Hii Ndo Njia Mojawapo Ya Kukabiliana Na Watu Wapenda Vyeo Lakini Hawataki Kujenga Chama Ndani Ya CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii Ndo Njia Mojawapo Ya Kukabiliana Na Watu Wapenda Vyeo Lakini Hawataki Kujenga Chama Ndani Ya CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Uyole12, Oct 19, 2012.

 1. U

  Uyole12 JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 586
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwanza kabisa naomba niwapepole watu wanaofanyia kazi maeneo ya Kariakoo maana siku ya leo ndo tumejua kwa nini watu wa Arusha ni Majasiri na hawaogopi mabomu ya machozi kwa sababu tu wameyazoea.

  Baada ya kutoa pole zangu naomba nijikite kwenye maada halisi iliyofanya leo hii nitume post JF. Hakika nimekuwa msomaji mzuri wa post mbalimbali hapa ndani na nimeona nitume mawanzo yangu kwa viongozi wa CDM maana mjenga chama ni mwanachama na mbomoa chama ni Mwanachama Mwenyewe. Nimekua naona post mbalimbali zinazoonyesha jinsi vijana CDM wanavyoutaka Uraisi kwa udi na uvumba wakati huu ni muda wa kujenga chama kupitia M4F. Nikaona nitoe ombi langu kwa viongozi wangu jinsi ya kukabiliana na hawa mabwana wapenda Uraisi.

  Napendekeza itakapo fika wakati wa kumtafuta mgombea wa Uraisi basi Wagombea wote waende kuomba kula kwa wanachama badala ya utaratibu uliotumika 2010 wa kuteuliwa na Kamati kuu nasema hii njia inaweza saidia kwa sababu yaweza kuwa na faida zifuatazo;

  Mosi: Mtaitangaza zaidi CDM na kupitia hii kitu Itasaidia kwenye Kampeni za uchaguzi mkuu na kushinda kiurahisi
  Pili: Mtaondoa dhana ya kuwa CDM ni ya Kaskazini kwa kuwa mgombea Uraisi atakua amechagulia kitaifa.
  Tatu: Ikitokea mgombea aliyeshindwa akaondoka ndani ya CDM na kutoa malalamiko itakuwa rahisi mwanachama kumdharau na kufanya CDM yenye guvu zaidi.
  Nnne: Kupitia hii njia mtafanya wanachama kukipigania chama kwenye uchaguzi maana mgombea waliemchagua ni chaguo lao si La kamati kuu pekee.
  Tano: Huu mfumo utawasaidia zaidi watu wanaokijenga chama sasA Kupitia M4C kwa kuwa ndio wapo karibu zaidi na wananchi waliowengi na kuacha wale wasiotumia guvu zao kujenga chama wasiambulie kitu.

  Faida zipo nyingi japokuwa huu mtindo huwa unategemea zaidi uchaguzi usio na mizengwe mfano wagombea wanapita mkoa mmoja wanaomba kula kula zinapigwa zinahesabiwa na kutanganzw then wanahamia mkoa mwingine. Pia huu utaratibu unaweza kukubwa na mamluki wengi cha kufanya ni kuchukua idadi ya wanachana wa 2013 badala ya 2012.

  Baada ya kusema hayo naomba kuwasilisha na pia naomba idadi ya Wanachana wa CDM Tanzania ili tuone kama Majority Rule inaweza kuapply 2015.
   
 2. k

  kinai Senior Member

  #2
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wazo lakini linahitaji tafakuri ya kina
   
 3. Allen Kilewella

  Allen Kilewella Verified User

  #3
  Oct 19, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 7,357
  Likes Received: 10,315
  Trophy Points: 280
  Unazungumzia "Kura" au "Kula" Kama ni kula basi hicho chama ni lazima kiwe cha walaji!!
   
 4. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,252
  Likes Received: 1,194
  Trophy Points: 280
  wazo zuri,ngoja waje wenyewe
   
 5. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 482
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wazo zuri lakini lina hasara nyingi kuliko faida kumbuka kinachowaumiza magamba mpaka sasa ni kura ya maoni iliyofanyika 2010 ikaibua makundi na manung'uniko
  wakihamua tumia mbinu hii wabidi wawe makini mno kuepusha majeraha..
   
 6. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,092
  Likes Received: 11,229
  Trophy Points: 280
  huyo zitto yupo wapi? Anafanya nini? Simpendi hata kidogo huyu mtu.
   
 7. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,549
  Likes Received: 611
  Trophy Points: 280
  Sahau, CDM haiwezi kufanya mabadiriko yoyote 2015. Bado wamelala......
   
 8. p

  petrol JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Tujaribu kujikita kwenye mada badala ya kukurupuka. sasa hapa zito katokea wapi tena? Mtu katoa mawazo - yanaweza kuwa mazuri au vinginevyo. Busara ni kuyachambua. Tujitahidi kuwa wajenzi badala ya kubwabwaja tu ilimradi tuonekane tunachangia.
   
 9. M

  Magesi JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili nalo neno
   
 10. a

  amani uvumilivu njaa New Member

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii njia ni nzuri kweli ila inategemea idadi ya mamluki wa ccm
   
Loading...