Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ulinzi ya Knight Support,David Sutton akitishia kuondoka kikaoni kwa ghadhabu baada ya Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Jenerali Matwani Kapamba (kushoto)kumueleza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Shamsi Vuai Nahodha (Mwenye suti aliyeketi ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa na Waziri Kiongozi Mstaafu SMZ)kuhusu kampuni yake,wakati waziri huyo alipotembelea kampuni hiyo ikiwa ni sehemu yake ya ziara kwa kampuni mbalimbali binafsi za ulinzi na uokoaji,Dar es Salaam.Picha na Fadhili Akida
Verdict:
Du! Kweli sikitiko eeh sikitiko limetupata Watanzania, kuwa sasa mambo yamefikia hivi! kudadeki! siamini macho! hata wageni wanaona kila kitu kipo shaghalabaga! kiasi wanaweza leta zogo 'high-table' mbele ya 'kadamnasi', maana tunajua mambo yalikuwa yanafanyika kwa kificho kati ya serikali na wawekezaji lakini sasa mambo hadharani! Watanzania 2015 lazima kubadili chama na mfumo mzima kama tunataka kujinasua kutoka 'janga hili'.