Hii ndo sababu Mahakama kuonekana kichaka cha Wanasiasa hasa CCM

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,148
25,814
Amani iwe nanyi wana Tanzania!

Moderators naomba msiunganishe wala kufuta huu uzi! Maana ni wa kipekee

Leo nimemsikia Jaji Mkuu akiongea na majaji na mahakimu huko Morogoro. Kilichonishangaza ni maneno aliyosema Eti wajaji na Mahakimu hasa kwenye kutoa haki wawe makini ili mahakama isionekane kama kichaka cha wanasiasa

Labda swali la kumuuliza Jaji Mkuu anafikiri kwa nini Mahakama kwa sasa ukiondoa Mahakama kuu tu ndo inaonekana kichaka cha wanasiasa?

Leo naomba nimuelezee kidogo!
Dunia nzima, mhimili uliowekwa kwa makusudi ili kulinda haki za wananchi dhidi ya serikali, viongozi na hata bunge, ni Mahakama.

Duniani kote, hata marais wakorofi huwa ukorofi wao unadhibitiwa na Mahakama. Ndo mana unaona hata nchini Marekani Trump ameweza kuwa Raisi kwa sababu maamuzi yake ya kipuuzi huwa yanapigwa nyundo na Mahakama.

Kwa hapa Tanzania , wenye akili zao waliona umuhimu wa mahakama ndo mana wakaweka article 107 ya katiba yetu hii hii mbovu inayosema mamlaka ya mwisho ya kutoa haki nchini itakuwa ni Mahakama. Kwa msingi wa kipengele hiki, ndo mana hata Majaji waliwekewa utaratibu maalumu wa kuwatoa kwenye nafasi zao ambao sio wa kawaida na ni mgumu kupindukia. Leo hii raisi anaweza kumtoa mkuu wa majeshi, kumvua jenerali nyota, kumvua mtu uwaziri mkuu ila hawezi kamwe kuamka tu na kusema namnyang’anya fulani ujaji. Ni lazima apitie utaratibu mgumu sana uliowekwa na katiba.

Shida kubwa iliyoonekana katika Awamu hii ya tano ni pale Mahakama hasa mahakama ya Rufaa ilivyokuja kujionesha kuwa ni chombo ambacho kazi yake ni kuwalamba miguu watawala.

Katika awamu hii ya Tano ndo awamu ambayo Mahakama ya Rufaa imejidhalilisha vibaya kwanza kwa maamuzi ya hovyo ya kurudisha wakurugenzi kusimamia uchaguzi ambapo kwa matendo yao hadi tumeona damu zikimwagika kwenye uchaguzi huu. Pili ni maamuzi waliyotoa ya kurudisha kipengele cha sheria cha kuruhusu serikali kushikilia watu na kuwanyima dhamana.

Kwanini lawama ni kwa mahakama ya rufaa???

Maamuzi mawili yaliyofanywa na mahakama ya rufaa yote yalianzia Mahakama kuu! Majaji wa Mahakama kuu wakielewa nafasi zao na unyeti wao kama majaji kuwa hawawezi kuendeshwa na mwanasiasa yeyote walitoa hukumu Nzito mbili ambazo zilitengeneza mwanga mpya kwa Tanzania. Hukumu ya kuwatoa wakurugenzi kusimamia uchaguzi iliweka njia Nzuri kuelekea Tume huru ya uchaguzi na hukumu ya kuzuia kifungu cha sheria kinachowanyima watu dhamana iliweka mwanga kuelekea Tanzania yenye amani na furaha kwa watu wake!

Shida ni Mahakama ya Rufaa ilivyoamua kwenda kinyume na nafasi nyeti iliyopewa na kupindua maamuzi haya muhimu ambayo yalikuwa yanaenda kuibadiri Tanzania.

Ni ukweli ulio dhahiri kuwa Jaji Mkuu anatakiwa afahamu kuwa ili Mahakama hasa Mahakama ya rufaa irudi kwenye nafasi ya kuheshimiwa na watanzania wote, ni vizuri majaji hawa wakajifunza kuwa kama Majaji kama Jaji Samata, Jaji Ramadhani, Jaji Kisanga, Jaji Rugakingira na Jaji Mwalusanya (ingawa hawakufika Mahakama ya Rufaa ila maamuzi yao yaliipa heshima mahakama ya Tanzania dunia nzima)

Ni Wakati wa Majaji wa Rufaa kujitambua na kubadirika!!
 
Nimemwona jaji mkuu, sura yake na anachoongea ni tofauti, nadhani alikuwa anaanua ngoma juani
 
Hasa huyu mama Mugasha, Mungu atakupiga kofi baya sana! Wewe ndiye uliyeto maamuzi ya MADED, ULAANIWE NA UZAO WAKO
Ni hatari kuu pale Mahakama inapogeuka mlamba viatu wa watawala. Matokeo yake wananchi wataamua kuchukua sheria mkononi kwa sababu chombo kinachotegemewa kuwapa haki kinawageuka na kuwa kibaraka wa watawala na agenda zao!
 
Huyu Jaji wa sasa ni mnafiki. Kwa uhakika wa 100%, mara kadhaa amekuwa akifanya vikao mbalimbali na viongozi wakuu wa CCM kupanga hukumu.

Tatizo kubwa kabisa la mahakama limesababishwa na huju jaji kada wa CCM. Huyu ameiharibu mahakama kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo.

Maneno yake msiyaamini kabisa. Jaji ameinajisi mahakama kwa kuifanya mahakama kuwa kitengo cha chama.

Hata kama Watanzania mara nyingi hawasemi lakini wanawajua viongpzi wote wanafiki. Huyu Jaji na Spika, ndio walioua mihimili miwili na wao kuamua kuwa sehemu ya muhimili wa Serikali.

Hawana jema ambalo kwalo watakumbukwa bali kwa uovu na unafiki wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Jaji wa sasa ni mnafiki. Kwa uhakika wa 100%, mara kadhaa amekuwa akifanya vikao mbalimbali na viongozi wakuu wa CCM kupanga hukumu.

Tatizo kubwa kabisa la mahakama limesababishwa na huju jaji kada wa CCM. Huyu ameiharibu mahakama kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo...
Anashindwa kujifunza hata kwa Jaji Nyalali. Jaji Nyalali alisave kipindi cha Chama kimoja ila alitofautiana na CCM na aliweza kum convince nyerere.

Hakuna majaji ninaowadharau kama majaji wa kipindi hiki!!! Wengi najua hawajui hata unyeti na ukubwa wa nafasi zao kama majaji!!! Wapowapo tu kila siku kujipendekeza kwa magufuli. Shame!!
 
Huyu Jaji wa sasa ni mnafiki. Kwa uhakika wa 100%, mara kadhaa amekuwa akifanya vikao mbalimbali na viongozi wakuu wa CCM kupanga hukumu.

Tatizo kubwa kabisa la mahakama limesababishwa na huju jaji kada wa CCM. Huyu ameiharibu mahakama kwa kiwango ambacho hakijawahi kuwepo...
Jaji anae kunywa chai kila asubuhi Ikulu (kila ufunguzi yupo) kuapishwa Dc yupo ajabu
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom