Hii ni bahati, balaa au mkosi

Mkaa Mweupe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
654
183
WanaJamii,

Naomba mnijuze, kuna watu waliopata kusoma sekondari (O-Level) pale Forodhani au Tambaza, afu wakapitia High School pale Mkwawa.

Wengi wenu nadhani mpo katika hii JamiiForum. Sasa baada ya muda wakati shule zote hizi ni non-existance watoto wako watakuelewa kweli ukiwaambia eti ulisoma mpaka form six wakati shule zenyewe hazipo? Au watakuona unawazuga?
 
masikini ya Mungu, utazinduka kukiwa tayari kumekucha, ngoja nikuache hivyohivyo!!!!!!!!!!
 
Kuendelea kuniacha sio suluisho mie naomba mnifumbue, hii maana yake nini?

mana yake ni kuwa yale kama majengo ni assets zinaweza kutumika kadiri inavyoonekana kuwa vyema kulingana na wakati. elimu uliyopata haifungamani na majengo hayta kidogo kama ingekuwa hivyo, waliosomea chini ya miti wangekuwa na mkosi ama balaa kubwa zaidi. acha ufahari wa kittoto sijui mi nilisoma wapi siui inte skuli mara santa naii, ayasaidii hayo mkuu
 
WanaJamii,

Naomba mnijuze, kuna watu waliopata kusoma sekondari (O-Level) pale Forodhani au Tambaza, afu wakapitia High School pale Mkwawa.

Wengi wenu nadhani mpo katika hii JamiiForum. Sasa baada ya muda wakati shule zote hizi ni non-existance watoto wako watakuelewa kweli ukiwaambia eti ulisoma mpaka form six wakati shule zenyewe hazipo? Au watakuona unawazuga?

Mkuu tatizo liko wapi hapa? Si vyeti utakuwa navyo? Unawaonyesha vyeti na kuwaelezea hayo mabadiliko watakuelewa tu. Hivi sasa kuna wengine shule zao za Msingi zimebadilishwa na kuwa sekondari kwahiyo hakuna tatizo kabisa, hayo ni mabadiliko tu ya kawaida hakuna cha bahati wala mkosi hapo.
 
Yep, umesoma wapi doesn't really matter!!! what matters is that you went to school up to a certain level and that is it. Buildings are not part of your brain Sir!!!!!
 
Utawaeleza tu kwamba nilisoma shule fulani na sasa hivi imekua chuo ataelewa tu na pia vyeti vipo kwa hiyo its very simple kuelewa.
 
Hadithi za mapokeo mbona zinakubalika? Kwani tunaposimulia tulitawaliwa na Waarabu, mara Wajerumani nk tulikuwepo, si mapokeo tu!! Hata ndugu zangu waliosoma Chuo Kiku cha Port au Prince huko Haiti mbona kimesambaratika, wataripoti nini? Kinachotakiwa ni kuwa muwazi na kuwaeleza hao wanaokuhusu kuwa, licha ya hizo institution kufutika/kubadilishwa matumizi, lakini ni ukweli ndiyo nilisoma huko.
 
Utirio si unao kichwani? Cheti ni karatasi tu hata akina Nchimbi wanavyo!
 
Mwanangu utirio umelala ile mbaya ila hofu yangu ni enzi zileee, na mimi nasoma shule aliyosoma mama/baba si unajua sifa za kitoto!
 
Mkuu tatizo liko wapi hapa? Si vyeti utakuwa navyo? Unawaonyesha vyeti na kuwaelezea hayo mabadiliko watakuelewa tu. Hivi sasa kuna wengine shule zao za Msingi zimebadilishwa na kuwa sekondari kwahiyo hakuna tatizo kabisa, hayo ni mabadiliko tu ya kawaida hakuna cha bahati wala mkosi hapo.
hapa ndipo nashindwa kutafsiri mambo kutoka jf hii mada ina maana gani,ujuaji mwingi.......
 
Lengo kuu la hii mada ni kuweza kukufikirisha. Kuna mambo katika maisha ambayo unaweza kusema kuwa yanatokea kama uliwahi kuota. Ila maisha ya mwanadamu yalishaandikwa.

Ukiwa na uwezo wa kusoma alama za nyakati unaweza kujua kabisa wewe ni mtu wa aina gani. Kuna baadhi ya watu kila mahali wanapokanyaga wakitoka lazima kutakuwa na anguko. Hivyo basi ukishawajua watu wa aina hiyo inabidi ukae nao chonjo.

Kuna watu wengine wanakuwa na maisha yanayofuta historia kabla hawajafa, hii hata na wao wakifa wanasahaulika kabisa (Sijui kwa nini!) Hii philosophy ni ngumu kidogo kuielewa, nimejaribu kuwashirikisha wanaJamii.
 
Mkaa mweupe

iko kazi....:confused:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom