Hii ni awamu ya CHADEMA kufutika kama chama kikuu cha upinzani nchini

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,806
2,000
Kama umedurusu vizuri historia ya upinzani Tanzania huwezi kuwa dismissive kiasi hiki unless uwe kwenye denial. Tuliokuwepo kuanzia uchaguzi mkuu Wa kwanza Wa vyama vingi mwaka 1995 tunajua. Ni pattern kwa kila chama cha upinzani chenye nguvu kupotea kila awamu mpya inaposhika hatamu. Dr. Lamwai mwaka 1997 alirudi CCM kutoka NCCR Mageuzi, kina Kasanga Tumbo, Fundikira na wengine wote walirudi CCM.
Soma historia na usiwe mbishi kwa vile tu akili yako INA matamanio makubwa kwa upinzani
Mkuu;
Ninakushukuru kwa kumpa maelezo zaidi.

Kama ni mtu mwenye nia ya kujifunza atajifunza lakini nina wasiwasi ni mmoja ya wale wanatumia mihemko katika kujenga hoja zinazotaka upembuzi yakinifu.
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,094
2,000
Hizo ni ndoto za mchana kweupe. Kwa mwenye akili kama yako,ataamini hivyo,Ila ukweli ni kwamba CCM wanatengeneza CHADEMA imara kuliko wakati mwingine wowote

If you don't believe me, take my words
hizi ndoto zilikuwepo tangu enzi za mwalimu. lakini mwishowake ndio hayo...wakat mwingine tujifunze kukubali ukweli hata ukiwa mchungu
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,291
2,000
CHADEMA haiwezi kufa kwa mbinu za kijinga kama hizi. Nawaona waliobuni mbinu hii kama vile wana akili ndogo. Wanafikiria kinyumenyume. CCM wanaifanyia CHADEMA 'pruning' bila wao kujua, hivyo itachipua upya na kwa nguvu.
Fikiria mara mbili kama kweli mbinu hii inaisaidia CHADEMA au inaiangamiza kabisa.
Kwa jinsi wasiodhaniwa wanavyojiunga na CCM inasababisha kutoaminiana kati ya viongozi na wanachama wa upunzani hii tunaita Divide and Rule (divide et impera in Latin).

Haujasikia mheshimiwa flani alitaka kupigana na mwezie kisa kutuhumiana usaliti kwamba mbunge flani anataka kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wa chama cha kijani?

Haujasikia kanda ya ziwa kuna watu wamevuliwa vyeo na kufukuzwa chamani kisa wanahisiwa kusaliti chama kwa kutaka kujiunga chama kingine?

Kifupi CHADEMA wameshaingia mkenge wanaanza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe huku adui akifurahia. Leo kwenye vikao vyao vya ndani vya madiwani, wabunge na viongozi wa CHADEMA na hata vyama vingine vya upinzani hawaaminiani tena sababu hawajui nani anahama kesho na atapeleka mikakati ya siri kwa mpinzani wao.
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
37,143
2,000

NCCR-Mageuzi imekuwepo tokea kwenye utawala wa awamu ya Rais Mwinyi.CUF iliendelea kuwa chama kikuu cha upinzani hata baada ya uchaguzi wa mwaka 2005.

CHADEMA haikuwa kuwa chama kikuu cha upinzani mwaka 2005. Nimekuambia baada ya Uchaguzi mkuu mwaka 2005, CUF iliendelea kuwa chama kikuu cha upinzani.Wewe ndiye unafikiria masuala ambayo sikuweka kwenye mada yangu.

Kazeni buti kuongeza madau makubwa makubwa mnaweza kufanikiwa...
[/QUOTE]NCCR-Mageuzi iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini..

Nimekunukuu hapo juu.

Ili chama kiwe kikuu cha Upinzani ni lazima kiwe na Madiwani na Wabunge wengi, ambapo wanapatikana baada ya uchaguzi mkuu.

