Hii ni awamu ya CHADEMA kufutika kama chama kikuu cha upinzani nchini

Hoja ya msingi sio CCM wanatumia njia gani bali hoja ya msingi ni kweli CHADEMA inadhoofika?
Mbinu kwa nini isiwe hoja ya msingi, mbinu inayotumika ni very unsustainable, mkataba wa Magufuli na Mungu ukiisha ndio mwisho wa hiyo strategy. Tengeneza mfumo ambao utafanya watu wakatae upinzani ( kama ipo) na sio kununua watu. Au hukumbuki kuwa hata biashara ya utumwa ilishamiri duniani lakini haikuwa sustainable, leo imebaki history.
 
Hizo ni ndoto za mchana kweupe. Kwa mwenye akili kama yako,ataamini hivyo,Ila ukweli ni kwamba CCM wanatengeneza CHADEMA imara kuliko wakati mwingine wowote

If you don't believe me, take my words
Ni kweli kabisa,wanatengeneza chadema imara ,lakini pamoja na u imara wa CHADEMA je watafanikiwa kupewa nafasi ya ubunge hata mbunge mmoja 2020?
 
Mwisho wa maisha ya kiumbe duniani huelezewa kama "Kufa" au "kuuawa/kuuliwa".

"Kufa" ni ahadi ya Mungu.
"Kuuawa/kuuliwa" ni uhalifu wa kibinadamu au wanyama.

Kwa muktadha wa bandiko lako ungeandika, "HII NI AWAMU YA CHADEMA KUULIWA/KUFUTWA KAMA CHAMA CHA UPINZANI NCHINI"
 
Chadema itaweka pingamizi kwa mgombea uraisi wa CCM...hakuzaliwa Tanzania kama katiba inavyotaka sifa za mgombea uraisi...

85.-(1) Mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya
madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa
Katiba hii na sheria iliyotungwa na Bunge;
Tena kesi ikafunguliwe EACJ hawana ujanja hao ...ila Upinzani kama CCM B wakati mwingine
 
There’s a saying that goes like: Once is chance, twice is coincidence, third time is pattern.

Nimeanza na angalizo hapo juu ili kuwasaidia wale ambao watadhani andiko langu ni kama ramli bila kuangalia ukweli wa historia.

Kwa wale wanaojua vizuri historia ya siasa za Tanzania lazima watatambua kuwa kila utawala mpya unaongia madarakani kwa tiketi ya TANU/CCM huhakikisha unafuta nguvu ya chama kikuu kilichokuwa cha upinzani na huibuka chama kingine kuchukua nafasi hiyo.

Mkakati huu hufanikiwa sana kwa sababu TANU/CCM ni Chama Dola na pia migogoro ya kiungozi ndani ya chama kikuu cha upinzani. Ninaposema CCM ni Chama Dola nina maana kuwa huwezi kuitenganisha CCM na ‘’Kitengo’’. Kitengo kwa lugha ya kiingereza kinaitwa Deep State. Swali labda utauliza, kwa nini huwezi kuitenganisha CCM na Kitengo (Deep State)? Jibu fupi ni kwa sababu Taifa letu limeundwa katika muundo huo.

Ifahamike kuwa chama kinakuwa ni kikuu cha upinzani kama kina wabunge na madiwani wengi. Ikumbukwe pesa za ruzuku zinategemea wingi wa Wabunge, Madiwani na kura za Urais. Huwezi kuendesha kwa mafanikio chama cha siasa nchini bila pesa za ruzuku toka serikalini.

Katika utawala wa Mwl. Nyerere mwaka 1961 kulikuwa na chama kikuu cha upinzani kulichoitwa ANC chini ya Zuberi Mtemvu lakini kufikia mwaka 1965 Rais Nyerere akawa amekifuta katika uso wa dunia.

Tuliona katika utawala wa Rais Mwinyi kulikuwa na NCCR-Mageuzi ambayo ilikuwa ni chama kikuu cha upinzani.

NCCR-Mageuzi iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya Rais Mkapa kuingia madarakani mwaka 1995 alihakikisha nguvu ya NCCR-Mageuzi kama chama kikuu cha upinzani inapotea nchini.

Kwa kudhihirisha hilo tuliona katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 NCCR-Mageuzi ikizikwa kama chama kikuu cha upinzani ambapo chama cha CUF chini ya Prof. Lipumba kiliibuka kuwa chama kikuu cha Upinzani nchini.

CUF iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini ambapo Rais Kikwete alichaguliwa kuwa Rais huku CUF ikiendelea kuwa chama kikuu cha upinzani.

Baada ya kuingia madarakani, Rais Kikwete alihakikisha nguvu ya CUF inapotea kama chama kikuu cha upinzani nchini.

Kwa kudhihirisha azma hiyo tuliona katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 CUF ikizikwa kama chama kikuu cha upinzani nchini ambapo CHADEMA kiliibuka kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi na CUF, tumeona CHADEMA ikiingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani na kutoka bado ikiwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kama historia inavyobainisha basi kifo cha CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani ni baada ya Uchaguzi Mkuu 2020.

Kwa wale wanatumia upeo mkubwa katika kuchambua na kuchanganua masuala ya kisiasa nchini watagundua kuwa dalili za CHADEMA kupotea kama chama kikuu cha upinzani nchini zimeanza kujionesha.

CHADEMA demise is a real thing, and it's happening now!

Hoja iliyoko mbele yetu kwa sasa ni chama gani kitachukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini baada ya Uchaguzi Mkuu 2020?

Ni chama gani kinaandaliwa kwa sasa ili kuchukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kama ambavyo CUF iliandaliwa kuchukua nafasi ya NCCR-Mageuzi na CHADEMA kuchukua nafasi ya CUF?

Nadhani wanaotumia 3D thinking and reasoning wamejua ni chama kipi kinaandaliwa kuchukua nafasi ya CHADEMA!
Ha ha haaa! Ruksa kuota; na kuokoteza matukio bila kuzingatia mazingira ya matukio.
 
Hoja ya msingi sio CCM wanatumia njia gani bali hoja ya msingi ni kweli CHADEMA inadhoofika?
Namjibia huyo jamaa mfano ni mimi mwenyewe nilikuwa upande wa watu Wenye mawazo mbadala wa wastani lakini kutokana na visa vya hovyo vinavyofanya na fisiem wakiongozwa na mkuu wao Pombe aka mdindifu sasa naipenda CHADEMA kindaki ndaki.

Tatizo mdindifu anafikiri upinzani ni viongozi wa juu wa vyama hapo ndipo akili yake ilipogota, amesahau wapinzani ni sisi wananchi ambao ni zaidi ya million 10 na upinzani unazidi kukua mioyoni mwa watu.
 
ACT ndiyo itainuka baada ya kifo cha CHADEMA, ambayo sasa hivi ishaanza kupotea
Chadema kitauliwa na vitu viwili tu 2020
1.Tume
2.Vyombo vya dola
Ila Trust me,CDM na upinzani wana wapenzi wengi mno(na hasa kipindi hiki).Sahau hiyo sijui Juhudi za....Huu utawala watu wengi wameumia hata kuliko uliopita.Walimu ilikua ukimaliza chuo ajira njenje,Watumishi madararaja$mshahara kupanda,njoo wafanyabiashara,Wakulima mazao bei ni ya kutupa.Sema tu sababu upinzani now upo Frustrated ila wangekua Active kuzuia hujuma ndogondogo hakika wana mtaji wa watu hata kuliko huko nyuma
 
Unaota.Zama zimebadilika.CHADEMA haiwezifutika.Ina mamlilioni ya wafuasi ambao siyo wanachama.Kama HAZINA KUU iko vizuri,wanunueni viongozi wao wote na wanachama wao 90% kabla ya 2019.Yaani bakizeni angalau wanachama wachache watakaowakilisha hicho chama katika chaguzi.Halafu WEKENI ULINGO SAWA WA SIASA.Hao pilisi kuna siku watachoka.Anzeni kujifunza kabla hawajachoka.Mzee Kikwete alitimiza wajibu wake,wa kuwatahadhalisha kuacha kutegemea polisi,lakini inaonekana CCM ni sikio la kufa.ITAKUFA.
 
Ndugu siku zinavyozidi kwenda uwezo wako wakuchanganua mambo umewa low kweli kweli ujinga huu ukimwambia jamaa yako anaechezea Kodi kwa mambo yakijinga akikusikia atakudharau sana
Ndugu wala usisumbuke na uwezo wangu!

Nilichofurahi ni kuwa umesoma mada yangu na kutoa angalizo lako.

Mambo mengine uliyoandika ni ramli tu kama ramli zingine!
 
There’s a saying that goes like: Once is chance, twice is coincidence, third time is pattern.

Nimeanza na angalizo hapo juu ili kuwasaidia wale ambao watadhani andiko langu ni kama ramli bila kuangalia ukweli wa historia.

Kwa wale wanaojua vizuri historia ya siasa za Tanzania lazima watatambua kuwa kila utawala mpya unaongia madarakani kwa tiketi ya TANU/CCM huhakikisha unafuta nguvu ya chama kikuu kilichokuwa cha upinzani na huibuka chama kingine kuchukua nafasi hiyo.

