Hii Ndoto inanisumbua Mwaka wa 12 Huu.

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Amani ya Bwana iwe Pamoja nanyi Ndugu zangu Wakristo/Waislam!

Nimejaribu kutafta msaada kuhusu hii ndoto kila mahala ila bado sijapata ufafanuzi wa kunisaidia.

IKO HIVI
Takribani miaka kumi na mbili iliyopita nimekuwa nikiota Ndoto, ndoto hii hutokea karibu na maji, tena maji ya mto yanayoenda kasi sanaa....Katika maji ya mto huu yanayoenda kasi nimekuwa na tabia ya kuvuka mto huu kwa shida sana japo kuna kufeli mara kadhaa ila huwa navuka Japo kwa shida sana.

Ndoto Hii huwa inajirudia sana...sometimes inakuwa ni mto ninaoufaham na mara nyingine sipajui kabisa (Kumbuka hii ndoto injihusisha na kuvuka tu mto wenye maji yanayoenda kasi)

Kila ninapoota hii ndoto yaani nakuwa na hofu hukohuko ndotoni.......Hali hii inanifikirisha sana.

Japo ni ndoto lakini nashangaa imejirudia kwa Miaka yote 12.

Ndugu zangu kwa wale Mliobarikiwa kuwa na uwezo wa kutafsiri ndoto nisaidieni ina Maana gani hii ndoto?

Asanteni sana!
 
Sio kwamba ndoto imekuwa ikijirudia, ila ni kwamba matukio yanayopelekea wewe kuota hicho unachokiota ndio yanajirudia.

TAFSIRI YAKE.

Unapita au hivi karibuni utapita kwenye msuko suko mkubwa aidha wa pesa au ndoa au chochote, ni kweli utavuka katika msuko suko huo ila ni kwa shida.
Waswahili wanasema, kufa hutakufa ila cha moto utakiona.

Cha kufanya.

Ukitoka hapo hapo kwenye ndoto unaomba kwa kuamuru kwa Mamlaka ya Jina la Yesu nasambaratisha misuko suko yote iliyo mbele yangu ambayo nimeiota kwenye ndoto ya kuvuka mto.

Ninaamuru daraja litokee katika huo mto nivuke bila misuko suko yoyote.
Unaweza kuweka na andiko kama lile la Yesu kuiamuru bahari ituie nayo ikatii au la Joshua na Makuhani wake walivyoyatindisha maji ya mto Yordani wakavuka salama.

Ajabu ni kuwa ukishamaliza maombi hayo ukalala tena, utaota ndoto ya pili tena inaonyesha kuwa unavuka salama, au umefika kwenye mto ukaahirisha kuvuka au utaona mawe ya kuvukia.

Kama utaona hujaridhika na ndoto ya pili, kwa maana kwamba umevuka ila ukalowana lowana au ulivuka kwa hofu, unaamuru tena kwa Jina la Yesu tena, na msuko suko utakoma.

Ndoto za namna hii sio za kuanza kulia lia Mungu akusaidie uvuke salama, ndoto za namna hii ni za kutumia mamlaka kuzisambaratisha, kumbuka Yesu aliwapa mamlaka wanafunzi wake ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za adui bila kudhurika.

Kwa hiyo usianze kulia lia au kumsihi Mungu aje akuokoe, yeye keshakupenyezea intelijensia, wewe inabidi uchukue hatua kwa kutumia mamlaka aliyokupa ndani ya Jina la Yesu na Damu ya Yesu.

Ndoto hio ni Mungu anajaribu kukuonya kuwa hivi karibuni kuna msuko suko, uchukue hatua, na sio ndoto mbaya ila ni ndoto ya onyo.

Na inatakiwa umuombe Mungu ndoto hio iwe inajirudia kama kuna msuko suko mahali uko mbele yako, na Mungu atakuwa akiona kuna jambo zito mbele atakuonya tena na tena.

Ubarikiwe.
 
Maana ya hii ndoto ni hii..

Kabla sijakueleza ndoto hii INA maana gani, elewa haya:-

# Maji
Maji hasa yanayoenda kasi au mengi mfano bahari au ziwa humaanisha tafrani au jambo kuu lenye dhiki.

Sasa basi nilivyoiangalia ndoto yako inamaanisha yafuatayo:-

Katika maisha yako kuna hatari kubwa ambazo hukunyemelea amabazo ndio hayo maji na huwa zinadiriki kukuangusha kama vile kukufilisi, kufa, kufungwa jela, au lolote kati ya Mayo, lakini wewe huwa /utazishinda kwa taabu sana.
Pia tambua kuwa hii ndoto huambatana na kuwa shida au taabu unazokumbana nazo husababisha na watu wanaokufahamu na kukuonea gere.
 
Mkuu ndoto yako nahitafsiri kama ifuatavyo

Wewe una kibamia ila unalazimisha kuingia kwenye rambo... sasa hali hiyo hujirudia pia ukiwa ndotoni jinsi unavyohangaika kujitutumua kwenye mshimo sio saizi yako
Be Matured Bro
 
Hahaaa you can't be serious aiseee!!!
 
Sio kwamba ndoto imekuwa ikijirudia, ila ni kwamba matukio yanayopelekea wewe kuota hicho unachokiota ndio yanajirudia.

TAFSIRI YAKE.

Unapita au hivi karibuni utapita kwenye msuko suko mkubwa aidha wa pesa au ndoa au chochote, ni kweli utavuka katika msuko suko huo ila ni kwa shida.
Waswahili wanasema, kufa hutakufa ila cha moto utakiona.

Cha kufanya.

Ukitoka hapo hapo kwenye ndoto unaomba kwa kuamuru kwa Mamlaka ya Jina la Yesu nasambaratisha misuko suko yote iliyo mbele yangu ambayo nimeiota kwenye ndoto ya kuvuka mto.

Ninaamuru daraja litokee katika huo mto nivuke bila misuko suko yoyote.
Unaweza kuweka na andiko kama lile la Yesu kuiamuru bahari ituie nayo ikatii au la Joshua na Makuhani wake walivyoyatindisha maji ya mto Yordani wakavuka salama.

Ajabu ni kuwa ukishamaliza maombi hayo ukalala tena, utaota ndoto ya pili tena inaonyesha kuwa unavuka salama, au umefika kwenye mto ukaahirisha kuvuka au utaona mawe ya kuvukia.

Kama utaona hujaridhika na ndoto ya pili, kwa maana kwamba umevuka ila ukalowana lowana au ulivuka kwa hofu, unaamuru tena kwa Jina la Yesu tena, na msuko suko utakoma.

Ndoto za namna hii sio za kuanza kulia lia Mungu akusaidie uvuke salama, ndoto za namna hii ni za kutumia mamlaka kuzisambaratisha, kumbuka Yesu aliwapa mamlaka wanafunzi wake ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za adui bila kudhurika.

Kwa hiyo usianze kulia lia au kumsihi Mungu aje akuokoe, yeye keshakupenyezea intelijensia, wewe inabidi uchukue hatua kwa kutumia mamlaka aliyokupa ndani ya Jina la Yesu na Damu ya Yesu.

Ndoto hio ni Mungu anajaribu kukuonya kuwa hivi karibuni kuna msuko suko, uchukue hatua, na sio ndoto mbaya ila ni ndoto ya onyo.

Na inatakiwa umuombe Mungu ndoto hio iwe inajirudia kama kuna msuko suko mahali uko mbele yako, na Mungu atakuwa akiona kuna jambo zito mbele atakuonya tena na tena.

Ubarikiwe.

Ubarikiwe Katika jina la Bwana Ndugu yangu katika kristo. Katika comment yako umenifungua Macho saana.....!
 
Mshukuru Mungu anakupigania maana kuna njia uniebdea ambayo si sawa. Jana lako tu lenyewe linaonyesha hupo kwenye mstari
 
Kwanza chunguza maeneo unayoishi kama unakaa mabonden chonga mtumbwi mapema ,hiyo ndoto inaonyesha mafuriko yanakuja
 
Back
Top Bottom