Hii ndo Zaburi ya 35 aliyotwambia tusome Halima Mdee

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
32,956
2,000
Yaani hizi siku 2 tu baada ya kuhamia huko kwa MATAGA tayari Halima ameshakua rafiki wa Gwajiboy?Maana hio mistari ya dini dizaini kama vile kapewa na Gwajiuno akaisome kwny Press.
Uno Uno Uno
 
Makerubi Mushi

Senior Member
Oct 14, 2018
116
225
Tuanomba asome Warumi 1; 26-28, Hivyo Mungu amewaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadiii matumizi ya asiiik kwa matumizi yasiyo ya asiii, wanaume nao hivyo hivyo, waiiacha matumizi ya mke wa asii, wakiwakiana tamaa wanaume wakitenda yasiyoyopasa wakapata nafsini mwao maiipo yaupotevu wao waiiyo haki yao.

Na kama waivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aiwaacha wafuate akiii zao zisizofaa wayafanye yasiyopasa. Je kama anafanya haya je Mungu hajamwacha anawezaje kutumia Zaburi ya 35 wakati Mungu kamuacha.
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
18,464
2,000

ZABURI 35​

Kuomba msaada
(Zaburi ya Daudi)

1 Ee Mwenyezi-Mungu, uwapinge hao wanaonipinga;
uwashambulie hao wanaonishambulia.

2 Utwae ngao yako na kingio lako,
uinuke uje ukanisaidie!

3 Chukua mkuki na sime yako dhidi ya wanaonifuatia.
Niambie mimi kwamba utaniokoa.

4 Waone haya na kuaibika,
hao wanaoyanyemelea maisha yangu!
Warudishwe nyuma kwa aibu,
hao wanaozua mabaya dhidi yangu.

5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
wakikimbizwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

6 Njia yao iwe ya giza na utelezi,
wakifukuzwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

7 Maana walinitegea mitego bila sababu;
walinichimbia shimo bila kisa chochote.

8 Maangamizi yawapate wao kwa ghafla,
wanaswe katika mtego wao wenyewe,
watumbukie humo na kuangamia!

9 Hapo mimi nitafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu;
nitashangilia kwa kuwa yeye ameniokoa.

10 Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote:
“Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe!
Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu,
maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.

11 Mashahidi wakorofi wanajitokeza;
wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12 Wananilipa mema yangu kwa mabaya;
nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

13 Lakini wao walipokuwa wagonjwa,
mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni;
nilijitesa kwa kujinyima chakula.
Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

14 kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.
Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,
kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.

15 Lakini mimi nilipoanguka walikusanyika kunisimanga.
Walikusanyika pamoja dhidi yangu.
Watu nisiowajua walinirarua bila kukoma,
wala hakuna aliyewazuia.

16 Watu ambao huwadhihaki vilema,
walinisagia meno yao kwa chuki.

17 Ee Mwenyezi-Mungu, utatazama tu mpaka lini?
Uniokoe kutoka kwenye mashambulio yao;
uyaokoe maisha yangu na simba hao.

18 Hapo nitakushukuru kati ya kusanyiko kubwa la watu;
nitakutukuza kati ya jumuiya kubwa ya watu.

19 Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange,
hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu.

20 Maneno wasemayo si ya amani,
wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu.

21 Wananishtaki kwa sauti:
“Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!”

22 Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo,
usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu,
usikae mbali nami.

23 Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee;
uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu.

24 Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, unitetee,
ufanye kulingana na uadilifu wako;
usiwaache maadui zangu wanisimange.

25 Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!”
Au waseme: “Tumemmaliza huyu!”

26 Waache hao wanaofurahia maafa yangu,
washindwe wote na kufedheheka.
Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi,
waone haya na kuaibika.

27 Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia,
wapaaze sauti kwa furaha waseme daima:
“Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno!
Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”

28 Hapo nami nitatangaza uadilifu wako;
nitasema sifa zako mchana kutwa.

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Kumbe taarabu zilikuwepo tangu kale
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
56,982
2,000
sawa, wanachama mko tayari kwa lolote, je, viongozi wenu wako tayari kwa lolote? hivi kweli Salim Mwalim alikuwa hajui mke wake Esther Matiko anaenda kuapishwa? kwenye lile kundi la akina mdee kuna wajumbe wa kamati kuu wana uhusiano wa karibu, usijidanganye walikuwa hawajui kinachoendelea......wakina halima watasamehewa na wataendelea na ubunge wao
Salimu Mwalimu ajue asijue cha msingi waasi hao walipaswa kutoa maelezo kwanini wameapishwa gereji bila idhini ya chama kwa mujibu wa katiba ya Chadema??
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,237
2,000
Sawa ukisemacho, lakini hao Chadema walizikamata Kwa Nani hizo kura mkuu

Ni walimtaja Nani waliyemkuta nazo?
Hujajibu swali langu.Narudia tena kukuuliza,kama ni chadema walichapisha kura fake kwa nini hawajakamatwa na polisi na kushtakiwa kwa kutenda kosa hilo ambalo ni very serious crime?
 
MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,064
2,000
Hii dhambi ambayo umeitenda kwenye jimbo lako umeshaitubu kwa wananchi wako? View attachment 1639057 View attachment 1639062 View attachment 1639063
CCM siyo mafala kiasi hicho waibe kura kwenye masanduku watembee nayo. huu ulikuwa plan 'B' ya Halima. hata km walipiga si kwa style hiyo. CDM ilipeleka mawakala bila kuwapa posho, bila kufanya uhakiki km siyo makada wa CCM, hapo ndiyo mchezo yote hufanyika kila mwaka lkn siyo kutembea na masanduku, hatuibaki hivo.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,237
2,000
CCM siyo mafala kiasi hicho waibe kura kwenye masanduku watembee nayo. huu ulikuwa plan 'B' ya Halima. hata km walipiga si kwa style hiyo. CDM ilipeleka mawakala bila kuwapa posho, bila kufanya uhakiki km siyo makada wa CCM, hapo ndiyo mchezo yote hufanyika kila mwaka lkn siyo kutembea na masanduku, hatuibaki hivo.
Kuchapisha kura fake na kutamba nazo mitaani tena kwenye vituo vya kupigia kura tena kwenye siku ya kupiga kura ni very serious crime,ni kosa la jinai ambalo ni serious sana!Sasa kama ni Mdee alichapisha kura fake kwa nini hajakamatwa na polisi na kushtakiwa kwa kutenda kosa hilo ambalo ni very serious crime?
 
MSHINO

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
1,064
2,000
Kuchapisha kura fake na kutamba nazo mitaani tena kwenye vituo vya kupigia kura tena kwenye siku ya kupiga kura ni very serious crime,ni kosa la jinai ambalo ni serious sana!Sasa kama ni Mdee alichapisha kura fake kwa nini hajakamatwa na polisi na kushtakiwa kwa kutenda kosa hilo ambalo ni very serious crime?
Hivi unamfahamu Halima, unamuona mtoto siyo? Halima amekaa kwenye game ya uchaguzi miaka 10, anajua kila mbinu, tuulize sisi tunaoishi jimbo lake, sema Halima alijisahau sana, kwa sababu Gwajima asingetoboa. wananchi walishamchoka.
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
21,743
2,000

ZABURI 35​

Kuomba msaada
(Zaburi ya Daudi)

1 Ee Mwenyezi-Mungu, uwapinge hao wanaonipinga;
uwashambulie hao wanaonishambulia.

2 Utwae ngao yako na kingio lako,
uinuke uje ukanisaidie!

3 Chukua mkuki na sime yako dhidi ya wanaonifuatia.
Niambie mimi kwamba utaniokoa.

4 Waone haya na kuaibika,
hao wanaoyanyemelea maisha yangu!
Warudishwe nyuma kwa aibu,
hao wanaozua mabaya dhidi yangu.

5 Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
wakikimbizwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

6 Njia yao iwe ya giza na utelezi,
wakifukuzwa na malaika wa Mwenyezi-Mungu!

7 Maana walinitegea mitego bila sababu;
walinichimbia shimo bila kisa chochote.

8 Maangamizi yawapate wao kwa ghafla,
wanaswe katika mtego wao wenyewe,
watumbukie humo na kuangamia!

9 Hapo mimi nitafurahi kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu;
nitashangilia kwa kuwa yeye ameniokoa.

10 Nitamwambia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote:
“Wewe ee Mwenyezi-Mungu, hakuna aliye kama wewe!
Wewe wawaokoa wanyonge makuchani mwa wenye nguvu,
maskini na fukara mikononi mwa wanyanganyi.

11 Mashahidi wakorofi wanajitokeza;
wananiuliza mambo nisiyoyajua.

12 Wananilipa mema yangu kwa mabaya;
nami binafsi nimebaki katika ukiwa.

13 Lakini wao walipokuwa wagonjwa,
mimi nilivaa magunia kuonesha huzuni;
nilijitesa kwa kujinyima chakula.
Nilisali nikiwa nimeinamisha kichwa,

14 kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.
Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,
kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.

15 Lakini mimi nilipoanguka walikusanyika kunisimanga.
Walikusanyika pamoja dhidi yangu.
Watu nisiowajua walinirarua bila kukoma,
wala hakuna aliyewazuia.

16 Watu ambao huwadhihaki vilema,
walinisagia meno yao kwa chuki.

17 Ee Mwenyezi-Mungu, utatazama tu mpaka lini?
Uniokoe kutoka kwenye mashambulio yao;
uyaokoe maisha yangu na simba hao.

18 Hapo nitakushukuru kati ya kusanyiko kubwa la watu;
nitakutukuza kati ya jumuiya kubwa ya watu.

19 Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange,
hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu.

20 Maneno wasemayo si ya amani,
wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu.

21 Wananishtaki kwa sauti:
“Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!”

22 Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo,
usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu,
usikae mbali nami.

23 Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee;
uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu.

24 Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, unitetee,
ufanye kulingana na uadilifu wako;
usiwaache maadui zangu wanisimange.

25 Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!”
Au waseme: “Tumemmaliza huyu!”

26 Waache hao wanaofurahia maafa yangu,
washindwe wote na kufedheheka.
Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi,
waone haya na kuaibika.

27 Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia,
wapaaze sauti kwa furaha waseme daima:
“Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno!
Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.”

28 Hapo nami nitatangaza uadilifu wako;
nitasema sifa zako mchana kutwa.

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Huo mstari wa 12 ndio unamuhukumu kwa maamuzi yake umwbeba vyote vinavyoendele juu yake
 
Rugaiyulula

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,523
2,000
Mwambie naye asome ZABURI 1: 1 - 6.

1.Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2.Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3.Naye atakuwa kama mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.

4.Sivyo walivyo wasio haki;
Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5.Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,
Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

6.Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,
Bali njia ya wasio haki itapotea.
Kwa kweli kamwaga ugali naona nawe umemwaga mboga 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
7,804
2,000
Wewe endelea kuchanganya siasa na dini tu, baada yako atakuja naye muislamu aweke yake, na budhist, bohra, ismalia n.k. n.k. Sijuwi tutafikia wapi?!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom