Sokoro waito
JF-Expert Member
- Nov 21, 2014
- 2,201
- 2,598
Natumai hamjambo wadau!
Napenda leo tujuzane zaidi kuhusu maana na tofauti ya neno Urafiki na Mazoea katika Mahusiano ya mtu na mtu au mme na mke.
Neno Urafiki humaanisha ukaribu wa kushirikiana au kuhusiana katika mambo mbalimbali kwa maelewano mema sambamba na uaminifu wote bila hata malipo yoyote ya kifedha au vitu au kwa malipo yoyote ya kifedha au vitu.
Lakini neno Mazoea humaanisha ukaribu wa kufahamiana kwa juu juu kwa watu wawili na sio kujuana zaidi kuhusu maisha yao, japokuwa wanaweza kuwa mara kwa mara wana tabia ya kufanya jambo flani pamoja lakini hilo haliwafanyi kuwa marafiki hata kidogo.
Jambo la kushangaza ni kuwa wanadamu wengi siku hizi siyo MARAFIKI bali WATU WALIOZOEANA, yaani wanaishi kwa kupendelea mara kwa mara kufanya jambo flani kwa pamoja kwasababu flani lakini sio kwasababu ya urafiki.
Urafiki ni zaidi ya mazoea bali urafiki ni upendo, uaminifu, kusamehe, kujali, kuheshimu na sifa njema.
AINA ZA URAFIKI WA KALE:
Hapo zamani wazazi wetu walikuwa na namna walivyoanzisha urafiki, namna hizo ni kama ifuatavyo:
(a) Urafiki wa Heshima.
Watu wawili walikuwa wakiheshimiana kiasi cha kutosalitiana au kufanyiana jambo baya, urafiki huu mara nyingi ulikufa mara tu mhusika mmojawapo alipofariki, japokuwa uliweza kuendelea kama atatokea mtoto wa rafiki aliyefariki akataka auendeleze urafiki wa baba au mama yake.
Hatahivyo urafiki huu haukuzuia pande mbili kuoana.
(b) Urafiki wa Damu au Mafuta.
Huu ni urafiki wa ajabu mno maana wahusika wawili walipoanza na urafiki wa kuheshimiana kiasi cha kupatana na kujiridhisha kuwa hata familia zao zaweza kuwa marafiki bhasi wazazi hao wa familia mbili tofauti walinunua nyembe moja wakachanjana ngozi ili kutoa damu halafu mwingine pia huichukua hiyo nyembe kabla haijakauka damu ili kujichanja nayeye ili kuonyesha kuwa amekubali kuanzisha undugu wa damu kupitia urafiki huo.
Urafiki huu ulihusu familia hata ukoo pia, tena ulidumu vizazi hata vizazi ila haukuruhusu watoto au uzao wa familia hizo kuoana au kufanya ngono ya namna yoyote ile yaani kwa lugha nyingine waliheshimiana kama kaka na dada.
Hatahivyo ndugu hao wa kiume katika familia hizo waliweza kupelekeana mahari mara tu kijana wa familia moja alipotaka kuoa, yaani mshenga(kule mkoani Mara wanamuita Omotemeri).
Urafiki huu ni wa viapo hivyo ulikuwa hatari sana kama mmojawapo angekiuka masharti ya uaminifu.
(c) Urafiki wa mme na mke.
Wenzi wengi wa nyakati hizo walikuwa marafiki na sio watu wa kuzoeana ovyo ovyo, kwa lugha nyingine walijifunza kupendana baada ya kuoa au kuolewa, hii iliwasaidia kuwa marafiki waliovumilia shida, karaha na raha pia.
Wenzi hawa hawakuoana kwasababu wamezoeana bali kwasababu wameridhia kuishi pamoja hata kama ni kwa kulazimishwa ila waliaminiana kiasi cha kuwa marafiki.
AINA ZA URAFIKI WA SIKU HIZI;
(a) Urafiki wa sababu flani.
