Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli

Charlzdeo 97

Member
Feb 17, 2020
13
9
Habari Mh rais Dr John Pombe Joseph Magufuli, Pole kwa majukumu mazito ya nchi kwa maana ya kitaifa na kimataifa kwa ujumla.

Awali ya yote tunatoa pongezi za dhati kabisa kwa serikali yako ya awamu ya tano, chini ya uongozi wako kwa kazi nzuri ulizozifanya na unazoendelea kuzifanya katika kuliletea maendeleo taifa letu, tunaona miradi mikubwa ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo usafirishaji na uchukuzi kama vile ufufuaji wa shirika letu la ndege ATCL ikiambatana na ununuzi wa ndege mpya kabisa.

Ujenzi wa reli mpya kabisa ya umeme (SGR), uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara kuunganisha mkoa na mkoa na kurahisisha mawasiliano,ujenzi wa barabara za juu (flyovers), Upitiaji upya wa mikataba na uboreshwaji wa sheria za madini hii ni kuhakikisha tunalinda rasilimali zetu na kunufaika kama nchi, mradi wa usambazaji wa umeme vijijini REA kupitia wizara ya nishati, haya ni machache tu katika yale mengi unayoyafanya.

Dhamira yako ya dhati na hulka ya kujitoa bila kujali hali hii inadhihirisha kua wewe ni mzalendo wa kweli.

Barua hii ya wazi imeandaliwa na sisi vijana 305 wa JKT tulioshiriki katika miradi mbalimbali ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa UKUTA wa Mererani, nyumba 41 za kikosi cha ulinzi wa Rais Buigiri Dodoma, ukuta wa Ikulu Dodoma na ujenzi wa ghorofa 12 za askari Magereza Ukonga Dar es Salaam uliyoikabidhi JWTZ kupitia kamandi ya JKT. Kama unakumbuka mnamo April 13, 2019 wakati wa makabidhiano wa nyumba za mji wa kiserikali pale Mtumba Dodoma ulifurahishwa na kazi nzuri tulizozifanya ukaguswa na kutoa zawadi ya ajira kwa vijana tulioshiriki katika miradi.

Mnamo mwezi wa tisa agizo lako lilitekelezwa na vijana tulipelekwa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS Kihangaiko Sept 7, 2019 mchakato wa usaili ulianza na kumalizika Oct 19, 2019. Hatutosahau Nov 28, 2019 vijana 305 tulisomwa kama UNFIT na kurudishwa nyumbani, lakini la kuumiza zaidi ni kauli ya kuambiwa tukajitibie, swali la kujiuliza tutajitibia vipi na uwezo wa kifedha ni mdogo?

Ukizingatia matatizo tuliorudishwa nayo ni yale tuliyoyapata moja kwa moja kwenye miradi kwa maana ya kimazingira na kazi ngumu tulizokua tukizifanya.

Lengo la kukuandikia Mh rais kama baba yetu na kama mzazi wetu tunaomba utusaidie vijana wako na utufikirie, sio tu kwa kurudishwa kule RTS tulipotoka la hasha bali kwa sehemu yeyote ile utakayoguswa na kuona tunaweza kufit, baba yetu wengi wetu sisi ni watoto wa masikini na wazazi walitutegemea sisi katika kuwainua ila matokeo yake tumekua mzigo kwa familia zetu.

Hatukupenda kufikisha kwako ujumbe huu kupitia huku lakini tulifanya jitihada nyingi kufikisha kilio chetu toka mwezi wa kumi na moja na kipindi upo mapumzikoni Chato kwa kutumia viongozi na wakubwa wa kiserikali na kupitia vyombo vyako vya usalama lakini mambo yalikua magumu na vikwazo vingi ila kupitia barua hii ya wazi tuna amin utalipata nakulifanyia kazi.

Tuna kutakia kazi njema na afya njema baba yetu kipenzi na raisi wetu mpendwa Dr John Pombe Joseph Magufuli

Mungu ibariki Tanzania.


IMG_20190119_153554.jpg
 
Daaa, mmepambana kwakweli kwanza Hongereni.

Pili napenda niwasihi vijana wangu, mtambue kuwa mojawapo ya kanuni mbaya sana katika utumwa ni kumtumia alafu akionekana kuchuja unamuuza au kumtupa akafie mbali.

Nyie hamkuwa na wala siyo watumwa na mmetumika kwenye special selection party ya kutumika ipasavyo, ila kutokana na kutumika mmepata madhara ya cement, vumbi, kuumia nk, jeshini ukiwa na madhara basi hauna nafasi.

So nawaomba ikitokea majibu yenu kutopata mwitikio mzuri, tengenezeni mfumo wenu wa uzalishaji kutokana na sehemu mlizopitia.
 
Hilo swala la nyie kuwa UNFIT shida ilikuwa ni nini hata???...maanake it doesnt make sense vijana 305 wote muwe na mapungufu...kama mlikuwa UNFIT hiyo miradi mlifanikisha vipi....?????
Ni swala ambalo ni gumu kdg kulizungumzia hum kiundani zaidi lakn kikubwa kilio chetu tunahitaji kimfkie mheshimiwa Rais Ntashkuru kma utakua na msaada na hlo hata kuweza kushare.
 
Tulia soldier wenzako walichimba vyoo kwa babu wa loliondo na kutengeneza mahanga mapya vikosini na walitoswa wengine wakajakuandamana hadi viaongozi wao wakasetwa ndani lakini bila bila mpaka sasa wako uraia serikal haina hata habari nao.

Ukitaka kujua mko wengi siku ike mkuu wa mkoa wa daslam makonda aliwaita ndio ungejua kuwa kuna jeshi nzima uraiani huko hawana kazi.

Tena hilo jeshi uondoe kabisa waioko suma maana wao hawakujitokeza
 
Kazi ngumu mapigo ya moyo yanaongezeka na presure hapo hapo.
Sisi kuna walioenda kabisa mafinga kipindi hicho walikuwa mafundi seremala na ujenzi wote walirudishwa unfit eti
Hilo swala la nyie kuwa UNFIT shida ilikuwa ni nini hata???...maanake it doesnt make sense vijana 305 wote muwe na mapungufu...kama mlikuwa UNFIT hiyo miradi mlifanikisha vipi....?????
 
Hii habari ningekushauri uiweke kwenye (jukwaa la siasa) huko najua watu wake mlengwa uliye mwandikia ambaye ni Rais wanapita pita sana kule so wataiona tu watampelekea ujumbe.
 
Back
Top Bottom