika wizara hiyo.
JE HAPO VIPI.....----???
Source ni NIPASHE
Home