Hii ndo siri ya taarifa ya TV zote kulazimishwa kujiunga TBC saa mbili jioni

Mimi siwezi kuangalia TBCCM
Mwaka juzi kulikuwa na sintofahamu kuhusu nani achinje iliyosababisha kifo cha mchungaji moja kanda ya ziwa. Wakati sarakasi hiyo ikiwachanganya watanzania, katibu wa Bunge Thomas Kashillah aliibuka na kusema Bunge halitaoneshwa tena kwenye Runinga. Mjadala ukahama kutoka uchinjaji na kuwa Bunge kutooneshwa. Serikali ikafanikiwa, kombe likafunikwa na mwanaharamu akapita.

Mwaka 2013 mvua kubwa kuliko hii ya mwaka huu ilinyesha na kusababisha mamia ya watu kulala njiani na njaa wakiwa na watoto. Njia zote za kuingia Dsm zilifungwa na maji na matokeo yake watu wakawa na hasira na serikali kutosimamia miundo mbinu vizuri jambo lililosababishia wao kupata madhara yale. wakati hayo yakipamba kwenye vyombo vya habari ghafla tukaambiwa Makamu wa Rais, waziri magufuli na mkuu wa mkoa wa Dsm wameanguka na helikopta. kama kwaida Mjadala ukahama kwa walioanguka na helikopta. Mwanaharamu akapita tena. Ikumbukwe kuwa hakuna kati ya walioanguka na helikopta aliyenda hospitali wala picha ya helikopta iliyoanguka haikuonekana mpaka leo kama kaburi la Daudi Balali wa EPA iliyoibuliwa na Dr Dlaa.

Wakati wa Bunge la katiba, Tundu Lissu na UKAWA waliibua madudu mengi kuhusu muungano hasa pale walipohoji lilipo kaburi la waasisi wa muungano amabao ni Hanga na wenzake. Wakati mjadala huo ukishika kasi Dodoma, ghafla serikali ikaibuka na ugonjwa wa Dengue. Tukaambiwa wamekufa watu wawili mara watatu wakati malaria inaua zaidi ya watu watatu kila siku achilia mbali hao watatu hata kama ni zaidi ya watatu waliokufa mara moja na Dengue. Baada ya hoja ya Muungano kupita Dengue nayo ikayeyuka bila maelezo ya kutosha.

Je, watu wameshajiuliza kwanini magaidi feki wa amaboni walikuja wakati hoja ya ESCROW ikivuma? Tuliambiwa kuna askari wetu wamekufa. Je, akina nani kwa majina na walizikwa wapi na lini? Nani ameona picha hata moja ya askari wetu?

Mifano ya usanii huu wa serikali kuibua hoja ili kujilinda au kufunika udhaifu wake ni mingi sana. Huko nyuma nilishaandika zaidi ya mifano kumi ya namna hii. Mifano hii michache inatosha kujenga hoja yangu. Kwa nini nimeyaeleza yote hayo??

Jana jioni nilimsikia kwenye ITV mwenyekiti wa MOAT ndugu Reginald Mengi akilalamikia serikali kutaka kupeleka mswada wa uhuru wa habari ambao moja ya kipengele chake kinavilazimisha vyombo vyote vya habari vikiwepo ITV, STAR TV, Chanel ten nk vijiunge na TBC saa mbili usiku kwa taarifa ya habari. kwamba vyombo vingine (TV zingine) havipaswi kuwa na taarifa yao ya habari wenyewe badala yake sheria itawalazimisha wajiunge na TBC. Je, hili linawezekana??

Mimi kama MIKAEL AWEDA sidanganyiki na hili. Nina wasi wasi nalo. Siamini kabisa nikirejea mifano tajwa hapo juu. Kwa maoni yangu taarifa hii imeletwa ili kubadilisha au kusahaulisha au kufunika mjadala wa ufisadi wa zaidi ya trilioni moja ulioibuliwa na Chadema baada ya kuchambua ripoti ya CAG. Kwa hiyo, taarifa hii imeletwa makusudi wakati bunge na vyombo vya habari vikijadili ufisadi huu wa serikali. Nijuavyo, Bungeni wakishamaliza taarifa hii ya TV zote kujiunga na TBC saa mbili jioni nayo itayeyeka kama taarifa ya Dengue, hoja ya kashilillah ya Bunge kutooneshwa na TV au helikopta kuanguka bila majeruhi wala picha yake kuonekana.

