Hii ni EPA nyingine: CDM wataka majina ya Makampuni yaliyopewa mabilioni kufufua uchumi

dazu

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
365
76
Na Gladness Mboma, Dodoma

SPIKA wa Bunge, Bi. Anne Makinda amemtaka Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo kuyataja bungeni kampuni 97 zilizonufaika na mpango wa kunusuru uchumi wa Tanzania kutokana na msukosuko wa fedha duniani.

Spika Makinda amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Bw. Pereila Ame Silima kushindwa kujibu maswali ya Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe na mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Leticia Nyerere waliotaka kutajiwa kampuni hizo.

Katika swali la msingi, Bi. Nyerere alitaka kujua ni kampuni ngapi, kwa majina na kiasi gani cha fedha zilizotumika kwa ajili ya kunusuru uchumi wa Tanzania katika kipindi cha mtikisiko wa uchumi wa dunia na fedha hizo zilitoka wapi na kiasi gani kwa kila chanzo.

Pia mbunge huyo alitaka kujua kama kampuni hizo zilipewa mkopo au msaada; na kama ni mkopo ni lini zitaaza kulipwa.

Pia alihoji fedha kiasi gani zimetumika hadi kufikia Desemba mwaka jana na kwa kuwa ni fedha za umma zinazokaguliwa na CAG, ukaguzi wake utafanyikaje kwa kuzingatiwa kuwa fedha hizo zilitolewa kwa kampuni binafsi.

Akijibu maswali hayo, Bw. Silima alisema hawezi kuyataja makampuni hayo kwa kuwa ni kuvunja utaratibu kwa kuwa ni siri kati ya benki na mteja.

Katika swali lake la nyongeza, Bw. Mbowe alihoji ni kwa nini kampuni hizo zisitajwe ikiwa zimenufaika na mamilioni ya fedha katika mpango huo, na baadaye Spika Makinda akamtaka Bw. Mkulo kutaja kampuni hizo bungeni, lakini hakueleza ni lini atatakiwa kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2009/10, fedha dola milioni 48, ambazo ni sehemu ya sh. trilioni 1.7 zilizopitishwa na bunge mwaka 2008, kwa ajili ya mpango wa kufufua uchumi, hazijulikani ziko wapi, ambapo alisema wazi kuwa aliomba taarifa juu ya fedha hizo akanyimwa.

Baada ya kutoa taarifa hiyo na kuiwasilisha katika mkutano wa bunge la Aprili, suala hilo liliibuliwa bungeni, ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Kabwe Zitto, alimuuliza swali la nyongeza Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda juu ya mahali zilipo fedha hizo, na kujibiwa kuwa kuwa wakati huo hakuwa na taarifa, huku Spika Anne Makinda naye akimtetea kuwa hastahili kulijibu.

Awali, akijibu swali la msingi la Nyerere, Bw. Silima alisema kupitia mpango huo kampuni 97 zilinufaika kwa kusaidiwa kufidia hasara waliyopata wakati wa msukosuko wa uchumi.

Alisema mpango huo ulikisiwa kugharimu sh. trilioni 1.7 kutoka vyanzo vya ndani na nje ya nchi.

Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni mikopo ya ndani sh bilioni 828 ili kufidia pengo la mapato na sh. bilioni 436.2 zikiwa ni mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na sh. bilioni 428.3 zilitengwa ndani ya bajeti ya serikali kwa ajili ya kulinda ajira, kipato, kuwezesha utoaji mkopo na uwekezaji katika miundombinu na kuongeza kuwa urejeshwaji wa mikopo hiyo utafanywa kwa mujibu wa mikataba iliyoingiwa.

"Kutokana na kanuni za kibenki, si sahihi kutoa taarifa za mteja mmoja mmoja kwa umma kama ambavyo swali la mbunge lilivyotaka," alisema.

Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana fedha zilizokuwa zimetumika chini ya mpango huo zilifika sh. trilioni 1.4535 pengo likiwa ni sh bilioni 239.

"Pengo hili lilitokana na kukosekana kwa fedha kutoka katika baadhi ya vyanzo pamoja na wafadhili mbalimbali. Kwa kuwa fedha hizi ziliingizwa kwenye bajeti ya serikali zitafanyiwa ukaguzi na CAG kama ilivyo kwa fedha nyingine za umma," alisema.
 
Hizo hela kwa nini sisingewekezwa kwenye kuzalisha umeme kwanza? Utakuzaje uchumi katika nchi isiyokuwa na umeme?
 
In an effort to fill the country’s recent revenue collection gaps, the Bank of Tanzania (BoT) has given the government nearly Tzs 600 billion from the stimulus package that was announced last year by President Jakaya Kikwete.

According to Prof. Benno Ndulu, the governor of the BoT, this funding is part of the total Tzs 1.7 trillion stimulus package that was reserved in order to shield the country’s economy from the effects of the global financial and economic crises.

Money from the stimulus package that has been allocated to the government has reportedly been used to support the education, health and agriculture sectors.