Kwa mara ya kwanza uchaguzi mkuu chini ya vyama vingi ulianza 1995, sasa hapo utasema vipi NCCR-Mageuzi ilikuwa chama kikuu cha Upinzani?

Tuzungumzie baada ya uchaguzi ambapo ndio kilianza kuwa chama kikuu cha upinzani, hapo ndio ilipo hoja yangu.

Ebu usizungumzie kipindi ambapo bado kilikuwa hakijaanza kushiriki uchaguzi ambapo ni kabla ya 1995(enzi za Mwinyi)
 
Kuntakint

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,770
2,000
There’s a saying that goes like: Once is chance, twice is coincidence, third time is pattern.

Nimeanza na angalizo hapo juu ili kuwasaidia wale ambao watadhani andiko langu ni kama ramli bila kuangalia ukweli wa historia.

Kwa wale wanaojua vizuri historia ya siasa za Tanzania lazima watatambua kuwa kila utawala mpya unaongia madarakani kwa tiketi ya TANU/CCM huhakikisha unafuta nguvu ya chama kikuu kilichokuwa cha upinzani na huibuka chama kingine kuchukua nafasi hiyo.

Mkakati huu hufanikiwa sana kwa sababu TANU/CCM ni Chama Dola na pia migogoro ya kiungozi ndani ya chama kikuu cha upinzani. Ninaposema CCM ni Chama Dola nina maana kuwa huwezi kuitenganisha CCM na ‘’Kitengo’’. Kitengo kwa lugha ya kiingereza kinaitwa Deep State. Swali labda utauliza, kwa nini huwezi kuitenganisha CCM na Kitengo (Deep State)? Jibu fupi ni kwa sababu Taifa letu limeundwa katika muundo huo.

Ifahamike kuwa chama kinakuwa ni kikuu cha upinzani kama kina wabunge na madiwani wengi. Ikumbukwe pesa za ruzuku zinategemea wingi wa Wabunge, Madiwani na kura za Urais. Huwezi kuendesha kwa mafanikio chama cha siasa nchini bila pesa za ruzuku toka serikalini.

Katika utawala wa Mwl. Nyerere mwaka 1961 kulikuwa na chama kikuu cha upinzani kulichoitwa ANC chini ya Zuberi Mtemvu lakini kufikia mwaka 1965 Rais Nyerere akawa amekifuta katika uso wa dunia.

Tuliona katika utawala wa Rais Mwinyi kulikuwa na NCCR-Mageuzi ambayo ilikuwa ni chama kikuu cha upinzani.

NCCR-Mageuzi iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya Rais Mkapa kuingia madarakani mwaka 1995 alihakikisha nguvu ya NCCR-Mageuzi kama chama kikuu cha upinzani inapotea nchini.

Kwa kudhihirisha hilo tuliona katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 NCCR-Mageuzi ikizikwa kama chama kikuu cha upinzani ambapo chama cha CUF chini ya Prof. Lipumba kiliibuka kuwa chama kikuu cha Upinzani nchini.

CUF iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini ambapo Rais Kikwete alichaguliwa kuwa Rais huku CUF ikiendelea kuwa chama kikuu cha upinzani.

Baada ya kuingia madarakani, Rais Kikwete alihakikisha nguvu ya CUF inapotea kama chama kikuu cha upinzani nchini.

Kwa kudhihirisha azma hiyo tuliona katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 CUF ikizikwa kama chama kikuu cha upinzani nchini ambapo CHADEMA kiliibuka kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi na CUF, tumeona CHADEMA ikiingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani na kutoka bado ikiwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kama historia inavyobainisha basi kifo cha CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani ni baada ya Uchaguzi Mkuu 2020.

Kwa wale wanatumia upeo mkubwa katika kuchambua na kuchanganua masuala ya kisiasa nchini watagundua kuwa dalili za CHADEMA kupotea kama chama kikuu cha upinzani nchini zimeanza kujionesha.

CHADEMA demise is a real thing, and it's happening now!