Hapa mjini usipokuwa makini wapo watu wana saikolojia ya kutaka urafiki hata kwa kulazimisha ilhali tu afaidike na kitu flani kutoka kwako, na baada ya hapo hutamuona tena akikukaribia.
Zipo ndoa kadhaa zimeanzishwa na urafiki wa namna hii ila hatari yake huja mara tu mmojawapo anapokosa kile alichokuwa akimendea kwa muda mrefu, kwa mfano pesa, mali, six packs, gari, nyumba, kazi nzuri, muonekano nakadhalika.
Urafiki huu siyo mzuri wa kuanzisha ndoa maana hakuna ajuae kesho kitakachompata hata kupoteza kile alichonacho leo.
(b) Urafiki wa mitandao.
Huu nao ni janga kubwa kwa kizazi chetu hiki, maana huwezi kutengeneza urafiki mzuri na mtu usiyemfahamu, hata ukifanya hivyo ujue unabahatisha tu, lakini ukweli ni kuwa marafiki wengi wa mitandao wamekuwa ni wababaishaji tu tena wanakuwa ni watu wanaopenda kuanzisha urafiki kwasababu ya upweke walionao katika maisha yao.
Haya tunayaita mazoea ya kuwasiliana kwa mitandao na siyo urafiki.
Ndoa nyingi zilizoanzishwa kwa urafiki huu hazina miisho mizuri.
(c) Urafiki wa mme na mke.
Aina hii ya urafiki ni kongwe mno, tangu enzi na enzi, kwa maana nyingine tunasema hata zamani walikuwapo marafiki wasaliti katika mahusiano au ndoa, kwa mfano DELILA msaliti aliyemsaliti SAMSONI(ukisoma biblia utafahamu zaidi) ila siku hizi watu wengi wanaoana wakiwa wamezoeana tu, baaada ya hapo wanazidisha mazoea tu tena wengine wakitembea njiani wameshikana mikono kana kwamba ni marafiki kumbe wamezoeana tu, ndiyo maana ikitokea changamoto kwenye familia nyingi ndipo utamjua mwenzio ni nani, yaani ni rafiki au adui.
Urafiki katika familia pia waweza jengwa kwa mazoea ya ukaribu wa kufahamiana na kuchukuliana katika mazuri na mabaya.
Ajabu iliyopo ni kuwa mme na mke ambao ni marafiki wa kweli huumia sana kiasi cha kushindwa hata kuoa au kuolewa mara mmojawapo anapofariki au hujitahidi kuoa kwasababu ya malezi ya watoto. Lakini kama walizoeana tu bhasi mwenzi aliyefiwa atasikitika ndani ya siku chache na kuanza kuzini ovyo ovyo.
Hata hivyo wanandoa wengi wameshindwa kuwa marafiki wa kweli badala yake wameishia kuzoeana kwa kulala pamoja tu.
kama wewe ni mchepukaji, Usiombe ukutane na wenzi ambao ni marafiki, hata ukimtongoza mke wake kwa mbinu gani utaambulia sifuri tu maana muunganiko wao ni imara kiroho(wana ulinzi wa kiroho) na kimwili, uaminifu kwao ni jambo la kawaida hata haliwapi shida kabisa.
Kwa kumalizia niseme tu kwamba wapo watu hapa duniani ambao wamekuwa ni marafiki wa nchi zao kiasi cha kutetea maslahi ya nchi zao kwa ujasiri wote, kwa mfano; Nelson Mandela, Kwame Nkurumah, Putin wa Russia, Fidel Castro wa Cuba, J.k Nyerere nakadhalika. Lakini wapo pia viongozi waliozoea madaraka hapa duniani wala hawana urafiki wowote na nchi zao, hawa nao ni wa kuepuka kama ugonjwa wa zika.
Jitathmini, je unalala pamoja na mwenzi wako kwasababu ya mazoea ya mme na mke au kwasababu ya urafiki wa mme na mke?