Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,900
6,657
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.

Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.

Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri.

Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.

Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)

Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.

Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao...

Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).

Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.

Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.

Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza

Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.

Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.

Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.

Catholic theological reflection.

Wanateolojia wa kanisa husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa MWANZO 3:15 kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.

Lakini Mungu anajua Zaidi (An omniscient) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu naomba hicho kitabu kama unacho nikisome mwenyewe. Tuma pdf yake humu
Icho hapo
FB_IMG_1617338326465.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani" kwahiyo unataka kusema bila malaika kumwambia Mungu asingejua matendo ya hao malaika?

"Lakini Mungu anajua Zaidi (AN OMNISCIENT) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu"

Kupitia hizo paragraph 2 inaonekana kama kuna ukomo wa kuona au kujua mambo Kwa Mungu, kama anajua zaidi hadi akafuta kizazi cha Nuhu nazani lengo lilikuwa ni kuondoa kizazi kiovu cha Nuhu na kuleta kizazi kizuri Ila cha ajabu hiki kizazi ndio kibaya kuliko ata cha Nuhu hivo sidhani kama alijua na hiki kizazi kitakuwa hivi

Kuendelea kumuacha shetani uraiani ili binadamu apambane nae mwenyewe ni Sawa na kujitekenya mwenyewe na kucheka mwenyewe, kama Baba huwezi kuwatakia mema watoto wako Kwa kuwaweka chumba kimoja na Nyoka, kuendelea kutuweka zizi moja na shetani na kutegemea tutakuwa tofauti na kina Nuhu inabidi uwe na akili za Wanyonge kuamini hili, Kamata shetani funga huko dunia iwe sehemu salama easy tu
 
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakinj ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi....
Nimekisoma chote hicho kitabu kina siri nyingi sana ambazo hazijulikani
 
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakinj ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi...
Niliwahi kupata dokezo kidogo wa hiki kitabu kupitia jarida moja la mashahidi wa yehova.. itabidi nikitafute nikipitie aisee.
 
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakinj ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi....
Aisee umejitahidi mkuu!
 
Ndio maana ya imani. Huwezi kulazimisha watu wengine waamini katika maandiko fulani, lakini inawezekana kwako wewe kuamini maandiko hayo. Kama ni kweli unayoyasema, basi RC waliona hayo maandiko hayaendani na imani yao.

Lakini RC hawajamzuia mtu kuyaamini. Cha ajabu watu wanataka wengine waamini imani fulani wakati wapo huru kuifuata, na hata katiba za nchi nyingi zinaruhusu tu
 
Maandiko ya Biblia yanajitosheleza kabisa, na ndio Mungu kataka tusome hayo tu.

Nje na hapo hakuna hekima tena, labda ukajifunze uchawi tu huko nje ya biblia.
Hiko kitabu kinatumika na Ethiopian Orthodox ambalo ndio kanisa la Kwanza Afrika hata kabla RC haijafikiriwa kuanza.

Je unaona nani yupo sahihi hapo? Au inakua halali pale tu mzungu akikiweka kwenye biblia?

Mfano Wimbo ulio bora una changamoto zote kma book of Enoch ila hakijatolewa and more so hta makanisani hakifundishwi regularly!! But kingekua nje ya Biblia kama naona jinsi mngekikejeli.
 
Hiko kitabu kinatumika na Ethiopian Orthodox ambalo ndio kanisa la Kwanza Afrika hata kabla RC haijafikiriwa kuanza.

Je unaona nani yupo sahihi hapo? Au inakua halali pale tu mzungu akikiweka kwenye biblia?

Mfano Wimbo ulio bora una changamoto zote kma book of Enoch ila hakijatolewa and more so hta makanisani hakifundishwi regularly!! But kingekua nje ya Biblia kama naona jinsi mngekikejeli.
Mimi naujua umuhimu wa agano la kale na muhubiri anatakiwa kulitumia vipi agano la kale kufundisha neno la Mungu,
Agano jipya pia.

Sasa kama kuna kitu cha muhimu mwanadamu kukijua na hakipo ndani ya biblia kiseme.

Kwasababu biblia inasema laiti kama biblia ingeandika kila alilolifanya Yesu kipindi chake isinge wezekana ?
Yohana 21:25
[25]Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
 
Mimi naujua umuhimu wa agano la kale na muhubiri anatakiwa kulitumia vipi agano la kale kufundisha neno la Mungu,
Agano jipya pia.

Sasa kama kuna kitu cha muhimu mwanadamu kukijua na hakipo ndani ya biblia kiseme.

Kwasababu biblia inasema laiti kama biblia ingeandika kila alilolifanya Yesu kipindi chake isinge wezekana ?
Yohana 21:25
[25]Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
Kasome Yuda 6 na 14-15 alafu uniambie ilikua quoted kutoka kitabu gani cha agano la kale then ukifaham naomba ukaulize kwanini mitume walikisoma alafu sisi tukataliwe?
 
Agano jipya.... Yuda mstari wa 6 na 14-15 then unipe mrejesho kuendana na nlichouliza hapo juu
Nimesoma kitabu hicho cha Yuda.

Lakini point yangu itabaki pale pale, ni mafundisho yapi ya Henoko unayoyalilia wewe ukitaka yawekwe kwenye biblia.

Manabii wa zamani walitoa unabii kuwaonya watu wa kipindi kile, si henoko peke yake alifanya hivo, wapo manabii wengi tu.

Lakini swali linakuja wewe uliyesoma kitabu cha henoko unanizidi nini mimi ambae sijakisoma. ?

Na kama waliounganisha vitatu vilivyounda Biblia waliona hakifai Roho mtakatifu aliwaonesha kuwa kimechakachuliwa ? Au si cha muhimu.
Utalazimisha kiwepo kwenye Biblia ?

Kama henoko anamafundisho muhimu sana, tuambie.
Maana mimi najua hata vitabu vya Solomon si vyote vilichukuliwa na kuwekwa kwenye biblia.
 
80 Reactions
Reply
Back
Top Bottom