Hii Ni HATARI saaanaa, Watanzania kuweni macho. Sasa uoga basi, tunahitaji maamuzi magumu


M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,135
Likes
1,578
Points
280
Age
51
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,135 1,578 280
CCM:Watumia udini kupitisha bajeti


Mgawanyiko umeibuka miongoni mwa wabunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ukihusishwa na masuala ya udini katika kupitisha bajeti za wizara zilizowasilishwa bungeni.

Mbunge wa Mchinga, Saidi Mtanda, anatajwa kuwa nyuma ya mkakati unaojikita katika misingi ya kidini, hususani alipochangia hoja katika hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa. Moja ya hoja iliyojengwa na Mtanda katika kuichangia bajeti hiyo, ni kuhoji sababu za kutofautiana kwa alama za ufaulu wa kimadaraja, kati ya wanafunzi wanaosoma elimu ya dini ya kiislamu na ile ya kikristu.

Kama vile haitoshi, Mtanda anaelezwa kukitumia kituo kimoja cha luninga kupitia moja ya vipindi vyake vya asubuhi, kujenga hoja zinazoashiria kuwapo ‘ubaguzi' wa kidini katika wizara hiyo.

JE HAPO VIPI.....----???


Source ni NIPASHE

Home
 
B

blueray

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Messages
2,219
Likes
6
Points
0
B

blueray

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2012
2,219 6 0
Huu ni uchochezi, ila kwa sababu ni mwana CCM basi poa tu
 
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,135
Likes
1,578
Points
280
Age
51
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,135 1,578 280
EEE ndio

Ukweli wa kuikosoa serikali inakuwa uchochezi kama ikisemwa na upinzani pekee, ila CCCCCM wakisema inakuwa sawa.
 
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
3,135
Likes
1,578
Points
280
Age
51
M

MPadmire

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
3,135 1,578 280
Jamani someni hii habari katika gazeti la NIPASHE
 
B

bato

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2012
Messages
2,891
Likes
1,347
Points
280
B

bato

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2012
2,891 1,347 280
Hii dhambi ya ubaguzi iloanzishwa na CCM imeanza kuirudi.2010 walisema CDM chama cha Wakristo/wakatoliki,mara chama cha kanda ya kaskazini.Sasa wameanza kubaguana wenyewe.Wanachangia wizara kutegemeana na imani ya waziri.Kama 2X7=15 iko kwenye vitabu vilivyopitishwa na wizara,mbunge unatetea nini?Labda mbunge naye ni mbulula!
 
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Messages
3,530
Likes
16,528
Points
280
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2012
3,530 16,528 280
Mgawanyiko umeibuka miongoni mwa wabunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ukihusishwa na masuala ya udini katika kupitisha bajeti za wizara zilizowasilishwa bungeni.
Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kamati ya wabunge hao, vimeeleza kuwa, licha ya chama hicho kuwa katika makundi yanayopingika kwa misimamo, wameibuka wabunge wanaotumia mianya ya kidini kupenyeza ajenda zao.
Hata hivyo, hali inaelezwa kuwa mbaya na inayohatarisha uhai wake, na kwamba jitihada za makusudi zinapaswa kufanyika kuwadhibiti ‘waasisi na watetezi ’ wa mgawanyo huo.
Mbunge wa Mchinga, Saidi Mtanda, anatajwa kuwa nyuma ya mkakati unaojikita katika misingi ya kidini, hususani alipochangia hoja katika hotuba ya bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.
Moja ya hoja iliyojengwa na Mtanda katika kuichangia bajeti hiyo, ni kuhoji sababu za kutofautiana kwa alama za ufaulu wa kimadaraja, kati ya wanafunzi wanaosoma elimu ya dini ya kiislamu na ile ya kikristu.
Kama vile haitoshi, Mtanda anaelezwa kukitumia kituo kimoja cha luninga kupitia moja ya vipindi vyake vya asubuhi, kujenga hoja zinazoashiria kuwapo ‘ubaguzi’ wa kidini katika wizara hiyo.
Wakati bajeti ya wizara hiyo ikiendelea kujadiliwa bungeni, vyanzo vyetu vinaeleza kuwa, wakati kasi ya hoja zilizojikita katika udini ‘zikiwatafuna’ wabunge wa CCM, Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa kamati ya wabunge wa chama hicho, hakuwepo mjini Dodoma.
Hivyo, nafasi yake ilichukuliwa na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, aliyeongoza kikao kimoja kilichoitishwa ghafla kulijadili suala hilo.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho, zilieleza kuwa Mtandao na wabunge wengine, waliungana kutaka suala ya ‘ubaguzi dhidi ya waislamu’ lishughulikiwe, hususani katika kuijadili bajeti ya Dk Kawambwa.
“Tunapokwenda hapaonyeshi dalili nzuri kwa chama chetu,” alisema mbunge mmoja kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, akitaka jina lake lisitajwe gazetini.
Mbunge mwingine kupitia Viti Maalum, alisema mgawanyiko unaoachwa kukua miongoni mwa wabunge wa CCM, ukielekezwa katika misingi ya udini, utakiathiri chama hicho na kuigawa jamii ya Watanzania.
“Inakuwaje Mbunge wa chama tawala, hata kama ni mawazo yake binafsi, anajielekeza katika kuchochea tofauti za kidini, anajenga hoja kumtetea Waziri kwa misingi ya dini, tunakwenda wapi,” alihoji
Hata hivyo, inaelezwa kwamba kasi ya hoja zinazojikita katika udini, ‘ilizimwa’ na Sitta ambaye hakuongoza kutoa mapendekezo ama mwongozo wa kuchangia bajeti ya Dk Kawambwa, badala yake alisema kila mmoja awasilishe mawazo huru, ingawa yenye kuisaidia ipite.
“Kama Sitta angeruhusu mjadala ule uendelee, ni wazi kwamba mambo yangekuwa mabaya zaidi…haistahili kuendekeza hoja hizi za kidini,” kilieleza chanzo chetu.
Hata hivyo, akizungumza na mwandishi wa habari baada ya kuchangia hotuba ya Dk Kawambwa, Mtanda, alisema ni dhana potofu ‘kumhukumu’ kwamba anahusika na hoja za kidini.
“Mimi ninazungumza hoja kwa vielelezo, sasa watu wasikimbilie kunihukumu kwa udini bali kuzijibu hoja kwa ufasaha,” alisema.
Mtanda alitoa pia kauli kama hiyo kabla ya kuchangia hotuba ya bajeti ya Dk Kawambwa, akijiweka kando na udini katika hoja zake.
Sitta anayedaiwa kukabiliana na wakati mgumu wakati mjadala uliojikita kwa misingi ya udini alipotakiwa kulielezea suala hilo, hakuwa tayari.
 
M

majebere

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
4,645
Likes
691
Points
280
M

majebere

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
4,645 691 280
Kichwa cha habari ni kama gazeti la uwazi,hisia kibao lakini ukiingia ndani unakuta habari uchwara
 

Forum statistics

Threads 1,274,860
Members 490,833
Posts 30,526,158