Hii ndo Tanzania yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii ndo Tanzania yetu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chuhila, Mar 18, 2010.

 1. c

  chuhila Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Je sheria hii mpya ya uchaguzi iliyosainiwa kwa mbwembwe zote kama ilivyokuwa imeahidiwa hapo awali itaweza kupunguza rushwa katika uchaguzi na hivyo kutupatia viongozi bora? Kama hivyo ndivyo nini hofu ya wanasiasa wa upinzani? Je wanaona ni kiinimacho?

  Tanzania kwa sasa yahitaji matendo ili iendelee na si maneno matupu ambayo mengi yao yamejaa hila na chuki za kisiasa. Mitandao ya rushwa na hongo kubwa kubwa nchini ni maingi na haiwezi kwisha kwa sababu hata hao wanaodhaniwa kuwa ni wapinga na wadhibiti rushwa wanafanya vitendo vya rushwa.

  Sasa nini mstakabali wa nchi yetu hasa katika mwaka huu wa uchaguzi? Yatubidi kujiuliza kwa sababu uchaguguzi utaleta viongozi wa kuongoza kama sio kutawala kwa miaka mingine mitano.
   
Loading...