Hii ni Dharau kwa Fani ya Udaktari!

Kuna sababu nyingi sana zinazotolewa kuwa zimesababisha mgomo wa madaktari.

Kwa ujumla kuna sababu zaidi ya kumi na mbili ambazo zinahusu uboreshaji wa huduma za afya kupitia vifaa tiba na majengo na uboreshaji maslahi ya madaktari. Kila kimoja kina umuhimu wake, lakini ningependa kujadili hiki cha maslahi ya madaktari kwa kuwa serikali ndio inakitumia kuchezea mpira wake kisiasa. Serikali haizungumzii kabisa kuhusu uboreshaji wa mazingira ya kazi, kama ukosefu wa vifaa tiba. Hadithi ni ileile kwamba serikali inajitahidi hatua kwa hatua kuboresha mazingira ya kazi na pia maslahi ya madaktari.

Kwa wengi wetu tunajua kwamba kusini mwa jangwa la Sahara kuna baadhi ya nchi ambazo zinajali sana maslahi ya madaktari wao kwa mpangilio ufuatao: Msumbiji, Rwanda, Botswana, Namibia, Angola na Afrika ya Kusini. Ukiacha Afrika ya kusini, aghalabu hizi nchi hazina uchumi wa kutisha, tena nyingizo zimekuwa katika machafuko ya muda mrefu.

Moja ya sababu kubwa sana kwa nchi za Botswana na Namibia kuwalipa madaktari wa kigeni mishahara mikubwa ni kutokana na upungufu mkubwa wa madaktari wazalendo katika nchi tajwa. Ni kawaida sana kwa vijana wa Kibotswana na Kinamibia kuwasikia wakisema kwanini wasome miaka mitano hadi sita chuoni ili tu kutengenezwa kuwa madaktari wakati akitumia miaka mwili hadi mitatu kupata diploma au digrii ya mambo ya utalii, ualimu, uchumi na fedha atalipwa kiasi kama anachopewa daktari wa digriii tena akiwa hajapoteza muda zaidi ya daktari. Sababu kama hizi zimesababisha vijana toka nchi tajwa kukosa morali ya kujiendeleza katika masomo ya sayansi hasahasa udaktari kwa kuwa wanaona wanapoteza muda kwa malipo madogo au yasiyotofautiana na taaluma nyingine zinazotolewa kwa muda mrefu. Kwa sababu hizi, madaktari wengi toka Afrika ya mashariki, yaani kenya, Uganda na Tanzania wameweza kukimbilia huko kwa wingi kwa kuwa mshahara nchini kwao ni midogo.
Sehemu kubwa ya dunia, madaktari kulipwa mishahara mikubwa kwa sababu husoma mara mbili zaidi ukilinganisha na baadhi ya taaluma. Hivyo hii ni motisha sana kwa wale wanaotaka kusoma kozi kama hizi, ili tusizidi kuwa na upungufu wa watu katika fani husika. Lakini pia vyuo vinavyofundisha udaktari huwa ni ghali sana ukilinganisha na taaluma nyinginezo na hivyo huhitajika walipe mikopo yao jambo ambalo pia Tanzania linahusu, ingawa wanafunzi wa sasa wanapewa udhamini kwa asilimia mia (wale wa nyuma kuanzia wahitimu wa mwaka 1994 hadi 2009 hawakusomeshwa bure, na hivi karibuni majina yao yalitolewa na bodi ya mikopo kama wadaiwa).

Madaktari kama walivyo wahandisi walikuwa ni wanafunzi wazuri sana toka wakiwa katika elimu za awali, na kwa bahati mbaya fani hizi hazina watu wengi sana kwa kuwa hupatikana kwa ushindani mkubwa, hivyo uhitaji wao huchangia katika kuwa na mishahara mikubwa kitu ambacho ni tofauti sana nchini kwetu ambapo tuna upungufu mkubwa wa madaktari na tungali tunawalipa pesa ndogo.
Katika nchi zilizoendelea, madaktari wanaofanya kazi vijijini hulipwa zaidi ukilinganisha na wale walioko mjini; labda sababu kubwa ni kuwa huduma za afya zinatolewa na sekta binafsi zaidi, wakati hapa nchini Tanzania zinatolewa zaidi na serikali hivyo kukosa nguvu za majadiliano na ushindanisha wa mshahara.

