Hii ni dalili ya kukata tamaa au ni ujasiliamali baada ya kupigika na maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni dalili ya kukata tamaa au ni ujasiliamali baada ya kupigika na maisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hofstede, Jul 31, 2010.

 1. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ukweli utaendelea kubaki kuwa, ili mtu aweze kuishi ana hitaji kazi ambayo ni "shughuli yoyote ya halali inayoweza kumpatia riziki yake". Suala la ajira kwa vijana na wananchi limeonekana kuwa ni bomu linalosubiri muda wake lilipuke. Kama mtu anaweza kuchukua risk ya kuweka maisha yake rehani ili mradi tu aweze kupata kitakachopatikana ili mkono uende kinywani basi ni dhahiri kuwa mtu huyo amekata tamaa ya maisha.

  Suala kubwa hapa ni kuwaandaa vijana kukabiliana na maisha yao kihalali, ikiwa ni pamoja na kuwajengea mazingira ya kujiajiri, mashambani na katika shughuli mbalimbali. Hili ni tatizo linalohitaji uongozi wa nchi kulipa kipaumbele kama janga la Taifa na kuelekeza nguvu zao huko.

  Hebu muangalie huyu jamaa alivyojiweka rehani kwa mchezo ambao ungeweza kuchukua maisha yake kabla hata ya kufanikiwa alichokitaka au wananchi wenye hasira wangemuotea. Kweli vibaka, majambazi si watu wa kupewa nafasi lakini kwangu mimi huyu namuona ni mwenye njaa, anayetafuta chakula kwenye mashamba ya watu wengine. H

  Haiingii akilini hata kidogo kuinganisha risk na return ambayo angepata kama angefanikiwa alichokihitaji. Angekuwa na SMG huyu angekuwa ni tishio kubwa lakini huenda hajaipata kwani inaoneka yupo tayari kwa lolote. Huu ni wakati sasa wa kuwaangalia watu kama hawa, maana kama Marehemu Prof. Chachage S. Chachage alivyokuwa akiamini ni kwamba "Bila ya watu kama hawa kuwa na maisha mazuri sisi wote hatupo salama"  Credit ya video: HABARI NI HABARI NDUGU YANGU
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,955
  Likes Received: 21,106
  Trophy Points: 280
  kazi kweli kweli.........
   
Loading...