In addition, the stimulus plan is intended to be used as a means to directly compensate exporters for losses, to guarantee debt rescheduling, and to increase the loans that are provided to farmers in order for them to obtain seeds, fertilizer and tractors.

Apart from the agriculture sector, other sectors that are critical to the country’s economic stability are also scheduled to receive funds from the stimulus package; these sectors include investment, infrastructure and food security.

Additionally, the government has also reportedly planned to grant guarantees to financial institutions in order to deal with various loans, amounting to Tzs 270 billion, that had been given to companies which they later failed to repay due to the economic crisis.

The terms of the guarantee have been set to extend for 2 years, during which time, based on arrangements that have been made between the government and the financial institutions that have extended these unpaid loans, the firms will not be charged interest on their repayment for the duration of the guarantee.

In a recent interview with The Citizen, Prof. Ndulu indicated that the shortfall in revenue collections has been caused, in part, by the recent global financial crisis, saying that the government had already borrowed Tzs 473 billion from the stimulus package and had also floated bonds that were worth Tzs 120 billion in an effort to further bridge the gap in the country’s revenue collection.

“One aim of the stimulus package was to cover gaps in revenue collection, and we set aside Tzs 825 billion for that purpose,” he said in The Citizen report, “but only Sh600 billion has been solicited so far.”

According to Prof. Ndulu, recent reports, which indicated that approximately Tzs 400 billion of the money that was loaned to the government by the International Monetary Fund (IMF) had been given to local banks, were unfounded.

Prof. Ndulu went on to explain that these funds were not meant to be distributed to local banks, but rather were to be used in order to stabilize the foreign exchange reserve.

In addition, the BoT governor said that no entity, other than the government, had received money from the stimulus fund, but that arrangements had been made in order to guarantee that those who were promised assistance through the fund were given assistance through selected banks, which are scheduled to begin receiving money from the package within a few days.
 
No comments ndio nawapenda watumishi wa Umma wanaoongozwa na serikali ya SISIEMU
 
Na Gladness Mboma, Dodoma

SPIKA wa Bunge, Bi. Anne Makinda amemtaka Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo kuyataja bungeni kampuni 97 zilizonufaika na mpango wa kunusuru uchumi wa Tanzania kutokana na msukosuko wa fedha duniani.

Spika Makinda amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Bw. Pereila Ame Silima kushindwa kujibu maswali ya Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe na mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Leticia Nyerere waliotaka kutajiwa kampuni hizo.

Katika swali la msingi, Bi. Nyerere alitaka kujua ni kampuni ngapi, kwa majina na kiasi gani cha fedha zilizotumika kwa ajili ya kunusuru uchumi wa Tanzania katika kipindi cha mtikisiko wa uchumi wa dunia na fedha hizo zilitoka wapi na kiasi gani kwa kila chanzo.

Pia mbunge huyo alitaka kujua kama kampuni hizo zilipewa mkopo au msaada; na kama ni mkopo ni lini zitaaza kulipwa.

Pia alihoji fedha kiasi gani zimetumika hadi kufikia Desemba mwaka jana na kwa kuwa ni fedha za umma zinazokaguliwa na CAG, ukaguzi wake utafanyikaje kwa kuzingatiwa kuwa fedha hizo zilitolewa kwa kampuni binafsi.

Akijibu maswali hayo, Bw. Silima alisema hawezi kuyataja makampuni hayo kwa kuwa ni kuvunja utaratibu kwa kuwa ni siri kati ya benki na mteja.

Katika swali lake la nyongeza, Bw. Mbowe alihoji ni kwa nini kampuni hizo zisitajwe ikiwa zimenufaika na mamilioni ya fedha katika mpango huo, na baadaye Spika Makinda akamtaka Bw. Mkulo kutaja kampuni hizo bungeni, lakini hakueleza ni lini atatakiwa kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2009/10, fedha dola milioni 48, ambazo ni sehemu ya sh. trilioni 1.7 zilizopitishwa na bunge mwaka 2008, kwa ajili ya mpango wa kufufua uchumi, hazijulikani ziko wapi, ambapo alisema wazi kuwa aliomba taarifa juu ya fedha hizo akanyimwa.

Baada ya kutoa taarifa hiyo na kuiwasilisha katika mkutano wa bunge la Aprili, suala hilo liliibuliwa bungeni, ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Kabwe Zitto, alimuuliza swali la nyongeza Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda juu ya mahali zilipo fedha hizo, na kujibiwa kuwa kuwa wakati huo hakuwa na taarifa, huku Spika Anne Makinda naye akimtetea kuwa hastahili kulijibu.

Awali, akijibu swali la msingi la Nyerere, Bw. Silima alisema kupitia mpango huo kampuni 97 zilinufaika kwa kusaidiwa kufidia hasara waliyopata wakati wa msukosuko wa uchumi.

Alisema mpango huo ulikisiwa kugharimu sh. trilioni 1.7 kutoka vyanzo vya ndani na nje ya nchi.

Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni mikopo ya ndani sh bilioni 828 ili kufidia pengo la mapato na sh. bilioni 436.2 zikiwa ni mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na sh. bilioni 428.3 zilitengwa ndani ya bajeti ya serikali kwa ajili ya kulinda ajira, kipato, kuwezesha utoaji mkopo na uwekezaji katika miundombinu na kuongeza kuwa urejeshwaji wa mikopo hiyo utafanywa kwa mujibu wa mikataba iliyoingiwa.

"Kutokana na kanuni za kibenki, si sahihi kutoa taarifa za mteja mmoja mmoja kwa umma kama ambavyo swali la mbunge lilivyotaka," alisema.

Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana fedha zilizokuwa zimetumika chini ya mpango huo zilifika sh. trilioni 1.4535 pengo likiwa ni sh bilioni 239.

"Pengo hili lilitokana na kukosekana kwa fedha kutoka katika baadhi ya vyanzo pamoja na wafadhili mbalimbali. Kwa kuwa fedha hizi ziliingizwa kwenye bajeti ya serikali zitafanyiwa ukaguzi na CAG kama ilivyo kwa fedha nyingine za umma," alisema.
Ujambazi ndani ya serikali!
 
Hii ni zaidi ya EPA hasa ukizingatia kiwango chenyewe cha STIMULUS PACKAGE. Ikithibitika kama watu wamegawana kiholela tena sidhani kama atabaki mtu katika serikali hii wakuficha sura yake. na dalili zimeshaanza kujitokeza kwani zoezi lilikugubikwa na usiri mzito mno. Hata CAG ameshindwa kupata list ya baadhi ya makampuni!

Hii ni hatari
 
Wanasema, Unapokuwa mwongo usiwe msahaulifu. Anachodai Beno Ndulu na Naibu Waziri wa Fedha vinagongana. Lakini hiyo si issue. Tunachotaka ATUTAJIE MAJINA YA MAKAMPUNI YALIYOPEWA STIMULUS PACKAGE WALA HATUTAKI KUJUA AKAUNTI ZAO ZIKO BANK GANI. WHAT WE NEED IS NAMEZ PLIZZ!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! NO BLABLAA
 
kama kweli mpaka CAG alinyimwa hiyo taarifa basi ni dhahiri kuna namna.....daah!haka ka-nchi wanavyokatafuna lakini kapo tuu!
 
Nadhani mna hamu sana ya kumuona Hamisi Kingwangwala (not sure na spelling ya surname)!!!!!!!!!!!!!!!! alisema mwenyewe lakini walichukua kabilioni kamoja tu!!!!! Marejesho is another topic that was above of that thread.
 
Na baada ya majina ya hao beneficiaries, tunahitaji stimulus package nyingine kwenye sector ya NISHATI kwani madhila yanayosababishwa na upungufu wa umeme ni makubwa kuliko yaliyosababishwa na Kuyumba kwa Uchumi wa Dunia hapa Tanzania. Haikuwa na tija kuwapatia private enterprise mapesa yote hayo wakati sector yetu ya Nishati inasuasua. kama fedha hizo zingewekezwa pale Stiglers Gorge basi tatizao la Umeme ingekuwa ni Historia kwa miongo mingi ijayo.

Kwa wenzetu marekani ambapo ndipo ulipozaliwa huu mpango wa stimulus package, hawakuishia kufidia makampuni binafsi tu bali walienda mbele zaidi kwenye zile sector zinazotoa ajira zaidi, pamoja na kuongeza public expenditure kwenye miradi inayotoa ajira nyingi lakini hapa kwetu watu wameishia kugawana tu.

Nasikia hata makampuni ya watoto wa wakubwa yapo ndani na ndio maana CAG hakuambulia hizo nyaraka. Na nimesikia kama hayo majina yakiwekwa wazi basi majina ya wamiliki halali wa hayo makampuni yatakuwa yameshabadilishwa katika Index of Registration pale Brela

Watanzania tuamke sasa
 
Hii serikali inapesa nyingi sana za kuchezea lakini haina pesa kabisa za kutatua matatizo ya wananchi wake.
 
Kampuni ni nyingi sana zilizonufaika na Stimulus Package 97? Mie najua angalau moja tu ambayo ilipewa kuwafidia wakulima wa pamba huko Nzega. Kampuni inaitwa MSK - Mama Salma Kikwete. Hebu endeleeni kutaja huenda tukajua hata nusu za kampuni hizo
 
Frankly speeking nilijua tangu mwanzo kwamba huu ulikuwa mchezo mchafu kama ule wa Marekani wa kuwaibia wananchi.Kwa serikali maskini kama ya Tanzania ambayo ni omba omba, nilijiuliza uwezo huo na upendo huo ghafla imeupata wapi.Kwanza serikali yenyewe inakopa kwenye makampuni ya ndani ambayo sijui kama ni hayo iliyo yakopesha,kama kweli imeyakopesha.

Back
Top Bottom