Ninashangaa sana kwa kiongozi mkubwa kama Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli za kukatisha tamaa kwa kada muhimu kama za madaktari. Kauli ambazo zinapunguza morali kwa wanafunzi walioko ngazi za chini sasa, kwamba daktari hawezi akalipwa zaidi ya kada nyingine. Hivi ni nani atataka mwanae akatumie zaidi ya miaka mitano kusomea digrii ya udaktari halafu mwisho wa siku akalipwe kama mtu aliyesomea digrii ya miaka mitatu? Hakuna hata mmoja, kwa kuwa huko kutakuwa ni kujitoa kunakozidi kipimo. Sasa tuwape motisha gani watu wanaosoma kozi za miaka mingi na ambazo ni muhimu zaidi kwa taifa letu? Ni kuwapa mazingira bora ya kufanya kazi, na pia kuwa na mishahara mikubwa zaidi ya wale wanaosoma kozi nyingine za muda mfupi.

Rais akiwa kama kiongozi wa nchi hii, anawajibika katika kupanga mipango endelevu ya afya ya nchi na si kuangalia kwa ufinyu wa mawazo kwa kipindi anachotaw
 
nimechoshwa na kauli eti daktari anapendelewa kwa kulipwa sana
........hebu nisaidieni mishahara ya hawa watu kwa level ya degree wanalipwa ngapi
........tanapa
.........tra
..........bot
........bandari
.......hazina
..........msd
..........nhif
..........kilimo
..........mahakama
.........ubalozini/mambo ya nje
..........etc....etc...
Acha upotoshaji wa kihuni, una hakika kuwa hao wote uliowataja hapo juu wanalipwa laki 9 kwa mtu anayeanza kazi leo.?? Hapo kuna ambao wanaanzia na laki 4.5 anapoanza kazi.
 
Mimi sio muamini wa serikali hii kutokana na baadhi yamambo mengi ambayo hayako sawa, ila kwa hili la madakitari kutaka kulipwa mara nane ya watumishi wengine wa umma wenye elimu sawa nalikataa. Natambua umuhimu na ugumu wa kada ya udakitari, lakin haiwezi kupelekea kujenga tofauti kubwa kiasi hicho kimasilahi na kada zingine. Kupigania hali bora mazingira ya afya nchini ni muhimu, lakin hayaweza kuboreshwa kwa muda mfupi hivyo, lakini pia haiwezi kuwa sababu ya kuacha watu waendelee kufa kwa kukosa matibabu
 
TELO

Usibishe bure mkuu. Tutorial Assistant anayeanza kazi mshahara wake ni mdogo lkn unazidi wa daktari. Ukweli ndo huo
 
Last edited by a moderator:
Amesema hata kama ni mtu kutoka ndani ya serikali kafanya hivyo, basi ni kwa matakwa yake mwenyewe
 
Kikwete! Sijui anaamini Mungu yupo? Mimi naona kama vile anakaribia kupata aibu kuubwaa! Mark my word!
 
Mungu huadabisha waovu, kwa kitu walichomfanyia dr uli, watatambua kweli GOD IS ARLMIGHTY! Subirini kidoogo tuu!
 