Nihitimiasha kwa kusema kuwa ninahitaji muda zaidi kuamini hili vinginevyo mwana wa Aweda hadanganywi na janja ya kufunika wizi wa matrilioni yaliyoibwa na viongozi wa serikali kwa kuibua hoja mbadala.

Nawasilisha
Mikael Aweda
0784 583 330
22/05/2015
 
hii ndo serikali sikivu ya kj. kuendelea kuipa ccm kura ni kusaliti taifa letu pendwa liitwalo tanganyika.
 
Ingenoga zaidi kama ungehusisha mfano wa Babu wa Loliondo wakati wa Dowance..!!

Hii ni hatari kubwa sana, inajenga taifa linalozoea kuiba taifa lisilowajibika iwe viongozi wao au Wananchi wenyewe, hapa hata akisimama Dr Slaa na kupigia kelele ufisadi huo itaonekana ni kawaida tu kwa Dr kulalamika, Wananchi watamsukiliza kisha wakaendelea na Mambo yao. Hakuna hatua yoyote inayochukuliwa. Kwa hapa tulipofika tunaitafuta Nigeria kwa kasi kubwa sana kwa ufisadi.

BACK TANGANYIKA

Kwei mkuu masikio yetu yamezoea kusikia hizi habari za ufisadi kiasi kwamba inakuwa kawaida maana baadae inakuwa kimya tena tunasubiri ufisadi mwingine utokee, nguvu inakuwa kubwa tunasahau hata kuangalia upande wa kuongeza makusanyo mengine zaidi na kubaki kukemea ufisadi ambao umetokana na makusanyo machache.

Nchi yetu ni wazee wa tria and error na sidhani kama hizi sheria zinatungwa na wataalam kama sio shinikizo la wanasiasa kwa kuwalazimisha warekebishe baadhi ya vitu kabla ya kuuleta mswada kwa majadiliano
 
Kwanza hyo sheria kweli ipo??
Maana inaweza kuwa ni ile ya miaka ya nyuma ambayo ilikuwa inazitaka radio binafsi kujiunga, cna kumbukumbu tv.. ila kama ipo naomba nakara tuwekewe ili tuisome,
Pili cna kumbukumbu nimeangalia lin tbc, may b wakati wa bunge, tatzo ni aina ya vipindi na ubunifu
Wakati yupo Tido kulikuwa na ubunifu na uwajibikaji leo ni boya tu..

Tatu nakubaliana na mtoa hoja kuwa huenda hii ni story ili kutuhamisha kwenye ajenda kuu
Nashawishika kukubali kutokana na hali halisi..
Think properly
 
Pumbaaaaaaaaaaa na upumbavu wa viroba. ITV na TBC ni ipi ilianza? Chanel Ten tunatizama saa moja. Hamna anayelazimishwa kwani Tv iko nyumbani kwako na remote unayo mwenyewe,nani atakuchagulia steshen. Mkiambiwa muache viroba hamsikii. Kila siku nawaita Baraza la vichaa Chadema (Bavicha) kwa kusapoti upuuzi kama huu
 
Hawajabadilika hata kidogo,tena sasa ndiyo mbaya zaidi............Ndicho hicho nachosemea,ile sheria haijafunga hizi station za binafsi kutangaza taarifa ya habari!Cha msingi ni muda tu uwe tofauti...Na kinachobaki ni uamuzi wa mlaji kuangalia au kutoangalia...........

Na hawawezi kuja nyumbani kwako wakakulazimisha uangalie TBCCM

we hujui saa mbili ndo mda mzur...kabla ya hapo na baada ya hapo wengi hawataona taarifa ya habari nzuri...
 
Michael Aweda, aliyosema Mengi yanaukweli na hiki ndicho kifungu Mengi alichokisemea jana

Chombo cha Habari kitakuwa na majukumu yafuatayo:- (a)

I .kwa chombo cha Habari cha Umma;
II. kutoa huduma ya habari kwa wote;

III.kutoa huduma za habari kwa Umma na Serikali,

IV.kuzingatia Maadili na Kanuni za Kitaaluma,

V.kuimarisha mawasiliano ya Serikali pamoja na mawasiliano ya Serikali na Umma,

kuujulisha Umma kuhusu masuala ya Maendeleo yanayofanywa na Serikali pamoja na Sekta ya umma

B) kwa chombo cha Habari Binafsi;

I..kutoa huduma za habari kwa Umma kwa kuzingatia masharti ya maeneo ya Kijiografia kwa mujibu wa Sheria hii.

II.kuzingatia Maadili na Kanuni za Kitaaluma;

III.kukuza uelewa kwa Umma katika masuala yenye manufaa kwa Taifa kupitia usambazaji wa habari;

IV.kujiunga na Chombo cha Habari cha Umma kwa ajili ya taarifa za habari za kila siku saa mbili usiku ili kuuwezesha Umma kufuatilia masuala muhimu ya kitaifa

Kifungu hiki cha IV ndicho kinacholeta makatizo mengi kwa binadamu wanasihasa wa Chiechiem
Sheria inatungwa kana kwamba taarifa ya habari ya saa mbili ni 'biblical' na kwamba haitatokea chombo hicho cha umma kikaona muda mzuri wa taarifa ya habari ni saa moja, tatu au hata kumi na mbili! Kwa nini ulazimishe watu wote kusikiliza hiyo taarifa ya habari hata kama hawapendi na unawanyima chaguo wanalolipenda? Haya yanaonekana Korea kaskazini tu sasa hivi!
 
we hujui saa mbili ndo mda mzur...kabla ya hapo na baada ya hapo wengi hawataona taarifa ya habari nzuri...
Haya ni mazoezi tu, nchi nyingi zinazotuzunguka prime time ya habari ni saa tatu. Hata hivyo kulazimisha chombo cha mtu binafsi anaye fanya biashara kutangaza habari zisizo uzi ka kwake ni kumuonea na ni dalili za udikteta. Je watatoa ruzuku kwa muda huo...?
 
Pumbaaaaaaaaaaa na upumbavu wa viroba. ITV na TBC ni ipi ilianza? Chanel Ten tunatizama saa moja. Hamna anayelazimishwa kwani Tv iko nyumbani kwako na remote unayo mwenyewe,nani atakuchagulia steshen. Mkiambiwa muache viroba hamsikii. Kila siku nawaita Baraza la vichaa Chadema (Bavicha) kwa kusapoti upuuzi kama huu

Ilianza ITV kabla ya TVT iliyokuja itwa TBC. hivi wale wabunge wapya wa kuteuliwa wanachangia na kutoa hoja kwenye hili bunge?
 
Oohoops! Here there is a truth from the facts and truth from the reasoning, both can derive the truth and probably shape society; + or -ly. What I believe is that, to you Mr. Aweda the only truth is what you see by your eyes.
 
Sheria inatungwa kana kwamba taarifa ya habari ya saa mbili ni 'biblical' na kwamba haitatokea chombo hicho cha umma kikaona muda mzuri wa taarifa ya habari ni saa moja, tatu au hata kumi na mbili! Kwa nini ulazimishe watu wote kusikiliza hiyo taarifa ya habari hata kama hawapendi na unawanyima chaguo wanalolipenda? Haya yanaonekana Korea kaskazini tu sasa hivi!

Nadhani Prof amefika mwisho wa kufikiri.Sielewi wanataka kutuficha nini na maisha yenyewe ya mtandao haya.Hata ukiwa uko chooni watakupata tu wakiamua.

Ila raisi ajaye anatakiwa awe very smart.Kuyapiga chini haya hote yanayofanyika dakika za majeruhi.Sina uhakika kama wanaCCM wanafurahia haya.Na sijui kama kweli anatutakia mema.Huyu bwana anagiza magari 700 ya polisi ameshindwa kununua BVR..haya tuko busy na mambi ya upuuzi ya maana tumewaachia watoto.
 
Mwaka juzi kulikuwa na sintofahamu kuhusu nani achinje iliyosababisha kifo cha mchungaji moja kanda ya ziwa. Wakati sarakasi hiyo ikiwachanganya watanzania, katibu wa Bunge Thomas Kashillah aliibuka na kusema Bunge halitaoneshwa tena kwenye Runinga. Mjadala ukahama kutoka uchinjaji na kuwa Bunge kutooneshwa. Serikali ikafanikiwa, kombe likafunikwa na mwanaharamu akapita.

Mwaka 2013 mvua kubwa kuliko hii ya mwaka huu ilinyesha na kusababisha mamia ya watu kulala njiani na njaa wakiwa na watoto. Njia zote za kuingia Dsm zilifungwa na maji na matokeo yake watu wakawa na hasira na serikali kutosimamia miundo mbinu vizuri jambo lililosababishia wao kupata madhara yale. wakati hayo yakipamba kwenye vyombo vya habari ghafla tukaambiwa Makamu wa Rais, waziri magufuli na mkuu wa mkoa wa Dsm wameanguka na helikopta. kama kwaida Mjadala ukahama kwa walioanguka na helikopta. Mwanaharamu akapita tena. Ikumbukwe kuwa hakuna kati ya walioanguka na helikopta aliyenda hospitali wala picha ya helikopta iliyoanguka haikuonekana mpaka leo kama kaburi la Daudi Balali wa EPA iliyoibuliwa na Dr Dlaa.

