Hii ndoa ya kinafiki kati ya CCM na ACT Wazalendo huko Zanzibar inachekesha sana

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
39,901
95,404
Inajulikana wazi kuwa mbunge mteule wa CCM bwana Sheha Mpemba Fakhi amejiuzulu nafasi yake ya ubunge ili kuokoa Serikali ya umoja wa Kitaifa iliyopo kati ya CCM na ACT wazalendo baada ya ACT wazalendo kutishia kujitoa katika serikali hiyo baada ya tuhuma za wazi kuwa uchaguzi haukuwa wa huru na haki.

Lakini kinachochekesha ni kwamba sababu walizotoa MaCCM mbunge wao kujiuzulu ni mbunge wao huyo mteule ambaye hata hajaapishwa kwamba ana changamoto za kifamilia.

Shaka anasema kuwa CCM wamepokea uamuzi huo kwa mshituko mkubwa na wanachama wa CCM watulie katika kipindi hiki kizito😂😂😂

Lakini siasa za namna hii ambazo zinafanyika bila tume huru ya uchaguzi ni siasa zinazoliingizia Taifa gharama kubwa zisizo za msingi kwani inalazimika uchaguzi urudiwe tena.Imagine tume ya Taifa ya uchaguzi imevuruga uchaguzi makusudi kwa kumtangaza mtu ambae hakushinda uchaguzi huo na sasa hivi tume hiyohiyo inabidi ifanye tena uchaguzi mwingine kwa gharama ya kodi za Watanzania.

Kungekuwepo na tume huru ya uchaguzi ni wazi kabisa kuwa uchaguzi huu usingerudiwa tena kwani kusingekuwepo na malalamiko yoyote yale baada ya mshindi kutangazwa na tungekwepa hii gharama ya kurudia uchaguzi.Hiki ni kiashirio kingine kwa nini kunahitajika katiba mpya yenye tume huru ndani yake kwani ingekuwepo tume huru gharama kama hizi zingeokolewa.

U7Hwr.jpg
 
Hao ndio CCM!

Wanapiga ngoma kisha wengine mnaanza kudemka!

Hata kama hupendi lazima udemke
 
Back
Top Bottom