Hoja iliyoko mbele yetu kwa sasa ni chama gani kitachukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini baada ya Uchaguzi Mkuu 2020?

Ni chama gani kinaandaliwa kwa sasa ili kuchukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kama ambavyo CUF iliandaliwa kuchukua nafasi ya NCCR-Mageuzi na CHADEMA kuchukua nafasi ya CUF?

Nadhani wanaotumia 3D thinking and reasoning wamejua ni chama kipi kinaandaliwa kuchukua nafasi ya CHADEMA!
Sometime uwa ckuelewi unaandika nn. Unauliza chama gani kinategemewa kuchukua nafasi ya chadema. Je umejiuliza kwanini chadema inakufa?? Na Kama chadema inakufa umejiuliza Tena inakufa kwasababu zipi. Unategemea chadema ikifa Kuna chama itakuja kwass mbadala. Muda mwingine Kama huna cha kuandika Bora ukae kimya
 
Inkubu

JF-Expert Member
Jul 6, 2016
489
500
Wana Lumumba mbona mnaweweseka,

Mnatumia nguvu nyingi sana kuaminisha watu upuuzi wenu.

Chama cha mumiani kutegemea dola kushinda chaguzi, na kujiaminisha eti mnaua upinzani ni mawazo hasi.

Kwa taarifa yako Chadema ipo na itaendelea kuwa chama kikuu cha upinzani,

Na inazidi kuimarika kuliko wakati mwingine wowote ule.

Kuendelea kujinasibu eti chama dola na mbinu za kuua upinzani bila kufikiri nyakati tulizopo naweza sema ni dalili za kuishiwa hoja.

Huwezi tegemea NEC na FFU alafu ukasema chaguzi zilikuwa huru na haki.

Acheni Sanduku la Kura liamue mshindi.
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,806
2,000
Ungekuwa unajua maana ya upinzani usingeandika hili gazeti lako. Upinzani siyo kikundi cha watu, upinzani siyo CHADEMA,CUF au ACT- Wazalendo, upinzani ni mawazo ,upinzani ni fikra,upinzani ni utashi. Nataka nikuambie leo unaweza kuua mtu lakini huwezi kuua mawazo na fikra. Hii maana yake nini CHADEMA na CUF vinaweza kufa lakini fikra na mawazo hayawezi kufa. Upinzani ni maisha ya mwanadamu.Kila sehemu kuna upinzani ,kwenye familia kuna upinzani ,ndani ya CHADEMA kuna upinzani ,CCM pia kuna upinzani.
Mkuu;
Hakuna sehemu nimesema CHADEMA kitakufa lakini pia hakuna sehemu nimesema CHADEMA kikifa na upinzani utakufa.

Ndio maana katika hoja yangu nimesema baada ya kudhoofika NCCR-Mageuzi na kupoteza sifa ya kuwa chama kikuu cha upinzani, CUF kiliibuka na kuchukua nafasi ya NCCR-Mageuzi.

Hata baada ya CUF kudhoofika, CHADEMA kiliibuka na kuchukua nafasi ya CUF.

Vivyo hivyo CHADEMA kikidhoofika, lazima kuna chama kingine kitachukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini.

Hii ina maana kuwa upinzani hauwezi kufa bali utaendelea kuwepo kwa sababu ni taasisi ndani ya fikra ambazo zinaunganishwa na chama cha siasa.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,650
2,000
Mkuu;
Hakuna anayesema CHADEMA itakufa. Ninachosema CHADEMA itadhoofika.

Tatizo ambalo ninadhani linakusumbua ni kudhani kuwa CHADEMA ni kama Baba na Mama kuwa huwezi kuachana naye au kumkataa.

Historia inaonyesha hata NCCR-Mageuzi ilikuwa na wafuasi kama ilivyo CHADEMA lakini hao hao wafuasi waliondoka na kuwa wafuasi wa CUF.

Hao hao wafuasi wa CUF waliondoka na kuwa wafuasi wa CHADEMA. Hoja yangu ni kuwa usidhani hawa wafuasi wa CHADEMA wataendelea kuwepo kama kesho tutaamka na kujikuta CHADEMA sio chama kikuu cha upinzani nchini.

Mimi si mwanachama wa cdm bali ni shabiki wa kutupwa wa cdm. Hivyo sio wa kuondoka maana sio mwanachama. Lengo la huu uzi wako na wengine wa aina yako ni kucheck kama hao washabiki wa cdm wako tayari kuhama. Ila ujue sasa hv hata kikipandikizwa chama kipya na hicho kitengo itabidi kijipange sana maana ufahamu nao sio mdogo hivyo. Nadhani Zitto anaitambua hali hiyo. Pamoja na kujitahidi kusogea karibu na cdm na kujaribu kucheza midundo ya cdm anaambiwa kabisa haaminiki. Hapo sasa ndio mziki ulipo.
 
successor

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
3,085
2,000
Fikiria mara mbili kama kweli mbinu hii inaisaidia CHADEMA au inaiangamiza kabisa.
Kwa jinsi wasiodhaniwa wanavyojiunga na CCM inasababisha kutoaminiana kati ya viongozi na wanachama wa upunzani hii tunaita Divide and Rule (divide et impera in Latin).

Haujasikia mheshimiwa flani alitaka kupigana na mwezie kisa kutuhumiana usaliti kwamba mbunge flani anataka kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wa chama cha kijani?

Haujasikia kanda ya ziwa kuna watu wamevuliwa vyeo na kufukuzwa chamani kisa wanahisiwa kusaliti chama kwa kutaka kujiunga chama kingine?

Kifupi CHADEMA wameshaingia mkenge wanaanza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe huku adui akifurahia. Leo kwenye vikao vyao vya ndani vya madiwani, wabunge na viongozi wa CHADEMA na hata vyama vingine vya upinzani hawaaminiani tena sababu hawajui nani anahama kesho na atapeleka mikakati ya siri kwa mpinzani wao.
Muda utaongea chief.
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,916
2,000
Mkuu;
Mimi nimejenga hoja ya kihistoria lakini wewe ulichofanya ni kujenga hoja kwa hisia zako.

Kwa hizi hisia zako hata NCCR-Mageuzi na CUF walisema kile ulichokiandika lakini leo sio vyama vikuu vya upinzani nchini!
historia ya KANU siyo historia ya CCM, hitoria ya UPC siyo historia ya CCM, eti kwa kuwa KANU na UPC ambavyo ni vyama viasisi katika nchi zao vimekufa/ kudhofika basi na CCM ambayo ni chama mwasisi wa nchi yetu kupitia TANU na TAA (siyo taa ya chemli)nayo itadhofika/itakufa.

Hali inayoikumba CHADEMA hata CCM huwa inapitia kwa njia moja au nyingine mpaka akina Nape wanalazimika kutumbukia shimoni kuiokoa CCM.

Nahata hili la kuvifunga mikono vyama vya siasa pinzani,kuzuiliwa kufanya mikutano ya kisiasa kwa uhuru wakati viongozi wa CCM wanazunguka nchi nzima kufanya mikutano,na hamahama ya wapinzani kuhamia CCM kwa hiyari/kununuliwa ni mpango maalumu wa kuiokoa ccm/kuimarisha ccm,na kuua upinzani ambao hawatafanikiwa kuua kwa kuwa wanachokifanya ni kama wanafunika moto na majivu halafu wanaamini kuwa wanazima moto.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,650
2,000
Una maana gani unaposema hakuna idadi ya wapiga kura?

Nimesema Chama chochote makini cha siasa ni kushika dola. Ndio maana huwezi kukuta eti sheria inasema ili uchaguzi ufanyike ni lazima pawepo na idadi fulani ya wapiga kura.

