Hii ni dhihaka kwa wakristo na ikemewe

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,225
157,419
Nimesikitika sana

17951602_10158579884630416_6132469750790083742_n.jpg


Duh jaman! Yesu gani na chupi hiyoo? Yesu anapewa na kinasa sauti (mic)???
 
Nimesikitika sana

17951602_10158579884630416_6132469750790083742_n.jpg


Duh jaman! Yesu gani na chupi hiyoo? Yesu anapewa na kinasa sauti (mic)???

Hawa uawezekana wanafanya IGIZO lenye ujumbe mzuri tu na sio dhihaka. Wanaomdhihaki YESU tunaishi nao na tunawaheshimu na wengine tunawapelekea sadana na mafungu ya KUMI kila Jumapili. na wengine hutongoza hata wake zetu. Mi sijui wanafanya nini, ili siwezi kuwahukumu kwa picha hii, wanaweza kuwa na ujumbe mzuri tu kwa watoto etc
 
Hawa uawezekana wanafanya IGIZO lenye ujumbe mzuri tu na sio dhihaka. Wanaomdhihaki YESU tunaishi nao na tunawaheshimu na wengine tunawapelekea sadana na mafungu ya KUMI kila Jumapili. na wengine hutongoza hata wake zetu. Mi sijui wanafanya nini, ili siwezi kuwahukumu kwa picha hii, wanaweza kuwa na ujumbe mzuri tu kwa watoto etc
Naungana na ww
 
Mkuu hili ni "Igizo" la Mateso ya Yesu Kristo,ilifanyika Ijumaa Kuu ndugu Bujibuji
Katika kanisa Katoliki kuna kitu kinaitwa "Inculturation" kwa Kiswahili "Utamadunisho" ,kwa wenzetu wa Protestant wanaita "Contextual Theology".

Hii ni ile hali ya kuufanya Ukristo uingie ndani ya utamaduni mahalia,kufanya Liturjia ya Kanisa iendane na mila na desturi za kanisa mahalia.Ndio maana unaona hawa wanaamua kuigiza ili kuufanya Ukristo na ukumbusho wa mateso ya Yesu ktk familia ya kanisa mahalia.

Ni igizo tu la kukumbusha safari ya mateso,kifo na hatimaye ufufuko wa Yesu Kristo.Hii ni kuthibitisha ili "Doctrine Theology" ya kanisa Katoliki inayoitwa "encarnation" yaani "umwilisho",yaani licha ua uwezo wake,bado Yesu aliteseka na kupata maumivu na kuuvaa ubinadamu.

Haya mambo ya utamadunisho yalianza toka enzi za Mitume wa Yesu,pale Mtume Paulo alipokwenda Athens-Ugiriki na kukutana na upinzani mkubwa sana wa kuhoji imani ya Kikristo,ili Wagiriki wa kijiwe cha Aeropagus waweze kusikiliza neno la Mungu,ilimbidi Paulo afanye "utamadunisho" kwa kuingiza ukristo ndani ya tamaduni za Wagiriki ili waweze kuupokea bila hofu.

Mtaguso wa Pili wa Vatican ukaja kutulia mkazo wa Utamadunisho,kulifanya haswa kanisa la Afrika kuuingiza ukristo ukatoliki ndani ya milq na desturi za Waafrika.Zamani mavazi ya mapadre kama kasula,mitro,stola,chingulumu na alba vilitoka moja kwa moja Vatican,lakini baadae "Inculturation" ikaruhusu mavazi hayo yatengenezwe kiutamadunisho,ndio maana leo unaweza kuona kasula ya padre imeshonwa kwa kitenge cha wax,stola ya kitenge au batiki kama asili ya mavazi ya Afrika.

Sasa vifaa vya altareni kama chalisi,chibolio,para nk vinaweza kutengenezwa kwa mti wa mninga na si chuma chenye nakshi ya dhahabu toka Magharibi.Hii yote ni "utamadunisho",yaani kuuingiza ukristo ndani ya utamaduni wa eneo fulani.Pia zamani misa za kanisa katoliki popote duniani zilikuwa zinaongozwa kwa lugha ya kilatini,ndio maana mapadre na waumini wa zamani walikuwa wanajua sana Kilatini,na Seminari ndogo na Kuu somo la Kilatini lilikuwa ni la lazima na unapswa kufaulu,moja ya sifa ya upadre ilikuwa kujua Kilatini cha kuongea na kuandika.

Sisi tuliofundishwa na Mapadre wa kwanzakwanza wa Tanzania,tulibahatika kujua Lugha ya Kilatini kwa sbb ilikuwa ni "lazima" kama vile leo ukianza shule ya Msingi unakutana na somo la Uraia,shule ya Upili ndio Civics,Shule ya Upili ya Juu ndio DS na chuo Kikuu ndio GS.Lakini sbb ya utamadunisho,kanisa likaamua kila kanisa litumie Lugha mahalia ili kuweza kufikisha Injili kwa watu kwa urahisi,ndio maana leo kuna misa na biblia mpaka zilizotafsiriwa kwa Kigogo,Kihehe,Kihaya,Kibena nk

Ulaya misa ni dakika 30,ukizidi sana basi 45....zaidi ya hapo watu wanakuachia kanisa wanasepa.Lakini Afrika misa ni masaa mawili na siku za sikukuu hadi masaa matatu na nusu.Ile Padre kuingia tu inaweza kutumia dakika 20,kwaya wanacheza na watoto wa kipapa wanarukaruka.Kupeleka neno la Mungu kwenye mimbari inavhukua dakika kumi toka nyuma ya kanisa huku watu wanatamadunisha,vipaji watu wanaimba zaidi ya dakika 20.Ngoma zinapigwa kanisani na vigeregere juu...Huu ndio utamadunisho wa kiafrika.Ulaya hukuti haya,watu watakuachia misa.Niliwahi sali Kongo Drc Jimbo la Goma...Watu wanaingia kanisani na vyungu kichwani vinawaka moto kama ishara ya utamadunisho.

Kwa hiyo usishangae,ndio maana siku hizi kuna hata picha za Yesu "muafrika",sanamu za Yesu zitokanazo na mti wa mninga nyeusi tiiiii,ile "Last Supper" ya Yesu na wafuasi wake iliyochorwa na Leonardo da Vinci na sisi tunaitengeneza kwa mti wa mninga.

Igizo hilo lisikutishe,ni matokeo ya "Vatican Council II" i.e Mtaguso wa Pili wa Vatican

Cc Otorong'ong'o SANCTUS ANACLETUS Dominus Vobiscum
 
Kwa hiyo usishangae,ndio maana siku hizi kuna hata picha za Yesu "muafrika",sanamu za Yesu zitokanazo na mti wa mninga nyeusi tiiiii,ile "Last Supper" ya Yesu na wafuasi wake iliyochorwa na Leonardo da Vinci na sisi tunaitengeneza kwa mti wa mninga.
Umenena vyema kabisa....Post hii ina kila aina ya vitamin na virutubisho vyote..

Ahsanta!
 
Back
Top Bottom