Serikali kabla ya kutunga sheria na kuanza kutumika ingekuwa ni vizuri ikaelimisha wananchi kwa kuweka matangazo kwenye Radio na TV.
Kuna wananchi wengi watajikuta wakilipa faini au kufungwa gerezani kwa sababu ya kutenda kosa bila kujua.
Ninajua ujinga sio utetezi lakini serikali lazima itumie hekima na busara kabla ya sheria kuanza kutumika.
Kwa sasa ukiongea na watu wengi hasa huku kijijini wanasema siku hizi sheria ni nyingi sana!Ni kweli...kama yule Mtanzania kule alijikuta yuko lupango kwa kusambaza picha za wahanga wa tukio la kigaidi...hapa kwetu zile picha za wahanga wa moto wa lori pale Morogoro zilisambazawa kwenye mitandao...Elimu ni muhimu kwa kweli ingawa kama ulivyosema 'ignorancce of the law is no defence'