Mkuu pole kwa kutaja sheria kam kigezo cha kupata madaraka. Iwapo sasa hivi hizo sheria za kupata kiongozi zinakiukwa wawaziwazi unawezaje kutaja sheria kama kigezo cha kupata madaraka? Huenda ukaamini jeshi litakuwa upande wa ccm, hilo jeshi lililojaa vijana sio la kuamini sana kwa kuongozwa na chama kizee. Hao wanajeshi tuko nao mtaani na wala hawako upande huo labda viongozi wao wachache ambao ni wazee.

Kwa taarifa yako ccm imefikia mwisho wa ushawishi na hiki kitendo cha kupora kura kimachomacho stay tuned hutoamini. Hizo sheria mmeamua kutoziheshimu ambazo watu ndio walikuwa wanazionea aibu basi mtafurahi. Watu watatumia mtindo huohuo wa kutoheshimu sheria kuchukua madaraka. Watu wanaona na wanawachora tu. Ww lete historia za nani alikuw vip mwaka 95 sijui 2000, zama zimebadilika boss.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,004
2,000
Kuna vitu vingi hujui, usijifanye mjuaji sana.

Hakuna anaejua vitu vyote, lakini katika hili sioni wewe unapointi gani zaidi ya kutoa maneno yasiyo muelimisha yeyote hapa JF. Kosoa nilicho andika tuendelee na mada.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,004
2,000
Hata Mbinu aliyotumia Mwl. Nyerere kukifuta chama cha ANC ni tofauti na mbinu aliyotumia Mkapa kuidhoofisha NCCR-Mageuzi, Hata Kikwete alitumia mbinu tofauti kuidhoofisha CUF.

Vivyo hivyo hata Magufuli atatumia mbinu nyingine ili kuidhoofisha CHADEMA
Ni kweli wanatumia mbinu "tofauti" kudhoofisha au kutaka kuua vyama vya upinzani lakini wote kinacho wapa kiburi ni UCHAMADOLA na likatiba libovu. Na ukichunguza sana ni uchu wa madaraka-lazima tushinde sisi, na hapo ndo CHAMADOLA kinapotumika. Mfano mnyime ruzuku Maalim, mpa Ruzuku Lipumba. Mpe Lipumba ulinzi, mnyime Maalim ulinzi. Hakuna mikutano ya hadhara, lakini wewe kila leo una mikutano inayo rushwa na TBC etc, na ndani yake unapiga siasa.
 
thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,206
2,000
There’s a saying that goes like: Once is chance, twice is coincidence, third time is pattern.

Nimeanza na angalizo hapo juu ili kuwasaidia wale ambao watadhani andiko langu ni kama ramli bila kuangalia ukweli wa historia.

Kwa wale wanaojua vizuri historia ya siasa za Tanzania lazima watatambua kuwa kila utawala mpya unaongia madarakani kwa tiketi ya TANU/CCM huhakikisha unafuta nguvu ya chama kikuu kilichokuwa cha upinzani na huibuka chama kingine kuchukua nafasi hiyo.

Mkakati huu hufanikiwa sana kwa sababu TANU/CCM ni Chama Dola na pia migogoro ya kiungozi ndani ya chama kikuu cha upinzani. Ninaposema CCM ni Chama Dola nina maana kuwa huwezi kuitenganisha CCM na ‘’Kitengo’’. Kitengo kwa lugha ya kiingereza kinaitwa Deep State. Swali labda utauliza, kwa nini huwezi kuitenganisha CCM na Kitengo (Deep State)? Jibu fupi ni kwa sababu Taifa letu limeundwa katika muundo huo.

Ifahamike kuwa chama kinakuwa ni kikuu cha upinzani kama kina wabunge na madiwani wengi. Ikumbukwe pesa za ruzuku zinategemea wingi wa Wabunge, Madiwani na kura za Urais. Huwezi kuendesha kwa mafanikio chama cha siasa nchini bila pesa za ruzuku toka serikalini.

Katika utawala wa Mwl. Nyerere mwaka 1961 kulikuwa na chama kikuu cha upinzani kulichoitwa ANC chini ya Zuberi Mtemvu lakini kufikia mwaka 1965 Rais Nyerere akawa amekifuta katika uso wa dunia.

Tuliona katika utawala wa Rais Mwinyi kulikuwa na NCCR-Mageuzi ambayo ilikuwa ni chama kikuu cha upinzani.

NCCR-Mageuzi iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya Rais Mkapa kuingia madarakani mwaka 1995 alihakikisha nguvu ya NCCR-Mageuzi kama chama kikuu cha upinzani inapotea nchini.

Kwa kudhihirisha hilo tuliona katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000 NCCR-Mageuzi ikizikwa kama chama kikuu cha upinzani ambapo chama cha CUF chini ya Prof. Lipumba kiliibuka kuwa chama kikuu cha Upinzani nchini.

CUF iliingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani nchini ambapo Rais Kikwete alichaguliwa kuwa Rais huku CUF ikiendelea kuwa chama kikuu cha upinzani.

Baada ya kuingia madarakani, Rais Kikwete alihakikisha nguvu ya CUF inapotea kama chama kikuu cha upinzani nchini.

Kwa kudhihirisha azma hiyo tuliona katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 CUF ikizikwa kama chama kikuu cha upinzani nchini ambapo CHADEMA kiliibuka kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi na CUF, tumeona CHADEMA ikiingia kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ikiwa ni chama kikuu cha upinzani na kutoka bado ikiwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Kama historia inavyobainisha basi kifo cha CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani ni baada ya Uchaguzi Mkuu 2020.

Kwa wale wanatumia upeo mkubwa katika kuchambua na kuchanganua masuala ya kisiasa nchini watagundua kuwa dalili za CHADEMA kupotea kama chama kikuu cha upinzani nchini zimeanza kujionesha.

CHADEMA demise is a real thing, and it's happening now!

Hoja iliyoko mbele yetu kwa sasa ni chama gani kitachukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini baada ya Uchaguzi Mkuu 2020?

Ni chama gani kinaandaliwa kwa sasa ili kuchukua nafasi ya CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kama ambavyo CUF iliandaliwa kuchukua nafasi ya NCCR-Mageuzi na CHADEMA kuchukua nafasi ya CUF?

Nadhani wanaotumia 3D thinking and reasoning wamejua ni chama kipi kinaandaliwa kuchukua nafasi ya CHADEMA!
Hili genge lifutike tu, hakuna namna nyingine ya hili genge kusavaivu
 
bernardp

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
619
1,000
Mapendekezo ya silaha nne zinazopaswa kumilikiwa na kila chama makini cha siasa

Chama cha siasa chenye nia ya kushika dola inakipasa kiwe na silaha za maangamizi zinazoweza ku-guarantee perpetual existence. Silaha hizi zapaswa zionekane na kila adui anayetamani kukidhuru chama. Silaha hizi zikiwa imara, zitawatisha maadui wa ndani na kuwaogofya maadui wa nje wasije wakajaribu kukiingilia chama kwa mbinu dhaifu. Na endapo atajaribu mtu au kikundi inapaswa chama kiwe na uwezo wa kujibu mashambuizi kwa kiwango cha kuogofya.

Silaha hizi zinapaswa ziwe active wakati wote wa uendeshaji wa chama na pale inapobainika kuna hatari kubwa kwa chama, hizi silaha zitakuwa msaada mkubwa sana kukiokoa chama katika mawimbi.

Silaha ya kwanza ni itikadi. Itikadi yapaswa kuwa clear sana. Isiwe rahisi kuonekana kama chama kingine tu cha siasa (Just another political party). Mfano - "Chama kinaamini katika sera za ubepari na masoko huru" au "Chama kinaamini katika ujamaa/ukomunisti" nk. itakuwa lazima kwa viongozi wa juu kupata mafunzo maalum ya itikadi kwa kushirikiana na marafiki wa kimataifa wenye mrengo unaofanana. Viongozi wote wa juu na wanaoibukia ni lazima wajengwe na chama. Wanaohamia wanapokelewa na kuwekwa kimkakati katika chama mpaka watakapochunguzwa na kukamilisha hatua muafaka ndipo wataweza kupanda ngazi na kufanana na wanaojengwa na chama.