ITEGAMATWI

kikwete mwenyewe alisema unapoangalia kiwango cha mshahara unaconsider muda wa mtu kusomea fani hiyo na umuhimu wake kwa jamii sasa umbumbumbu unautoa wapi? hata libya ya ghadafi unakuta dokta alimzidi mshahara waziri!! professa sawa kasoma muda mrefu kuliko daktari na majimarefu nae kasoma muda mrefu kuliko daktari? halafu inategemea professa wa nini huwezi kufananisha prof wa kiswahili na prof wa cardiology,
 
Last edited by a moderator:
Wabunge kulipwa mil 10 haf wabunge wenyewe akina komba,bukwimba,shibuda,maji marefu,lùsinde and co unalinganisha vp na wa2mishi wengine wa uma?
 
TELO

Kwa hiyo wewe uanakubaliana na hoja dhaifu za seriakli kwamba haina hela? kwa nini haina hela. Let them put their priorities right wakusanye kodi sawasawa. Milioni tatu na nusu itawezekana km hata kwa kada nyingine.

Lazima tuipe changamoto serikali ifikirie zaidi namna ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Inawezekana kabisa ila kwa vile na wewe unakubaliana na ngonjera za serikali kwamba hakuna hela basi. Milioni tatu na nusu ni kitu gani km kodi zikitozwa inavopaswa na matumizi yasiyo ya lazima yakaondolewa ambao kila siku watu wanapigia kelele?

Serikali iamke ichemshe bongo, iache kuendesha mabo kimazoea hela zipo.
 
Last edited by a moderator:
Mimi sio muamini wa serikali hii kutokana na baadhi yamambo mengi ambayo hayako sawa, ila kwa hili la madakitari kutaka kulipwa mara nane ya watumishi wengine wa umma wenye elimu sawa nalikataa. Natambua umuhimu na ugumu wa kada ya udakitari, lakin haiwezi kupelekea kujenga tofauti kubwa kiasi hicho kimasilahi na kada zingine. Kupigania hali bora mazingira ya afya nchini ni muhimu, lakin hayaweza kuboreshwa kwa muda mfupi hivyo, lakini pia haiwezi kuwa sababu ya kuacha watu waendelee kufa kwa kukosa matibabu

Mimi nadhani mafisadi na watafuna nchi ndiyo tayari wameunda matabaka katika jamii.
 
Kwa mujibu wa mazungumzo ya mwisho wa mwezi yaliotolewa na raisi JK kwa watanzani,bwana ulimboka si muajiriwa wa serikali ila alichaguliwa kuwasemea madaktari!
Hii sielewi imekaaje,
yani jopo lote la madaktari nchini hakukua na mtu thabiti wakufanya hili?
 
Mimi napenda ukweli (facts) na siyo upotoshaji. Wewe ulipoleta hoja ya kujustify malipo ya mil.3.5 kwa madaktari wanaoanza kazi ulisema kwamba wewe ni Ass.Lecturer wa UDSM na kusema mengi. Mimi nilichofanya ni kuleta figure na ukweli wenyewe.

Mimi naomba wasomaji waelewe kwamba mimi sipingi madai ya Drs wetu, lkn najaribu kuona nini justification ya wao kudai 3.5 mil.?, ukiangalia series ya yale madai utagundua kwamba priority haikuwa mazingira ya kazi bali madai binafsi. Madai yao ni ya msingi, lkn nashawishika kuamini kwamba Drs hawakuwa na timu nzuri inayoelewa nini cha kunegotiate na serikali. Wao walikwenda kwenye negotiations kama watu wa kwenda kutoa maelekezo basi. Na hili mimi ndiyo nashawishika kuamini kwamba Drs wetu hawajafanikiwa kwenye madai yao kwasababu hawakuwa na timu iliyojiandaa na kujua nini tofauti kati ya negotiations na madai. Kwenye negotiations lazima uweze kujustify offer zako na si kutoa maelekezo.
we umekazania madokta hawakwenda kufanya negotiation je serikali ambayo ilienda kufanya negotiation ni ambayo ilisema madai ya madokta ni ya msingi ilifika dau gani madokta wakakataa? inaposema itaongeza 15-20 percent huoni nayo inakuwa inakuja na order kwenye meza ya majadiliano?
 
Back
Top Bottom