Mkakati huu hufanikiwa sana kwa sababu TANU/CCM ni Chama Dola na pia migogoro ya kiungozi ndani ya chama kikuu cha upinzani. Ninaposema CCM ni Chama Dola nina maana kuwa huwezi kuitenganisha CCM na ‘’Kitengo’’. Kitengo kwa lugha ya kiingereza kinaitwa Deep State. Swali labda utauliza, kwa nini huwezi kuitenganisha CCM na Kitengo (Deep State)? Jibu fupi ni kwa sababu Taifa letu limeundwa katika muundo huo.

Ifahamike kuwa chama kinakuwa ni kikuu cha upinzani kama kina wabunge na madiwani wengi. Ikumbukwe pesa za ruzuku zinategemea wingi wa Wabunge, Madiwani na kura za Urais. Huwezi kuendesha kwa mafanikio chama cha siasa nchini bila pesa za ruzuku toka serikalini.

Katika utawala wa Mwl. Nyerere mwaka 1961 kulikuwa na chama kikuu cha upinzani kulichoitwa ANC chini ya Zuberi Mtemvu lakini kufikia mwaka 1965 Rais Nyerere akawa amekifuta katika uso wa dunia.

Tuliona katika utawala wa Rais Mwinyi kulikuwa na NCCR-Mageuzi ambayo ilikuwa ni chama kikuu cha upinzani.

NCCR-Mageuzi iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya Rais Mkapa kuingia madarakani mwaka 1995 alihakikisha nguvu ya NCCR-Mageuzi kama chama kikuu cha upinzani inapotea nchini.

Kwa kudhihirisha hilo tuliona katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 NCCR-Mageuzi ikizikwa kama chama kikuu cha upinzani ambapo chama cha CUF chini ya Prof. Lipumba kiliibuka kuwa chama kikuu cha Upinzani nchini.

CUF iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini ambapo Rais Kikwete alichaguliwa kuwa Rais huku CUF ikiendelea kuwa chama kikuu cha upinzani.

Baada ya kuingia madarakani, Rais Kikwete alihakikisha nguvu ya CUF inapotea kama chama kikuu cha upinzani nchini.

Kwa kudhihirisha azma hiyo tuliona katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 CUF ikizikwa kama chama kikuu cha upinzani nchini ambapo CHADEMA kiliibuka kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi na CUF, tumeona CHADEMA ikiingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani na kutoka bado ikiwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kama historia inavyobainisha basi kifo cha CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani ni baada ya Uchaguzi Mkuu 2020.

Kwa wale wanatumia upeo mkubwa katika kuchambua na kuchanganua masuala ya kisiasa nchini watagundua kuwa dalili za CHADEMA kupotea kama chama kikuu cha upinzani nchini zimeanza kujionesha.

CHADEMA demise is a real thing, and it's happening now!

Hoja iliyoko mbele yetu kwa sasa ni chama gani kitachukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini baada ya Uchaguzi Mkuu 2020?

Ni chama gani kinaandaliwa kwa sasa ili kuchukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kama ambavyo CUF iliandaliwa kuchukua nafasi ya NCCR-Mageuzi na CHADEMA kuchukua nafasi ya CUF?

Nadhani wanaotumia 3D thinking and reasoning wamejua ni chama kipi kinaandaliwa kuchukua nafasi ya CHADEMA!
Kisije kikapasuka icho chama chako cha wajinga tuu

Keep your words usiishi kwa kukrem
 
You're such a great fool man!!!Ikifutika then?au tanzania itageuka dubai!!!Hapo Lumumba pana pepo la kunyonya akili za watu na hatimaaye kubaki km mazombie.Nimemsikiliza leo Dr KM nikawaza akili za kapeleka wapi amebaki mtupu
Kama mimi ni mjinga basi wewe ni zaidi ya mjinga.

Why waste your time reading foolish post? You must be more than blockhead!

Utamwelewaje Dr KM wakati akili zako ni zaidi ya nincompoop.

Wewe sio zaidi ya mjinga bali ni mtu ambaye hatambui ukubwa wa ujinga wake.
 
Msemakwel mi najiuliza hv kwann haya yote ya nyie kuhangaika na kuwekeza fedha na juhudi nying ktk kuua upinzani.??
Umesema vyema kuwa ssm na serkal (Dola) ni kitu kimoja na havitenganiki hii ni kwel kabsa..
Sasa kwann msiamue kufuta mfumo wa vyama vingi ibaki ssm pekee mtawale mnavyotaka
 
Back
Top Bottom