Hii ni aibu kubwa sana kwa Harmonize

IMG_20210916_164017.jpg
 
Na mimi nimeona nimesikitika sana ila ukiwa mwenye nyumba ndo unaweza kuelewa kwanini watu tumeamua nyumba zibaki magofu bila watu. Kadhia niliyoipata kupangisha nyumba Dodoma ilinifanya heri nibaki maskini jeuri kuliko kuwa na wapangaji.

Mpangaji wakati anatoka anakuibia vitanda, magodoro na bado anakutukana mpaka matusi ya nguoni. Heri nibaki na nyumba bila mpangaji kuliko mateso kama ya huyo wa Harmoniser.
Niko dodoma hapa nimepanga uswahilini mkuu. Kuliko nyumba iote vichugu si nikakae hapo ata nifekee fekee nyasi
 
Yani na usanii wote huo asiwe na nyumba hata ya 50M,huo ni uong
Hana nyumba. Alianza kujenga sijui Madale sijui wapi.. ila hakumaliza na mlinzi hajalipwa mshahara miezi 7.

From..
Harmonize Adaiwa Mshahara

Jamani hawa watoto kwa kujikweza hawajambo, Harmonize nyumba yake ya Madale ndiyo hii hapa mnayoiyona.

“Ninavyojua hana nyumba nyingine zaidi ya hii, lakini nina uhakika angekuwa na nyingine ningejua kwa sababu nipo karibu sana na mama yake,” anasema jamaa huyo.

Alipoulizwa juu ya madai yake ya kutolipwa kwa miezi saba, jamaa huyo alifunguka na kukiri kwamba, ni kweli ana miezi saba bila kulipwa mshahara wake wa kulinda na kutunza eneo hilo kama makubaliano ya awali yalivyokuwa.

“Aliyewaambia hajakosea hata kidogo, ni kweli hapa nilipo nina muda wa miezi saba sijalipwa pesa yangu na bado ninalinda.

“Ikumbukwe pia na mimi nina familia na watoto wanatakiwa kwenda shuleni na kulia kodi ya pango.

“Harmonize hana habari na mimi kabisa. Ukimwaambia anakujibu kuwa sijakutafuta mimi ulitafutwa na mama, kama una shida mwambie mama yeye ndiye ataniambia mimi eti kwa sababu mama yake ndiye anasimamia ujenzi.

“Kuna kipindi nilipatwa na msiba wa mwanangu wa kumzaa kabisa, nilimpa taarifa Harmonize juu ya suala hilo, lakini huwezi kuamini, Harmonize alinitumia shilingi elfu thelathini tu,” alilalama shamba boy huyo akiomba taarifa zimfikie Harmo kwani anateseka na maisha magumu.

Ili kujua ukweli juu ya jambo hilo, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta mama mzazi wa Harmonize ambaye inasemekana ndiye msimamizi wa nyumba hiyo ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili mwanawe ambapo alisema kuwa, hawezi kuzungumza kitu chochote juu yake na hata kwa mtoto wake.

“Siwezi kumzungumza kitu chochote kinachomuhusu mwanangu na hata mimi mwenyewe, mimi siyo mtu wa mambo hayo hata kidogo, ndiyo maana ninaweza kupanda daladala na wala mtu asijue kama mimi ni mama wa Harmonize,” alisema mama huyo kisha akakata simu.
 
Back
Top Bottom