Silaha ya pili ni makada walioiva kiitikadi waliojengwa na chama kuanzia chini. Hapa sidhani kama kuna haja ya maelezo marefu sana kwa kuwa itikadi haiwezi kuwepo bila watu wanaoishi hiyo itikadi.

Silaha ya tatu ni intelijensia za wazi na za siri. Intelijensia ni lazima iwepo kwa ajili ya kukiokoa chama kitakapokuwa kimekumbwa na balaa la aina yoyote. Intelijensia inaweza kuwa katika mfumo wa mkakati (strategy organ) na inatakiwa iwepo ya ndani na ya nje pia. Lazima kitengo hiki kiwe na uwezo wa kijasusi na kiweze kuchunguza nyendo za competitors na pia kiweze kutambua mapungufu ya ndani na kuyatengenezea mikakati imara.

Silaha ya nne ni ulinzi. Kila kitu duniani kinapaswa kulindwa. Atakayedhamiria kukiangamiza lazima atambue kuwa atatafutwa tu kwa namna yoyote. Ulinzi ni jambo la kawaida sana ila lapaswa kupewa uzito mkubwa unaostahili. Hakuna survival ya kiumbe chochote bila ulinzi. Mungu ameumbia kila kiumbe ulinzi wa kukabiliana na mazingira. Hivyo ni muhimu sana chama kuwa na ngome imara za ulinzi wa nje na ndani pia. Siri na mali ya chama lazima vilindwe dhidi ya wabaadhirifu. Pia uhai wa chama lazima ulindwe kwa gharama zozote dhidi ya mahasimu wa nje. Yeyote aliyepo kwenye party structure inampasa aheshimu taratibu maana ataijua nguvu inayoweza kumwangukia endapo atajaribu kukengeuka.
 
monongo

JF-Expert Member
Oct 25, 2011
388
225
Mimi sishangai kwa yote yanayofanyika katika siasa za hapa kwetu, maana toka mwanzo mkuu alishasema kuwa ole wake kiongozi yeyote atakaye tangaza kuwa mshindi ni WA upinzani,atakuwa amejifuta kazi. Hata kama ningekuwa Mimi nisingechafua kitumbua changu
 
Omerta

JF-Expert Member
Jan 3, 2016
4,345
2,000
CCM imepoteza mvuto ipo katika hatua za mwisho kujinusuru na kaburi lake
 
shungurui

JF-Expert Member
Sep 1, 2008
3,699
2,000
Najua unandika haya kwa sababu unalipwa ila hata wewe mwenyewe unajua kabisa hicho mnachokifanya hakitafanikiwa, nyie mdanganyeni jiwe ili mle kodi za wananchi maana anandoto za kutawala milele
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,806
2,000
Akili za Lumumba hizi... Hayo yote ya kuua upinzani ni kwa faida ya nani hasa?
Halijalishi ni akili za Lumumba au Ufipa, kinachoangaliwa ni hoja kutoka kwenye hiyo akili.

Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa CHADEMA imeundwa ili iwe msindikizaji au UDP imeundwa ili iwe kama ilivyo?

Vyama vya upinzani vitawezaje kupata madaraka/dola bila kuodhoofisha CCM?

Kama vyama vya upinzani vinafanya jitihada za kuidhoofisha CCM ili vipate dola kwa nini CCM isifanye jitihada za kukidhoofisha chama ambacho inaamini ndio hatari zaidi katika maisha yake?

Hoja ya kusema kwa faida ya nani, umeishajiuliza kwa nini vyama vya upinzani vinataka kuidhoofisha CCM? Kwa fikra zako zinataka kuidhoofisha CCM kwa faida ya nani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom