Hii ni Aibu Chuo kikuu Tanzania na masomo ya Introduction to Computer? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ni Aibu Chuo kikuu Tanzania na masomo ya Introduction to Computer?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Rutunga M, May 26, 2011.

 1. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nashindwa kuelewa mstakabali wa elimu ya bongo na mapokeo ya ICT
  Nimejuzwa na ipo katika matangazo ya Chuo kikuu huria cha tanzania kwamba kinatoa mafunzo ya awali ya computer kwamba wahitomu watapata vyeti.
  Masomo wanayotoa ni Introduction to Computer,Ms Word nk

  Swali hivi kama haya yanafundishwa na chuo kikuu je kule chekechea wanafundishwa nini?

  Nimesikitika sana!

  labda nimeelewa vinginevyo
   
 2. mirindimo

  mirindimo JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 60

  Hapana si aibu hata kidogo tena wanasaidia sana kuna watu wanafika chuo hata kushika mose kwao ni shida,dont look at yourself na ukajilinganisha na mtu mwingine!! Pia hata kama unachukua masomo ya postgraduate kuna vyuo kupata access ya computer pia ni shida,computer labs ziko kama majina tu,na ukienda stationary utakuta kuna kazi kibao watu wameleka wafanyiwe zikiwemo assignment etc
   
 3. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Sasa tatizo ni nani? Mbona wanaofundishwa hapo wapo waliomaliza drs la 7
   
 4. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani ni tatizo, tena kubwa ambalo vyuo vikuu vimeona ni nafasi /opportunity ya kujipatia miradi ( kupata hela ya vitafunio) kwa kutumia umaarufu wa majina ya vyuo husika, kwani asilimia kubwa ya wabongo hawajui kutumia computer na siku hizi watu wanaoishi mijini wanaanza kuona umuhimu wakujua matumizi yake.

  We have a long way to go, kwani bado tunajiita tuko kwenye 21st century wakati tunajikita kwenye introduction badala ya kufanya research ambazo zitasaidia kutengeneza computer za kwetu zinazoendana na mazingira yetu ya kibongo. Tunaagiza computer kila siku, lakini hatutaki kuzuia Silcon na Nickel za kabanga (Ngara) zinazotengeneza vifaa vya computer ( wajanja wanaziiba kila siku tena bila kulipa kodi), ngoja labda hizo intoduction to computer ndo mpinduzi ya kisayansi na Technolojia, lakini nachelea kusema "WE ARE IN A WRONG DIRECTION" na bahati mbaya wenzetu wanakimbia siye ndo tunavuta shuka kitandani.

  Bahati mbaya zaidi, tunapigizana kelele na shule za kata, walimu hakuna, vitabu hakuna kila mwaka wakati tunajua tatizo na solutions bado tunajishauri kuchukua hatua haraka.

  Maoni:
  Serikali + Wadau + watalaam wa kila nyanja, tujitoleeni kuhudhuria kwenye makongamano/mikutano tutoe maoni ikibidi tusichoke kuwa wabunifu ili tusaidie nchi yetu jamani. Vyuo vya computer vinatakiwa viwepo kila kata na vyuo vikuu viache tamaa ya hela vifundishe watu namna ya "critically thinking, analysing and researching for result oriented"
   
 5. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Huna cha kushangaa watanzania wanaojua kutumia computer hawazidi milioni 5 kati 46mil.
   
 6. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Waulize hao wenye degree ya computer hizo introduction to word au Excel?
   
 7. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  sijui ndiyo walimu?
  Tanzania tuna safari ndefu katika mambo ya elimu
   
 8. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Usishangae ni kawaida, Vyuo vikuu wanasoma watu wa aina zote.

  Kuanzia watu wenye elimu ya chini hadi ya juu.

  Ndo maana ya kuwa na kozi muda mfupi, muda mrefu na kozi maalum ambayo mtu au kikundi cha watu wanaweza kuomba wenyewe wafundishwe elimu fulani.

  Hata wewe ukihitaji ujuzi fulani unaangalia chuo kipi unaweza kupatikana huo ujuzi unapeleka maombi. Ili mradi uwe na mshiko wa kutosha kulipia gharama za mafunzo.
   
 9. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hujui kwamba watu wanagraduate vyuo vikuu na certificates, diploma, degree, nk? Likiwepo pengo la kielimu mahali ni halali chuo kikuu kuliziba bila kujali level.
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hakuna aibu yeyote katika hilo. wala usisikite ni kwamba huelewi tu....

  Kwanza elewa maudhui ya chuo kikuuu huria. Kuna wafungwa Pia wanasoma pale Kama unajiuliza kusuhusu watoto wa primary sasa sijui kwa wafungwa ndo utashangaaa au utasikitika.

  Pili
  wanaofundisha hizo introduction to computer sio lecturer wale wanafundisha nondo hasa za comuter.

  Tatu kama wana facilities na resouces ambazo hazitumiki efectively ni wajibu wao waazitumie hata kama ni kuwafundsha watu intoduction to use the internet. Kuliko lab kukaaa bila kutumika muda mrefu. kwa nini wasisaidie kuongeza maarifa kwenye jamiii. ???

  Nne ni kozi za muda mfupi ama wiki watu an nne ambazo mahitaji ya watu wanafundishwa hata mtoto wa darsa la tano anaruhusiwa.


  NB
  Sio tu Chuo Kikuu Huria hata vyuo kama UDSM wenye vitovo mbali mbali wanafundisha cousrse ndogo ndolo kwa ajiliya wa wanafuzi wa pimary, secondary na hata wazee amabo wanaenda kujifunza. Unaweza kukuta kitivo cha Biashara wana course ya Introduction TO excel.

  So kwangu there is nothing wrong ni njia kuongeza maarifa na ujuzi kwenye jamiii. Tena Binafsi ningepnda kusikia wanatoa ofa maalum za bei nafuu zaidi au hata bure kwa watoto wa darasa la saba wa kata waliyopo.
   
 11. Given Edward

  Given Edward Verified User

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 862
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi kuna taasisi/chuo/kampuni inayodeal na kukuza vipaji vya teens ambao wanajihusisha na IT e.g programing, graphics, animation, e.t.c?
   
 12. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,060
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  I just stole your idea, I'm gonna start company to help teens in that area
   
 13. K

  KyelaBoy JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2008
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Matumizi ya computer kwa Tanzania ni kuandika na kusoma email,blogs n.k ni sawa na mtu mwenye roli la tani 10 anafanyia kazi ya kubeba mkungu mmoja wa ndizi au anabeba gunia moja la mkaa kila siku kwa ajili ya kujiletea maendeleo
   
 14. mazd

  mazd Senior Member

  #14
  May 27, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  i think we have alread tolk about this, and i will anounce it official along my animation movie
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Ni makosa kufikiri kwamba introduction to Computing ni somo lisilofaa kufundishwa chuo kikuu. Nafikiri ni umasikini wetu tu unaotufanya tupaone chuo kikuu kama sehemu fulani ya ajabu. Nakubali inawezekana ukatakiwa kuwa na basic computing knowledge ku enroll katika a computer science program - and even that is not necessary- lakini vipi kama mimi nimekuja kusoma sociology na sihitaji kujua computing zaidi ya the basics?

  Wewe ulitaka wafundishe nini? Computer Programming na Artificial Intelligence ?

  Kuna watu wengi tu ambao taaluma zao hazihitaji kujua computer zaidi ya level hiyo ya introduction, na wako chuo kikuu kusoma mambo mengine. Kwa kuchukua kozi hii itawasaidia kujua computer kwa level wanayoihitaji tu, na si zaidi.

  Zaidi ya hapo, vyuo vikuu kibao nchi zilizoendelea vinatoa certificates za introductory computing, as a matter of fact nilikuwa namsaidia mzee mmoja mstaafu, yeye hataki kujua mambo mengi sana ya computer, anataka kujua kutumia internet vizuri tu ili ku research mambo ya afya yake na dawa anazotumia. Kaenda chuo kikuu cha karibu, kajisajili katika evening classes, kahitimu course hizo hizo za introduction to computing, zinamfaa.

  Tatizo letu hatuangalii elimu kama a practical tool to help us in life, tunaangalia elimu kama some abstract glorified credential held at the top of unrealistic ivory towers, not to be tarnished by the actual needs of everyday people.

  Ndiyo maana mpaka leo vyuo vikuu vyetu havijai kibaba, tunaona chuo kikuu ni sehemu moja ya ajaaabu.
   
 16. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana maendeleo kwa watanzania ni tatizo. Hivi wewe unaona aibu chuku kikkuu kufundisha introduction wakati wateja wako wengi kuliko wanaojua? Ni fikra potofu kujiangalia wewe kama wewe angali ana wengine. Umeona lile tangazo la HAKI ELIMU? Naomba likusaidie na kusahihisha thread yako;
   
 17. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  sijaona cha ajabu kwa elimu ya bongo ilivyo.
   
 18. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ajabu itoke wapi kakayangu wakati vijijini hakuna wanaojua computer. Tangazo la hakielemu linaonyesha uhalisia wa nchi hii. Usishangae kesho tukaanza kufundishwa hata aeiou.
   
 19. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  We ulitakaje mwehu nini
   
 20. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2011
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbona hata vyuo vikuu vya nchi zilizoendelea vinafundisha Intro to Comp? Madarasa yake wanayaita 100 level.
   
Loading...