Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Kwanza ni chama ambacho kinakuwa na sera ambazo hazina manufaa kwa taifa na wananchi wake,sera ambazo zinapinga maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Chama ambacho kimefilisika kisiasa kinakuwa na mgombea ambae anaropoka hovyo majukwaani bila kujua athari ya mambo anayoyaropoka. Mfano anasimama jukwaani anasema nikiwa rais nitaruhusu watu kuuza mazao nje wanavyotaka. Je hajui kuwa mazao yakiuzwa hovyo kutaibua mfumuko wa bei ndani ya nchi yake? Hii ni sababu wafanyabiashara watauza bila mpangilio mazao nje ya nchi na kusababisha uhaba mkubwa.
Chama kilichofilisika kisiasa kinakuwa na mgombea ambae anasimama jukwaani na kusema ni makosa kuhoji vitambulisho vya uraia kwa wageni wanaoingia nchini au raia ambao wanahisiwa kuwa sio watanzania hasa wanaokaa mikoa ya mipakani. Je mgombea wa chama kama hiki hajui umuhimu wa usalama wa taifa lake dhidi ya wakimbizi au raia wanaoingia isivyo kihalali hapa nchini?
Chama kilichofilisika kisiasa kinakuwa na wanachama na wafuasi ambao ni mbumbumbu,maana wao wanakuwa kama Nyumbu anapokuwa porini,maana hukimbia hovyo kwa kufuata kundi bila kutumia akili, Nyumbu anaweza kuvuka mto hata kama kuna Mamba kisa tu anaona kundi la Nyumbu wenzake wanavuka mto.
Chama makini hakiwezi kuwa na wanachama na wafuasi ambao wakimsikia mgombea wao anasema ndege za Atcl zilinunuliwa bila kufuata utaratibu wa manunuzi na pesa hazikupitishwa na bunge,wao wanakurupuka mitaani na kwenye mitandao kuanza kushabikia uzushi ambao hauna ukweli,wanaudandia kama hoja yenye mashiko.
Chama makini hakiwezi kuwa na wanachama na wafuasi ambao wakishapewa majibu kuwa Bunge lilipitisha pesa za kununua ndege za Atcl,ghafla wanataka waonyeshwe mikataba. Je mikataba ya nchi huwa inawekwa hadharani kwenye magazeti au mitandao ya kijamii?
Kwa muktadha huu ni dhahili kuwa Chadema imefilisika kisiasa haina wanachama na wafuasi wenye kutumia akili,bali wamebaki kuwa watu wa kukariri uzushi na uongo bila kutumia common sense. Je chama kama hiki kitapata hata madiwani mwaka huu?