Wakati wa Bunge la katiba, Tundu Lissu na UKAWA waliibua madudu mengi kuhusu muungano hasa pale walipohoji lilipo kaburi la waasisi wa muungano amabao ni Hanga na wenzake. Wakati mjadala huo ukishika kasi Dodoma, ghafla serikali ikaibuka na ugonjwa wa Dengue. Tukaambiwa wamekufa watu wawili mara watatu wakati malaria inaua zaidi ya watu watatu kila siku achilia mbali hao watatu hata kama ni zaidi ya watatu waliokufa mara moja na Dengue. Baada ya hoja ya Muungano kupita Dengue nayo ikayeyuka bila maelezo ya kutosha.

Je, watu wameshajiuliza kwanini magaidi feki wa amaboni walikuja wakati hoja ya ESCROW ikivuma? Tuliambiwa kuna askari wetu wamekufa. Je, akina nani kwa majina na walizikwa wapi na lini? Nani ameona picha hata moja ya askari wetu?

Mifano ya usanii huu wa serikali kuibua hoja ili kujilinda au kufunika udhaifu wake ni mingi sana. Huko nyuma nilishaandika zaidi ya mifano kumi ya namna hii. Mifano hii michache inatosha kujenga hoja yangu. Kwa nini nimeyaeleza yote hayo??

Jana jioni nilimsikia kwenye ITV mwenyekiti wa MOAT ndugu Reginald Mengi akilalamikia serikali kutaka kupeleka mswada wa uhuru wa habari ambao moja ya kipengele chake kinavilazimisha vyombo vyote vya habari vikiwepo ITV, STAR TV, Chanel ten nk vijiunge na TBC saa mbili usiku kwa taarifa ya habari. kwamba vyombo vingine (TV zingine) havipaswi kuwa na taarifa yao ya habari wenyewe badala yake sheria itawalazimisha wajiunge na TBC. Je, hili linawezekana??

Mimi kama MIKAEL AWEDA sidanganyiki na hili. Nina wasi wasi nalo. Siamini kabisa nikirejea mifano tajwa hapo juu. Kwa maoni yangu taarifa hii imeletwa ili kubadilisha au kusahaulisha au kufunika mjadala wa ufisadi wa zaidi ya trilioni moja ulioibuliwa na Chadema baada ya kuchambua ripoti ya CAG. Kwa hiyo, taarifa hii imeletwa makusudi wakati bunge na vyombo vya habari vikijadili ufisadi huu wa serikali. Nijuavyo, Bungeni wakishamaliza taarifa hii ya TV zote kujiunga na TBC saa mbili jioni nayo itayeyeka kama taarifa ya Dengue, hoja ya kashilillah ya Bunge kutooneshwa na TV au helikopta kuanguka bila majeruhi wala picha yake kuonekana.

Nihitimiasha kwa kusema kuwa ninahitaji muda zaidi kuamini hili vinginevyo mwana wa Aweda hadanganywi na janja ya kufunika wizi wa matrilioni yaliyoibwa na viongozi wa serikali kwa kuibua hoja mbadala.

Nawasilisha
Mikael Aweda
0784 583 330
22/05/2015

Naona unafananisha 'apples' na 'oranges'.
 
Very shallow. Unataka kuwa shujaa over nothing. Hatukubaliani na hatua ya serikali Lakini hii post yako too thin
 
nani atazame tbc, wakati wa habari nitapata muda wa kutazama tamthilia na movie nizipendazo
 
Kina BBC na nduguze nao watakuwa wanajiunga na TBC au?
Lkn haina shida wajiunge tu wakimaliza wanaanza yao au wanaanza taarifa zao kabla ya saa mbili ikifika saa mbili wanajiunga nao
 
Ni wazo zuri la serikali, hao wengine wanaweza kuchagua mida mingine ya kuonyesha habari...Sijaona tatizo katika hilo.
Ingekuwa wamezuiwa kutoa habari hapo sawa.
Tutazoea tu...tuheshimu serikali iliyopo madarakani.
hata kama inafanya ujinga na haiwaheshimu watu wake iheshimiwe tu?serikali isiyojiheshimu sioni kama inasitahili kuheshimiwa pia
 
Back
Top Bottom