Hii ndoto lini itatimia?

fundiaminy

JF-Expert Member
Jun 4, 2009
355
51
katika gate ya ikulu mzee mmoja alikuja na kumuomba askari ruhusa kumuona rais JK.askari akamjibu mzee kwamba JK si rais tena na wala hakai ikulu.mzee taratibu akaondoka..siku ya pili mzee akarudi tena na kumuomba askari yule yule ruhusa ya kuingia na kumuona rais JK.Askari akamjibu wee mzee si jana nilikuambia kuwa JK sio rais tena na wala hana makazi ikulu? Mzee taratibu akaondoka na kwenda zake.Siku ya tatu mzee akarudi tena na kumuomba askari ruhusa ya kuingia ikulu ili amuone rais JK..Askari akamuangalia na kumuambia tena kwa utaratibu.Mzee ni siku ya tatu unakuja na kuuliza swali lile lile.nimekuambia JK sio rais bana.na wala haishi humu tena.kwa nini unauliza uliza? Mzee akamjibu askari.siulizi kwa ubaya ila toka juzi nafurahia sana majibu yako.Askari akanyooka na kumpigia mzee saluti na kumjibu tupatane tena kesho asubuhi mzee..duh!
 
Back
Top Bottom