Hii ni awamu kabambe sana, taratibu tutafika uvumilivu na uzalendo unahitajika

monomotapa

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
437
325
Awamu hii ukitingisha kiberiti cha kiutapeli tu umedakwa, kama mtu unajijua una asili ya wizi afadhari ufanye kazi nyingine ujiibie mwenyewe ili uone uchungu wa wizi
Ushauri wangu kwa Uongozi wa sasa "Kuandaa warithi wenye misimamo kabambe isiyotikisika na wenye kuangalia maslahi ya nchi kama ajenda namba moja, na uwajibikaji na kupiga vita rushwa kama safu hii ya juu ya Mheshimiwa Rais Magufuri" Ili siku za usoni kuwe na mwendelezo mzuri wa maadili katika Nchi hii. (Proper definition of the Nation) Mambo ya kubahatisha kupata viongozi ndo yaliyotufikisha hapa tulipo.
Mungu akubariki sana sana Rais wetu na akulinde na kukupa nguvu zaidi
Mafisadi na wote waliosababisha tuwe kwenye umasikini huu walaaniwe. Ama kweli mwizi hana alama sikutegemea wasomi waliopewa dhamana wanaweza kututapeli kiasi hiki.
Ni kazi ngumu lakini mambo mazuri huwa yana maumivu yake na yanahitaji muda.
Tuvumilie na kumsaidia Mheshimiwa Rais wetu na safu yake nzuri ana nia ya dhati na njema sana kwa nchi yetu Tanzania .. Mungu ibariki Tanzania
 
Rais kama nia njema anayo, PhD zote zile kutoa report mbovu mara mbili sidhani. Watu wa academics hua nawaheshimu sana maana najua process inavyokwenda hadi kutoa conclusion hua inafanyiwa very careful analysis.

Kupigwa kekundu kweli tulikua tunapigwa vizuri na ni aibu watu wanafanya kazi miaka yote hawakujali kabisa, uzalendo ni zero maana kuna chance kubwa walikua wanahongwa wanatulia.

Tatizo ni Bashite tu, anamuangusha sana mzee na skendo zake.
 
Back
Top Bottom